Kuna siri nzito kwenye Deni la Taifa

wakuu mnakumbuka shuka kumekucha.............ila ufujaji wa kodi ztu ni mkubwa mno,haviniingii akilini
hata kidogo kwamba kuna Bilion moja wamelipwa wafanyakazi hewa,hivi ni wepi hawa ?hatuwajui kweli?tumewalipaje?
kwani pesa zao zimeingia katika acount gani?.
Kwani tumeshajiuliza tangu bwana mkubwa aingie madarakani amesafiri nje ya nchi ni marangapi?hadi leo na kila safari iligharimu kiasi gani?.
kuna sababu gani za kimsingi kutoa misamaha ya kodi,je ni kampuni gani na za nani zilifutiwa madeni na sababu zilizopelekea,

Hili tatizo la "Wafanyakazi hewa" Serikalini ni la miaka mingi sasa lakini hakuna hatua zozote zile zinazofanywa na Serikali ili kudhibiti huo wizi wa miaka nenda miaka rudi. Wameliacha liendelee kwa miaka yote hiii ili waendelee kupata mianya ya kuibia walipa kodi.
 
Tatmini nzuri, na maswali uliyoyauliza ni ya msingi sana, tatizo la madeni tuliyo nayo pesa nyingi zimeingia kwenye matumizi badala ya uzalishaji, na hiyo inatosha kufanya deni lizidi kukua.
 
Yeah Siri iliopo ni kuwa WORLD BANK na IMF walisubiri Mpaka Nyerere akajiuzulu wakaanza kuwatisha Mwinyi na Mkapa kuwa nchi yenu itaanguka kwa madeni kama hatagawa hayo madini yenu kwa mataifa ya Magharibi, ili tu kuweza kulipa Madeni na sio kumaliza kulipa Madeni

Angalia Makampuni ya kigeni yakaja tukawapa GOLD with 100% sisi tukaambulia taxes, na hazitoshi, Botswana wao wanapata 40% ya Madini yao na hawana Deni IMF or WORLD BANK

Sasa hatujui Deni letu likoje huko Wamebeba Dhahabu, Almasi, Tanzanite na Madini Mengine Mengi hatuna Idadi yana Gharama Ghani haturuhusiwi kuangalia Mifukoni wanabeba nini, Tunawomba wajenge Barabara Wanagoma, Shule wanakataa, Hospitali wanasema haiwasaidii...

We are back to NEO-COLONIALISM they please the few leaders wao wana kila kitu na watoto wao; watoto wao wanaanza kugombea Ubunge wazazi wamezeeka, back to the same route

LINI DENI LIALIPWA... WE NEED CHANGE
 
Tunakopa adi tufikishe 50 trilioni afu tunawapa CDM inchi tuone watafanyeje.

Kama na wewe wanakugawia hongera kwa ujinga, sijuwi kama unafaidi ufisadi huo na wale ndugu zako wanaotaabika vijijini.

a)
- Hawana elimu bora, afya wala maisha bora
-Hawana uhakika wa kesho yao itakuwaje

b) Utamwachia nani deni la Tril 50, wewe, baba na jamaa yako mtaishi wapi uk, uSA au hapapa? tafakari

Kumbuka unapojadili jambo kwa ushabiki unajifedhehesha na zaidi unawafedhehesha wale wote wanaokutegemea uwakomboe ili siku zijazo wapate haki ya msingi katika mgao wa keki ya taifa.

Nakama wewe ni masikini kama mimi sijui tuendako, maana wewe, mimi watoto wetu na vitukuu vyetu tutashiriki kukamuliwa kulipia matumbo ya unaowatetea kwa ujinga na ushabi.

-
 
Yeah Siri iliopo ni kuwa WORLD BANK na IMF walisubiri Mpaka Nyerere akajiuzulu wakaanza kuwatisha Mwinyi na Mkapa kuwa nchi yenu itaanguka kwa madeni kama hatagawa hayo madini yenu kwa mataifa ya Magharibi, ili tu kuweza kulipa Madeni na sio kumaliza kulipa Madeni

Angalia Makampuni ya kigeni yakaja tukawapa GOLD with 100% sisi tukaambulia taxes, na hazitoshi, Botswana wao wanapata 40% ya Madini yao na hawana Deni IMF or WORLD BANK

Sasa hatujui Deni letu likoje huko Wamebeba Dhahabu, Almasi, Tanzanite na Madini Mengine Mengi hatuna Idadi yana Gharama Ghani haturuhusiwi kuangalia Mifukoni wanabeba nini, Tunawomba wajenge Barabara Wanagoma, Shule wanakataa, Hospitali wanasema haiwasaidii...

We are back to NEO-COLONIALISM they please the few leaders wao wana kila kitu na watoto wao; watoto wao wanaanza kugombea Ubunge wazazi wamezeeka, back to the same route

LINI DENI LIALIPWA... WE NEED CHANGE

Hakutishwa mtu bana ni upumbavu wao tu hawa akina Mwinyi na Mkapa ambao waliamua kuyafanyia kazi mapendekezo mbali mbali ya IMF na WB bila kutathmini kwa kina athari zake kwa Watanzania. Kama wangeamua kuyatahmini kwa kina na kuweka maslahi ya nchi mbele basi kamwe wasingeyakubali. WB na IMF wasingeweza kuifanya chochote Tanzania kama Mwinyi na Mkapa wangeyakataa mapendekezo yao mbali mbali ikiwemo kushusha thamani ya shilingi, kuuza mashirika mbali mbali ya umma na pia kuwakaribisha nchini "wachukuaji" wenyewe akina Mkapa na Mwinyi na sasa Kikwete huwaita wawekezaji pamoja na kuwa hakuna chochote wanachowekeza.
 
Hasira sana. Malipo ya wafanyakazi hewa ni mtandao wa mafisadi moja ya njia ya kukusanya mapato yao kila halmashauri lazima iwe na wafanyakazi hewa kadhaa. Kuhusu deni la taifa kuongezeka kwa kipindi kifupi na misamaha ya kodi kwa vigogo,wafanyabiashara wakubwa makada wa ccm,madini na rasimali nyingi za taifa zinafunywa. Safari za jk na mwendazake nje ya nchi ukiuliza safari moja tu walitumia kiasi gani utaambiwa ni siri ya magogoni na ni kodi yetu. C.A.G hana cha kutusaidia hiyo ripoti kabla kupelekwa bungeni jk kaisoma na kupitisha safi wadanganyika hao kawape hiyo. Tusaidiane kutoa hii taaluma humu kwa watu wengine huko tunakoishi kwa mabadiliko yajayo hawa magamba watatulisha nyasi mapema tu. Raisi ana ndege ATCL haina ndege na wafanyakazi wanalipwa mishahara lazima deni liongezeke na bado. Nashukuru.
 
Samahani wanajamvi,mie naomba sie watu wa Mtwara tusiusishwe na hilo deni,kwani hatukushirikishwa wakati wa kukopa wala kutumia hiyo Pesa.
Tena nyie ndo mkae kimya maana CCM/JK ndipo Wanapovunia kura huko.
 
MKUU tanzania is borrowing to consume,.....unacheza na Mh wa kutumbua!
 
hiyo deni ni ukimwi wa taifa, it will never be cured in the vnear future, na mfumo tulio nao.

just creating vicious cycle of depedency, kukopa kulipa deni!!
 
Jiulize hii pesa imetumikaje?
534975_289835637761970_100002066077119_675573_2046081357_n.jpg
 
Kuna uongo katika vipimo noti ya 10,000.00 haina urefu wa 15cm na upana wa 7.5cm.

Ila deni ni kweli 14.4tril. Nji haina hela deni linazidi kuongezeka tu. Hapo sasa.
 
asante sana mkuu 'black bat' kwa kufanya illustration ambayo nadhani hata Mtanzania aliyeko huku kwetu ataweza kuelewa ni nini nchi inadaiwa.

Na pia nashukuru kwa kuweka swali la msingi ambalo hatuna budi kujiuliza yaani hizi pesa zilitumikaje!

My take:
nadhani ile trillion 3 ya mheshimiwa mmoja inaweza kuwa inawakilisha asilimia ndogo tu za kilichofichwa lakini badala ya kuanza na tusivyovijua tuanze na hiyo irudishwe kwanza ili deni libaki trillion 11.4.
Huu utakuwa muda mzuri zaidi kwenye historia ya nchi hii isiyokuwa na mwelekeo kupata mwelekeo
 
Swali kubwa ZIMETUMIKAJE
Kama kuna mwenye taarifa atuambie zimetumikaje na ni watanzania wangapi wamefaidika na hilo deni ambalo tumekopa
Maana tusiendelee kusema deni la taifa wakati mzee wa pale Njenjenkuru Lindi hana dawa hospital, shule yake kwa watoto wake haina madawati wala vitabu wala majengo ya madarasa na hana uhakika wa kula siku ya leo
 
shimbo rudisha 3tr.ina maana uwekezaji ktk gas na madini hau ingizi pesa bali unatoa pesa!kilimo kwanza nacho kinakula
 
asante sana mkuu 'black bat' kwa kufanya illustration ambayo nadhani hata Mtanzania aliyeko huku kwetu ataweza kuelewa ni nini nchi inadaiwa.

Na pia nashukuru kwa kuweka swali la msingi ambalo hatuna budi kujiuliza yaani hizi pesa zilitumikaje!

My take:
nadhani ile trillion 3 ya mheshimiwa mmoja inaweza kuwa inawakilisha asilimia ndogo tu za kilichofichwa lakini badala ya kuanza na tusivyovijua tuanze na hiyo irudishwe kwanza ili deni libaki trillion 11.4.
Huu utakuwa muda mzuri zaidi kwenye historia ya nchi hii isiyokuwa na mwelekeo kupata mwelekeo
tatizo zile benki za southafrica zitakubali kuiachia ile pesa?
 
Usikute hawa viongozi wetu hawajui implication ya kukua kwa Deni la Taifa.
Maana itafika kipindi tutakuwa hatukopesheki kwa madeni kila kona tena ya kujitakia bse hayana impact kwa uchumi wetu.
Kama walichukua kujenga roads mbona roads nyingi zimesimama kujengwa kisa ela?
Kama ni kulipa salaries mbona kuna watu it takes time kupata salaries
 
shimbo rudisha 3tr.ina maana uwekezaji ktk gas na madini hau ingizi pesa bali unatoa pesa!kilimo kwanza nacho kinakula
Si za Shimbo, Ungesema Kikwete rudisha Tr3.
Ni sawa na kusema Ridhiwani anamiliki 60% ya Afghem Tanzanite wakati ni Kikwete.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom