Kuna tatizo gani uchaguzi usifanyike Jumapili?

Kumekuwa na idadi ndogo sana kwa Wapiga kura kujitokeza kwenye Uchaguzi kutokana na siku ya Kupiga kura kupangwa Jumapili.

Tangia Mwaka jana wapo Wanasiasa akiwepo Deus Kibamba alishauri Serikali kupitia Tume Ya Uchaguzi kupuka kupanga siku ya kupiga kura Jumapili na badala yake kupendekeza Jumatatu ambayo hakuna imani inayo athirika.

Sasa pamoja na juhudi hizi Serikali imekuwa Kiziwi na Uchaguzi mwaka huu upo Tarehe 25/10/2015 ambayo ina angukia siku ya Jumapili.

Maoni yangu mimi kwa wale ambao wanapinga uchaguzi kufanyika siku ya Jumapili wasije wakasusa mwaka huu badala yake nawashauri kwa dhati jitokezeni kwa wingi kujiandikisha kwenye BVR harafu tarehe 25/10/2015 achaeni kabisa ibada tumung'oe mkoloni!!

Nimefurahi sana msimamo huu kwa watu wa Kagera ambapo wameleta msiamiati wa kumung'a mkoloni

Hii mada imekaa kiudini udini futa delete kabisa mods
 
Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Mwanakondoo Ameshinda, Shaloom, Ndugu Wachungaji Katika Nchi Yetu Tunaelekea Katika Tukio Moja Kubwa, Tukio Hili Ni Tukio La Kihitoria Katika Nchi Yetu, Tunakwenda Kufanya Uchaguzi Wa Kuchagua Viongozi Mbalimbali Wa Nchi Hii, Nasema Ni Tukio La Kihistoria Kutokana Na Mwamko Wa Watu Tofauti Na Myaka Mingine, Tumeshuhudia Watu Wakilala Vituoni Kwa Ajili Yakuandikisha Ili Waweza Kupata Haki Yao Ya Kupiga Kura, Uchaguzi Huu Utafanyika Jpili, Ambayo Bila Shaka Ni Siku Ya Ibada, Ombi Langu Naomba Makanisa Nchi Nzima Yafanye Ibada Jmosi, Ili Kuwapa Nafas Waumini Ya Kupiga Kura, Ibada Hii Ya Jmosi Iwe Ya Maombi Mazito Ikiwemo Na Kukesha Kwa Ajili Ya Kuliombea Taifa Uchaguzi Uende Salama, Naami Mtalifanyia Kazi Ombi Hili
 
Kila dhehebu lina utaratibu wake ambao hautaathiri shughuli za uchaguzi. Kwa ushauri wangu ni kila dhehebu liangalie utaratibu mzuri ambao hautawanyima watanzania haki yao ya kikatiba. Ni suala la ndani zaidi. Pia suala la kuombea uchaguzi halitakiwi kuwa la siku bali hili tumeanza kuliombea siku nyingi na tunaendelea na Jumapili ya tar.25/10/15 tutaendelea kuomba ili Mungu adumishe amani Tanzania.
 
Kama mnashindwa kusamehe cku moja kila baada ya miaka mitano hiv waislamu watasemaje ikiwa wao kila wiki iendayo kwa mungu wanatakiwa kazini siku ya ijumaa siku ambayo pia wanatakiwa msikitini?
 
Watu wanashangaza kweli sioni ubaya kwa siku moja tu kwani wao ndo wanajua sana kusali

Hawa ndio wataleta vita kwa kuhoji vitu vidogo.

Wasabato jumamosi mapumziko.

Wakristo wote isipokuwa wasabato jumapili mapumziko.

Waislamu ijumaa wanaenda kazini na waajiri wengine hawatoi hata fursa kwa waislamu kwenda msikitini.

Hivi mtu unashindwa kuingia misa ya kwanza kisha saa tano uende kupiga kura? Au unashindwa kuanza kupiga kura kisha baadae uende kanisani?

Tusiingize nchi katika machafuko, tudai mambo yanayotujenga.
 
Back
Top Bottom