Kuna siri gani kwenye ulimwengu wa kiroho ukilala chali?

Naomba unieleze mambo yafuatayo kwann yanatokea wakati mtu amelala chalii tu

i. Kufikiri kwa makini na kulala chalii

ii. Kupumzisha mwili(relaxing) na kulala chali.

iii. Ndoto za ajabu mfano kupaa,kupambana na wanyama,mauaji na kulala chali.

iv. Majinamizi(kujiskia km vke unanyongwa unapoteza pumzi) wakati umelala chali..

v. Kutoka nje ya mwili(astral projection) wakati mtu amelala chali.

vi. Mtu akifa analazwa chali.

Pia je mtu anapolala chali ubongo huwa anajisogea kwenda nyumaa toka utosini?
Nenda hraka hospitali, una malaria mwilini!!
 
In short, kutokana na hali ya utulivu katika mwili, utokanao na kulala chali, inapelekea your spirit to be active than your fresh, halii inakupelekea kuingia kwenye ulimwengu wa roho, unapo ingia kwenye ulimwengu wa roho huku ukiwa hauna nguvu za kiroho matokeo yake ndio kukimbizwa na wanyama au hatahata kupambana na roho chafu zinazo lingana nguvu na wewe.

Kumbuka kila mnyama ana maana yake unapo muona katika roho. Kwa kuongeza kuna baadhi ya vyakula ukila roho yako inakua active, na baadhi ya milalo inawe kukusaidia kua active katika roho. Na kuna namna ya kujua matukio yanayo endelea katika eneo ulilopo. Kuna mengi sana, hapa natumia simu napata tabu kuandika
Duuh
 
Unapolala chali ulimi unarudi nyuma hivyo kupunguza ukubwa wa njia ya hewa. Hali hii husababisha ubongo kukosa oksijeni ya kutosha hivyo kupata maluweluwe.
Nimelipenda hli jibu,
Liko kisayans zaid
 
Mm sio kulala chali tu
Kuna upande wa kitanda nkilala nkiwa nimeeka kichwa huwa naota ndoto za ajabu ajabu tu
Lkn upande mwngne hua tofaut
 
Naomba unieleze mambo yafuatayo kwann yanatokea wakati mtu amelala chalii tu

i. Kufikiri kwa makini na kulala chalii

ii. Kupumzisha mwili(relaxing) na kulala chali.

iii. Ndoto za ajabu mfano kupaa,kupambana na wanyama,mauaji na kulala chali.

iv. Majinamizi(kujiskia km vke unanyongwa unapoteza pumzi) wakati umelala chali..

v. Kutoka nje ya mwili(astral projection) wakati mtu amelala chali.

vi. Mtu akifa analazwa chali.

Pia je mtu anapolala chali ubongo huwa anajisogea kwenda nyumaa toka utosini?

Aisee Bujibuji inawezekana hii kitu ina ukweli wake mkuu. Ni siku nyingi najiuliza ila sipati jibu tena itabidi nimuulize na mshana jr hii kitu. Ni hivi, nikitongozwa na msichana au msichana akijipendekeza kwangu lazima nitamuota tu usiku anakuja katika ujio wa kichangudoa/bongo muvi, haswa nilalapo chali na kuanza kutafakari yaliyonisibu kwa ile siku. P.S. Sipendi machangu wala mademu wa bongo muvi.
 
Unapolala chali ulimi unarudi nyuma hivyo kupunguza ukubwa wa njia ya hewa. Hali hii husababisha ubongo kukosa oksijeni ya kutosha hivyo kupata maluweluwe.
Hahahaaa! Wana Sayansi mnaponiachaga hoi!
 
Hii hali hata mimi naota nakabwaa halafu nakosa nguvu za kujiondoa. Nikilala tofauti hakuna tatizo mpaka sasa silali chali hata iwe vipi ni ubavu tu
 
sasa tule chakula gani kizuri usiku?

Hujanielewa, nazungumzia nafsi yangu. Nimegundua kama nikila kuku roast ama mishikaki na sahani mbili za pilau uwa nalala vizuri kabisa ila nakuwa mbaguzi katika ndoto zangu. Nikiota niko na mwarabu, muhindi ama mzungu mara nyingi nahamka na hasira na sipendi kukutana na hao watu njiani.
 
Mimi nikilala chali, naota naingiliwa kimwili....na nikijipapasa nakutana na hali fulani ya umajimaji....

