Kuna sheria yoyote ya kudhibiti ufugaji holela kwenye maeneo ya makazi?

Cyan6

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,531
1,205
Napata shida na Jirani yangu, anayefuga kuku wa kienyeji na kuwaacha huru wakizunguka mtaa mzima na kuharibu bustani za majani, miti, maua na uharibifu mkubwa wa mazingira! Nimemsihi awafungie ndani ya uzio wake lakini imeshindikana. Nichukue hatua gani? Naomba msaada!
 
Ukiwa unasubiria ushauri wa kisheria hebu nunua manati kwanza! Wakitokeza tu unawaponda vichwa! Ukilenga wawili watatu mwenyewe atawafungia tuu! jirani yangu shamba alikuwa na mchezo huo nikaweka fencing wire bado akawa anachokonoa wire ili kuku wake wapite kwa chini..siku moja nilikwenda shamba na mbwa nikawaachia wakafaniwa kuuwa watano mbele ya wanae....hajarudia tena!
 
Hahaaa umenichekesha mkuu! Yangu ni tofauti kidogo. Ni makazi na si shamba. Na kila mmoja wetu ana uzio wa ukuta! nje ya ukuta kuna eneo la kuzunguka plot ambapo nimepanda loans(majani) maua na miti ya kivuli kuhifadhi mazingira!
Sasa utata ndiyo upo katika eneo hilo, kwa maana yeye anawaacha kuku wanatoka ndani ya uzio na kuzurura mtaani na kuharibu mazingira yetu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom