Kuna njama za kuwachafua zaidi Karamagi, Msabaha

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Kuna njama za kuwachafua zaidi Karamagi, Msabaha
Peter Nyanje

KWA mantiki ya kawaida, choki huwa safi baada ya kuoshwa kwa maji safi. Chombo kilicho safi, iwapo kitaoshwa na maji machafu, basi matokeo yake chombo hicho huambukizwa uchagu kutoka katika maji yaliyotumika kukioshea. Hatimaye, chombo hicho nacho huchafuka.

Kama chombo ni kichafu, halafu kikaoshwa na maji machafu, uwezekano mkubwa ni kuwa uchafu wa chombo unaweza kuondoshwa, lakini uchafu wa maji machafu ukabaki katika chombo, hivyo kukifanya chombo hicho kiendelee kuwa kichafu.

Kwa mantiki hiyo, ili chombo kiwe kisafi kikioshwa na maji machafu, huishia kuwa kichafu.

Haya ndiyo serikali inayotaka kuyafanya kwa waliowahi kuwa mawaziri katika Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, waliolazimika kujiuzulu Februari, mwaka huu, kutokana na kashfa ya Richmond.

Walipokuwa wanajiuzulu, walikana kuhusika kwa namna yoyote na aina yoyote ya ukiukwaji wa sheria na taratibu, katika mchakato wa kuipatia Richmond kandarasi ya kufua umeme wa dharura.

Hii haiwezi kuwafanya Karamagi na Dk. Msabaha kuwa wasafi kwa sababu kukana kwao bado hakujathibitishwa na chombo kingine huru.

Inagwa sehemu ya tuhuma dhidi yao zimethibitishwa na baadhi ya vyombo, lakini hatuwezi pia kusema kuwa Karamagi na Msabaha ni wachafu kwa sababu chombo cha kutoa haki hakijalipitia suala hilo na kutoa maamuzi yake.

Kwa hiyo, Karamagi na Msabaha wanaweza kuwa wachafu au wasafi, lakini hatua ya serikali kuitumia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwachunguza wanasiasa hawa, itakuwa ni kutowatendea haki.

Hii ni kwa sababu usafi wa TAKUKURU yenyewe kama ilivyo kwa akina Karamagi na Msabaha, nao upo mashakani kutokana na yale yaliyobainishwa na Kamati Teule ya Bunge.

Kamati hiyo, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), katika mapendekezo yake, ilitaka TAKUKURU ifanyiwe mabadiliko makubwa.

Kana kwamba hiyo haitoshi, kamati ilipendekeza; “Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU awajibishwe kwa manufaa ya umma na maofisa wa TAKUKURU walioshiriki kwenuye zoezi la uchunguzi na kuandaa Taarifa ya Richmond Development Company LLC iliyoficha ukweli nao pia wawajibishwe kwa manufaa ya umma”.

Lakini katika taarifa yake ya kuonyesha jinsi serikali ilivyoyatekeleza mapendekezo hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiripoti bungeni, alisema vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa kina kwa lengo la kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote iliyojitokeza wakati wa mchakato huu inayomhusisha Karamagi, katika suala hili.

Sote tunafahamu kuwa chombo cha dola chenye mamlaka ya kufanya uchunguzi wa masuala ya rushwa nchini hivi sasa ni TAKUKURU, ambayo Dk. Mwakyembe na wenzake walitueleza kuwa inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa kutokana na upungufu uliobainika ndani yake.

Tangu mapendekezo hayo yatolewe hadi sasa hatujasikia mabadiliko yoyote kufanyika kwa TAKUKURU. Zaidi sana, Pinda alizidi kuionyesha taasisi hiyo kama yenye usafi wa kutilia mashaka pale alipoeleza kuwa hata Mkurugenzi wake mkuu, Edward Hosea, ni miongoni mwa maofisa wa serikali ambao wametakiwa kujieleza, kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Hizi zinaweza kuwa tuhuma tu, lakini sidhani kama chombo kinachotuhumiwa kinaweza kutumika kumchunguza mtuhumiwa mwingine. Hii ni sawasawa na kutumia maji machafu kuosha chombo. Hata kama chombo hicho ni kisafi, hatimaye kitachafuliwa na yale maji machafu.

Tukiiachia TAKUKURU ifanye uchunguzi dhidi ya Karamagi na Msabaha, itakapotoa matokeo yake na kubainisha kuwa mawaziri hao wa zamani walijihusisha na rushwa, wapo watakaohoji iwapo hiyo si njama ya TAKUKURU kutaka kujisafisha na udhaifu iliouonyesha awali?

Pia, kama TAKUKURU ikisema mawaziri hao waliojiuzulu hawakujihusisha na rushwa, wengi watasema walitarajia hivyo kwa sababu TAKUKURU ilishasema tangu awali kuwa hakukuwa na rushwa katika suala hilo.

Hadhi ya Karamagi na Dk. Msabaha katika sakata hili lote itawekwa sawa na uchunguzi utakaofanywa na chombo ambacho usafi na uadilifu wa viongozi wake hauna mashaka. TAKUKURU hii tuliyo nayo sasa, ambayo kiongozi wake mkuu naye yupo chini ya uchunguzi, haina sifa hiyo hata kidogo.


Source: Tanzania Daima
 
Kuna njama za kuwachafua zaidi Karamagi, Msabaha
Source: Tanzania Daima

Sijamuelewa mwandishi kuwa kama haiamini TAKUKURU inawezaje kuwachafua Karamagi na Msabaha? Na je mwandishi ana uhakika gani kuwa watu hawa wasafi? Ni kipimo gani alichonacho mwandishi ambacho kinapelekea kusema kuwa tayari hawa jamaa wamechafuliwa na wakiendelea kuchafuliwa zaidi ya hapo basi ni kuzidi kuchafuliwa? Na je standard ipi ya mla rushwa ambayo inapelekea kuwa asiwe mchafu,mchafu kiasi au zaidi? Na je anataka Hosea ampe sh. ngapi ili naye uchafu wake usiwe zaidi ya alivyo?

Waberoya
 
kuna kuchanganyana hapa ni kama swala la relativity, vitu viwil vikiwa vinaenda kwenye spidi inayofanana na vinaenda sambamba basi kama uko kwennye chombo kimojawapo utaona kile chA PILI KAMA HAKIENDA NA KUWA VYOTE VIWILI VITAKUWA KAMA VIMESIMAMA, KARAMAGI, MSABAHA, NA LOWASA IN ONE HAND, NA TAKUKURU CHINI YA HOSEA IN ANOTHER HAND WOTE NI WACHAFU.

TUNAHITAJI CHOMBO KAMA MAHAKAMA NA MAGEREZA KUWASAFISHA
 
Wangepekewa mahakamani wakasafishwe sio wanawasafisha kwa maandamano na mapokezi...........huo ni kuwaibiaa fikra wapiga kura....
 
Sijamuelewa mwandishi kuwa kama haiamini TAKUKURU inawezaje kuwachafua Karamagi na Msabaha? Na je mwandishi ana uhakika gani kuwa watu hawa wasafi? Ni kipimo gani alichonacho mwandishi ambacho kinapelekea kusema kuwa tayari hawa jamaa wamechafuliwa na wakiendelea kuchafuliwa zaidi ya hapo basi ni kuzidi kuchafuliwa? Na je standard ipi ya mla rushwa ambayo inapelekea kuwa asiwe mchafu,mchafu kiasi au zaidi? Na je anataka Hosea ampe sh. ngapi ili naye uchafu wake usiwe zaidi ya alivyo?

Waberoya

Wenye akili na wenye kukumbuka mambo ni kuwa kwenye hotuba ya mhe mizengo hakugusia kitu chochote kuhusu Lowasa! zaidi ya kuwataja wawili hawa kuwa ndio wanaochunguzwa na ikiamanisha Lowasa yeye hahusiki tena! Jamani kumbukeni wakati mkataba unasainiwa (RICHMOND) huyu jamaa alikuwa PM na yeye ndie aliekuika baraza la mawaziri na kutoa amri ya mkataba huu kusainiwa sasa iweje rungu liwaangukie kina Msabaha peke yao? huu si uwajibikaji! kuna ukweli pia umedhihiri kuwa Lowasa alipokuwa PM alimshinikiza Amos Makala kusaini mkataba wa ujenzi wa jengo la UVCCM kwa vyovyote vile Makala asingemkatalia PM na wakati ule hakuna aliejua kama Lowasa angeanguka kwenye nafasi ile! Kumwacha Lowasa na kuwachunguza kina Msabaha ni uonevu ulipitiliza!

Hii nchi ni yetu sote lazima wakubwa na wadogo wawajibike sio wakubwa waache wadogo wafanywe mbuzi wa kafara.
 
Back
Top Bottom