Sielewi!!!
Daa ! Hahaha ! Pole sana !

Lakini ukifikilia kwa njia ya kisayansi zaidi , ukilala chali , njia ya hewa hupungua kutokana na partial obstruction kutokana na ulimi kuanguka nyuma haswa ukiwa katika deep sleep ! Hii inaweza kuletea kupungua kwa oxygen towards the brain ni hivyo ku mimic asphyxiation ( lack of oxygen due to strangulation)! Kinachofuata sasa ! Kuna mwingine anapata jinamizi kama tulivyozoea kuita , lakini pia , kuna watu wakipata asphyxia hufikia mshindo ! Sio uncommon watu wanapo nyongwa ku climax kama vile alikuwa anafanya mambo ya wakubwa na pia wapo ambao huwataka partner zao wawakabe shingo ili wakamu ! So Madame B inawezekana kabisa wewe hupata sexual stimulation kutokana na upungufu wa oxygen ! Mind you , sio lazima iwe hivyo ila nawaza kwa sauti !
 
Utafiti wako ni fake na ni Jibu! Ukita chali haiwezekani pua inangalie juu kana kwamba hujasinzia; lazima kichwa kidondoke kulia au kushoto
 
In short, kutokana na hali ya utulivu katika mwili, utokanao na kulala chali, inapelekea your spirit to be active than your fresh, halii inakupelekea kuingia kwenye ulimwengu wa roho, unapo ingia kwenye ulimwengu wa roho huku ukiwa hauna nguvu za kiroho matokeo yake ndio kukimbizwa na wanyama au hatahata kupambana na roho chafu zinazo lingana nguvu na wewe.

Kumbuka kila mnyama ana maana yake unapo muona katika roho. Kwa kuongeza kuna baadhi ya vyakula ukila roho yako inakua active, na baadhi ya milalo inawe kukusaidia kua active katika roho. Na kuna namna ya kujua matukio yanayo endelea katika eneo ulilopo. Kuna mengi sana, hapa natumia simu napata tabu kuandika
Aimee umedadavua vizuri. Ukiweza kuandika kwa computer funguka basi zaidi.
 
Utafiti wako ni fake na ni Jibu! Ukita chali haiwezekani pua inangalie juu kana kwamba hujasinzia; lazima kichwa kidondoke kulia au kushoto

Mkubwa !

Asante kwa comment yako !
Kwanza nikuambie ! Haya si majibu ya utafiti wala sijakuambia nimefanya utafiti !
Nilichokisema nikutokana na knowledge ndogo niliyonayo kuhusu mwili wa binadama na sijafikia level hiyo uisemayo ya utafiti ! Siku ingine soma vizuri na usome katikati ya mistari ili utoe comment zenye kueleweka na kuelimisha !

Nimejaribu ku hypothesize kutokana na ninachokijua bro ! Lakini pia si kweli ni lazima ukilala basi shingo itawnda upande ingawa pia hutokea ! Likewise, kwa vyovyote vile , ukiwauliza walio toa au kuchangia bandiko hili , sio mara zote ukilala chali basi yatakutokea hayo yaliyosemwa ! Sasa kama unahusisha ubongo wako vizuri na ya GT wengine , basi utaona kuwa labda mantiki ktk comment yako ipo , na pia kwangu ipo ! Lakini pia nilitoa angalizo ktk comment yangu kuwa ninafikilia kwa sauti na si kwamba ndio jibu kamili kwa madame B ! And pls utafiti sio jambo dogo na haliwezi fanyika kwa siku moja , isipokuwa mawazo kama hilo langu ndio huzaa tafiti !

Sasa challange kwako , unayo reference au umefanya tafiti yoyote kuonyesha ni lazima shingo iende upande ukilala au ni vipi mkubwa ! Karibu sana kwa majadiliano
 
Mwalimu ethical nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa ila na haya pia nahisi wanafunzi wako wanapaswa kuyafahamu:

1.ndoto hazikwepeki ziwe ni nzuri ama mbaya lazima ziwepo maana wakati mwingine hata Mungu amekuwa akiongea na watu kupitia ndoto.lazima tuote

2. Binadamu ni roho ni kweli mwili ukiwa umelala roho inapiga mzigo kama kawa na ndio hapo panakuwa na mapambano kama ilivyo katika mwili,mapambano hayaishi.

