Kuna takwimu juu ya hili!?

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Nilipokuwa nasoma Kenya kuna kipindi walitoa takwimu kuhusu waume kupigwa na wake zao.
Kama sijasahau, it was an alarming 43% in the lake zone!
Sasa jana kuna jambo lililotokea;
Nikiwa naenda kumchukua dada yangu saluni maeneo ya kijichi-mbagala,
niko nje kwenye ka-restaurant napata soda yangu nikingoja wamalize. Kwa pembeni
amekaa mbaba mmoja na binti wanapiga stori zao.
Mara ghafla akaja mkewe yule baba akaanza kumfokea,
"Unafanya nini na huyu mwanamke hapa?"
mara, "Haya nikukute nyumbani sasa hivi!"
Mume akalalama kiasi, "sasa unataka kuaibishana hadi huku"
Mke wake akamjibu mara ya pili na ya mwisho, "Sitaki maneno, ondoka sasa hivi nikukute nyumbani!"
Yule bwana kwa unyonge kabisa akanyanyuka tena bila hata kuaga akaenda zake...

Nikabaki najiuliza, hivi hata huku Tanzania kuna wabongo wanaonewa na wake zao namna hii? Kupigwa je?
are there any statistics of such things?
Maana kule Kenya, ilibidi na wababa wanaopigwa na wake zao wajitokeze nao kutaka kusaidiwa....huku vipi? ama hali haijawa tete bado? ama ni kuvumiliana ktk harakati za kudumisha amani?
 
Sina data za bongo, ila ubaunsa upo saana tu, hatusemi
 
Kwa hiyo wabongo ni waoga ama ndo uvumilivu wetu watanzania?
 
Sasa huyo baba anaonewa au anakumbushwa tu wajibu wake wa kuwepo nyumbani kwa muda huo?!
 
Sasa huyo baba anaonewa au anakumbushwa tu wajibu wake wa kuwepo nyumbani kwa muda huo?!

Kha! kama ningeweza kuandika hiyo discussion na sauti zake ungeelewa. Jamaa anagombezwa kabisa na mke wake. Halafu baada ya jamaa kwenda mkewe akalianzisha na yule binti aliyekuwa anaongea na mumewe.
Jamani, kukumbushana gani huku!??
 
Kha! kama ningeweza kuandika hiyo discussion na sauti zake ungeelewa. Jamaa anagombezwa kabisa na mke wake. Halafu baada ya jamaa kwenda mkewe akalianzisha na yule binti aliyekuwa anaongea na mumewe.Jamani, kukumbushana gani huku!??
Mbona wanaume hua wanawakumbusha wanawake kwa style hiyo?!Tena na makofi juu!
 
Mbona wanaume hua wanawakumbusha wanawake kwa style hiyo?!Tena na makofi juu!

lol! wanawake wagumu kuelewa,lol!
n'way, hilo limefahamika tangu siku nyingi and it's being dealt with through various organizations and women bodies.
Tatizo ni hili la wanaume?! is it that serious tuliundie tume ama bado ni mmoja mmoja sana!??
 
lol! wanawake wagumu kuelewa,lol!n'way, hilo limefahamika tangu siku nyingi and it's being dealt with through various organizations and women bodies.Tatizo ni hili la wanaume?! is it that serious tuliundie tume ama bado ni mmoja mmoja sana!??
Ngoja nikuulize swali ambalo jibu lako litajibu swali lako!Ingekua ni wewe ungependa kuwe na sehemu uende ukalalamike?!
 
wanawake wa bongo wana heshima za kukera nakumbuka babangu alikuwa anajifanya kidume sana cha kumponda mamangu nikadhani hawezi kujiteta kumbe alikuwa anamuheshimu,siku alipomuonyesha yeye nani alikoma kuringa....kwa hiyo kupigwa inawezekana ila mnaheshimiwa tu!
 
Ngoja nikuulize swali ambalo jibu lako litajibu swali lako!Ingekua ni wewe ungependa kuwe na sehemu uende ukalalamike?!

Kwanza hata katika kusadikika hilio haliwezekani!!!

Pili, tuassume ndiyo...kama kuonewa huku kumezidi kweli mimi ndo ningekuwa mwenyekiti wa chama hiki..Chama cha wanaume wanaopigwa na wake zao Tanzania,lol!

NO WAY..kweli ningeumia kindanindani tu...

btw, do u min to tell me hili suala linaweza kuwa that serious bongo hii!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom