Kuna ubaya wowote kumchagua Kikwete awe Mfalme?

Lakini huyu Kikwete sijui tumemkosea nini sisis wa Tanzania! mtu hana uwezo wowote wa kutuongoza yaani hata watoto wanatambua hilo lakini anang'ang'ania tu...na hila ameisaha fanya sana tu ili awe raisi na aendelee.....
Kikwete tuache bwana, kama ni rekodi ya kuwa raisi kama Nyerere tayari umeipata...wako watu wengi tu wanauwezo wa kutuongoza vizuri na wewe unawajua na unashiriki kuwapiga vita!
Tuache,tuache!
(UWT najua mnasoma sana humu mkamwambie)
 
ufalme huu tuwape mara ngapi au unataka tuwatangaze rasmi tu? manake mambo yanayo fanywa na uongozi wa ccm kama sio ufalme basi sijui tuite nini.
 
Mara baada ya kuvikwa Taji la Ufalme, atalivua na kumgawia Mfalme Museveni wa EAC.
 
"If you cant beat them join them"
Tumeisha tengeneza mazingira ya Ufalme kwa Kikwete, sasa tuuhalalishe basi. Mimi nimemuona Mzee Mwanakijiji kama yule mtoto aliyekuwa anamwona Mfalme mpenda makuu na kupiga kilele kuwa hajavaa chochote! Mzee Mwanakijiji anapiga kelele kuwa kuna tatizo, na kama hilo tatizo halionekana basi tulikubali na kulihalalisha!
 
Haiwezekani kumchagua mtu yeyote awe mfalme kwani ufalme ni wa kurithishana!! so hata ingekuwa vizuri au vibaya, that wouldnt happen, unless Neno mfalme hapa lina maana nyingine
 
Mie naona sawa tu. Anaweza kuwa mfalme ila madaraka yake yawe wamepunguzwa. Kazi zote za kiserikali ziwe chini ya Waziri Mkuu kama ilivyo Spain, UK, Sweden, nk.

Ila wasiwasi wangu mie ni mmoja:
Watu kama Ruge, Makamba childrens, Kusaga etc yaani kwa ufupi Watoto wa MUJINI, wanaweza wakaja na mawazo yao mapya ya kumuingiza mfalme wetu mjini. Kibaya zaidi kinachoweza kutokea ni KUMNUNULIA vazi zito sana mfalme wetu, vazi ambalo hakuna mtu yeyote duniani ameshawahi kulivaa, vazi la bei mbaya sana. Vazi hilo, materials zake ni aghali sana, ila ni zuri mno, itabidi tulinunue hata kama ikibidi tule nyasi. Ili kuonyesha tofauti na mavazi mengine duniani, hili vazi litakuwa halionekani yaani Invisible.
Itakuwa furaha kumuona January Makamba na Ruge wakimvisha Mfalme wetu vazi lisiloonekana, na yeye akiendelea ku-smile. Huo mie ndiyo woga wangu maana watoto wa siku hizi, watamwaga radhi palepale.
 
Back
Top Bottom