Kuna siri gani kati ya Polisi na wezi wa spea za magari Ilala gerezanii?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Katika jambo ambalolimekuwa likiumiza vichwa vya watu wengi nchini ni kuwa inakuwaje mtu anapoibiwa kifaa cha gari yake anaambiwa aende mtaa wa Gerezani Ilala atavikuta vitu vyake. Na anapokwenda kweli hukuta vifaa vilivyoibwa na kuvinunua upya.

Hivi kweli hapo bado tunasema nchi hii ina askari polisi? Au polisi yetu ni kwa ajili ya kuzuia maanadamano ya CHADEMA tu? Hivi ni nani ambayehajasikia ushenzi huu unaofanywa na wezi hao? Ninalazimika kuamini kuwa Polisi wetu kuanzia kwa IGP wanajua kabisa ushenzi huu ila kuna masilahi wanayoyapata. Haingii akilini kuibiwa maliyako na siku moja baadae unaenda kuuziwa mali hiyohiyo huku serikali ipo.

Watu wanaposema wamechoshwa na ushenzi huu mnasema wametumwa na CHADEMA. Hivi kweli serikali inashindwa kutokomeza genge hili? Ni bora mkatangaza kuwa hakuna jeshi la Polisi na kila mtu ajilinde kivyake. Huu ni upuuzi!!!!

Najua kesi kama hizi zimewapata wadau wengi na wamekuwa wakiugulia machungu kimyakimya.
 
Hili tatizo liko hapo Dar muda mrefu sana na hakuna IGP wala RPC aliyewahi kulishughulikia. Anayeshangaza zaidi ni Kova pamoja na kujitutumua kuwa anakamata majambazi lakini anataka kutuambia halijui hilo?
Mambo mengine unakuta ni hao hao Polisi .....?
 
Hii ndio overtime ya Polisi Kuchukua extra Income!! Wanafahamu yote haya ila hawana nia ya dhati Kuyazuia Haya yasitokee!! Kova ndio Hivyo tena yupo studio anakamilisha single yake (Part 2) sasa unategemea nini Zaidi? Na Kwa taarifa yako matukio ya ujambazi wa kutumia silaha sasa yameongezeka na yapo Juu sana!! na hakuna polisi anayejali!! Sasa sijui tukimbilie wapi?
 
si wauza spea za wizi tu, hata wauza madawa ya kulevya, wauza bangi na wakwepa kodi ,POLISI inawajua ila ukiwa ccm mkuu hata kama unanunua vya wizi hukamatwi. UKITAKA MAMBO YAKO YAKUNYOOKEE HAMIA CCM!
 
Hicho kitu huwa alwayz najiuliza. Why????? Tanzania why???? Nashauri vipuri vya magari used is better vikauzwa na maangent maarumu na wasiwe wengi, from here followup ya wezi hawa itakuwa lahisi. Nasema na nitarudia kusema Police wa nchi hii wengi wao wanauwezo mdogo sana kazi yao nikutmia nguvu na si akiri, looking on this ni bora tukajilinda wenyewe. Kamata mwizi ua
 
Wanakula kamisheni hawa Polisi! Rushwa, rushwa, rushwa, nchi hii inanuka rushwa!
 
Back
Top Bottom