Kuna saa unaweza usijisifie kuwa Mtanzania

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Kuna wakati mwingine huwa najisikia vibaya sana kujivunia Utanzania wangu! Kwenye macho ya wengi huwa tunaonekana watu wenye amani sana! Kiukweli sivyo!
Nimeangalia ITV leo kule Meatu! Askari anapiga watu mabomu anawasha kibiriti kuchoma nyumba ya mtanzania mwenzake huku wamekamata AK47 as if wale ni waasi wa kivita! Yet we are saying nchi ya amani. Hivi wale Watanzania wamependa kukaa kule porini jamani. RC, DC na viongozi wa Shinyanga na Meatu wameenda kufanya nini kule? Kukaa maofisini na kucheza karata kwenye computer tu! Siku hawa wahanga wakiamua kukataa manyanyaso wanayoyapata toka serikali yao mtasema waasi?
Tuwe na huruma na wenzetu.
Iko siku moja hawa watu wataadhibiwa ama kukutana na gadhabu ya Mungu kwa kuwatesa viunbe wake
 
Back
Top Bottom