3. Kwavile roho hailali ni dhahiri baadhi ya milalo kama kulala chali kunafanya damu isizunguke vizuri,hivyo roho lazima itafute namna ya kukuamsha ili uweke mambo sawa.hapo hata ndoto mbaya roho inaweza ikakuletea.

4. Wakati mwingine ndoto mbaya huletwa na vitu vilivyojazwa katika akili zetu,unawaza nini siku nzima.ukiangalia sinema za kutisha kabla ya kulala,kupata shambulizi usiku ni kawaida.hapo huitaji damu ya Yesu,unahitaji kubadili mwelekeo.

5. Mwisho ni kweli vita ya kiroho ili ushinde unahitaji nguvu za kimungu.

Hayo ndio mawazo yangu.

Asubuhi njema.
Mm ilikuwa kila nikilala huku nimevaa socks lazima nishikwe na jinamizi. Kila nikilalia mto mgumu kiasi shingo ikapinda ni lazima nishikwe na jinamizi. Mwanzoni nilikuwa nadhani ni uchawi ila baadaye nikaja kugundua kuwa si uchawi maana nikilala bila kuvaa socks sipatwi na jinamizi! Kimsingi niligundua kuwa roho zetu huwa zinatafuta mbinu ya kutuamsha kama tumelala vibaya ili tuweze kulala vzuri. Roho ili ikuamshe inatumia mbinu nyingi ikiwemo kukuletea hali ya kushikwa na jinamizi, kukuotesha ndoto ambayo itakupelekea upate taabu hadi ustuke n.k.
Pamoja na yote, kuna ndoto za kutoka kwa Mwenyezi MUNGU, za kutoka kwa sherani na ndoto za shughuli nyingi na ndoto ya kulala vibaya au ndoto ya shambulio la kimwili. Ni vyema mtu ukajifunza kutofautisha ndoto hizi.
 
Mimi Niseme Hivi:
Wakati Mtu Uote Ndoto Mbaya Ni Pale Ambapo Unakuwa Umeover Dose Mwili Wako Au Kauli Ya Kueleweka Unaushughulisha Mwili Wako Hali Ya Kuwa Ni Muda Wa Kulala Lazima Utakutana Na Vitu Kama hivi:

1:Kumwaga machozi hovyo

2:Udenda,

3:Kuongea hovyo usingizini

4: kunigwa na jinamizi

5: kuweweseka usingizini

6: kuamka na kutembea hali ya kuwa umelala

7: kukimbizwa na watu

8: kudumbukia Shimoni

9: kumwaga mbegu na tupu kuuma sana wakati wa kumwaga

10: Kuota Ndoto Mbaya...

Haya Husababishwa na mambo yafuatayo..

1: kulala kama shetani bila kujua mungu yupo..

2: kula chakula kingi muda wa kulala saa nne usiku na kuendelea..

3: mazingira ya kulala

4: mtindo wa kulala... au pozi...

Hapa Mnachokiandama nyinyi ni mtindo wa kulala na mmelenga mtindo mmoja tu basi na mimi nitaqafungukia kwenye mtindo huo huo...

kwanza kabisa kuna kulala chali kwa aina zaidi ya sita

1: kulala chali huku makwapa yapo juu (mbaya)

2: kulala chali mikono kifuani (mbaya)

3: kulala chali mikono kwenye uchi (mbaya)

4: kulala chali shingoni upande (mbaya)

5: kulala chali miguu umekunja (mbaya)

6: kulala chali huku mikono imenyooka sahihi (nzuri)

isipokuwa nayo ukikosa position ya kichwa sio nzuri...

mfano: mto mkubwa (utaota jinamizi) na mto mdogo wa kubinua kichwa (utaota unakimbizwa)

mto straight ndoto njema, astral projection,lucid dreams na kujikinga na maumivu ya mgongo......

unapolala chali damu inapita kila kona ya mwili na unapojikunja inakwama...

mfano hapo ulipoangalia juu utahisi tofauti angalia kifua chako utahisi unakabwa sasa pindi unapojikaba utakereka kama unanigwa ambayo hupelekea ubongo kukuletea ndoto ya jinamizi
na sidhani kama kuna mtu alishawahi kutoka kwenye ndoto ya jinamizi akaendelea kulala chali.... vile vile mf: chakula kikizidi tumboni na kinahitajika kusagwa utaota unadondoka,kimbizwa,simba n.k mradi tu mwili usage kwanza ile chakula...

kuna mwenye swali labda?
Hii fact, nyingine nyingi ni porojo
 
Back
Top Bottom