Kuna sababu gani ya kuendelea na kikao cha bunge?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,758
12,174
Ukifuatilia mijadala ya bunge kuhusu bajeti ya serikali na hoja ya waziri mkuu utagundua kuwa miradi mingi iliyopangwa miaka mitatu iliyopita ama haijatekelezwa au haijaanza kabisa!

Ushauri wangu ni kuwa wabunge waamue kusitisha mijadala ya wizara nyingine zote na kuiagiza serikali kuendelea utekelezaji wa miradi iliyopangwa miaka iliyopita badala ya kuanza kujadili miradi mipya! Hii itaokoa muda na fedha kujadili miradi isiyo tekelezeka!

Tafakari!
 
Hata wanavyojadili haina maana kabisa yaani spika sijui anaharaka ya nini wakati kila siku mamabo yale yale eti kuna mambo waziri anasema kwa ajili ya muda atayaeleza baadae

maoni yangu kwa nini wasizungumze swala moja week nzima wakalimaliza kwa mfano leo nimesikia tan power wamekopa nssf billion alafu hio inakuwa ni deni la taifa maana hio hata mimi na wewe tutalipa wakati mkapa kala
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom