kuna nini kichwani mwa mke wangu

jamii leo nimeona nijisalimishe haba kwenu labda nitapata maarifa.
mke wangu ana msifia sana mdogo wangu wa kiume, yaani kuna wakati hata hakuna humuhi wa hizo sifa lakini yeye anamwaga tu sifa kwa bwana mdogo!!!!!!
nimefanya utafiti sijagundua kitu chochote mimi nampenda sana mdogo wangu nashindwa kumuondoa hapa nyumbani kwa kutumia hisia tu kwamba yawezekana kuna kitu kati yake na mama watoto au mama watoto anakitu kichwani?

mahusiano yetu yako sawa tu sijagundua kasoro, lakini sifa na maongezi muda wote kuhusu bwana mdogo sasa yanaanza kunipa ishara mbaya kichwani mwangu

naombeni maarifa sitaka kuchemka nawajari na kuwapenda wote, mmoja kama mke na mwengine kama ndugu

TUKICHEKA NA CCM TUTAVUNA MABUHA.
"Freedom is never voluntarily given by the oppressor;it must be demanded by the oppressed".
Martin Luther King, Jr

http://www.lifeofmshaba.com
wanaoteseka na ufisadi ni wanawake na watoto

@ KIKWETE HATOKE MAGOGONI HATUFAI

Aisee im out
 
Pole sana ndg yangu kwa hali hiyo, lakini pia nikupongeze kwa kutochukua uamuzi haraka.
Swali langu kwako;
Je, mkeo ni mama wa nyumbani? Na mdogo wako hana kazi, biashara wala haendi shule?Na je hapo kwako hakuna watu wengine zaidi yenu hasa muda wa asbh hadi jiono? Kama majibu ni ndiyo, ndiyo maana mkeo ana muda mwingi wa kukaa na mdogo wake, na anamjua vilivyo maana muda wote wako nyumbani pamoja.

Nionavyo mimi;
Huenda mkeo hana maana mbaya kabisa kuhusu kumsifia kwake mdogo wako, ndiyo maana anadiriki kukuambia, kama angekuwa na mahusiano, sidhani kama angethubutu kumsifia mbele zako.

Kwa upande mwingine, inawezekana anazuga tu, ila wewe angalia mazingira ya nyumbani kwako yalivyo utapata jibu hasa ukimuangalia mdogo wako alivyo siku hizi na umri wake pia utakuambia kama anaweza kufanya kitu kama hicho.
Alternatively, mpeleke likizo mdogo wako kwenu kama miezi miwili au mitatu kisha umsikie mkeo baada ya kuondoka yeye anasemaje, utapata jibu. Pole sana

Pole mkuu, kwani humuamini mdogo wako?Na hata Mkeo?
Mara nyingi wadogo zetu wa kiume wanapata nafasi ya kuwa karibu na shemeji zao kwa kuwa muda mwingi wanakuwa pamoja kuliko sisi na hasa kama mke si mfanyakazi.Si wakati woote wakatumia ukaribu huo vibaya, japo kwa sehemu kubwa wakiutumia huo ukaribu vibaya Inaharibu Familia.
Mwanzoni mwa miaka ya 90 nilikuwa na rafiki yangu alikuwa anakaa na kaka yake Pale Ilala , mara nyingi nilikuwa namtembelea yule rafiki yangu, kwa kweli Jinsi rafiki yangu alivyokuwa karibu na shemeji yake nilikuwa simuamini kabisa, Japo rafiki yangu ni mkimya sana. Walikuwa pamoja kila mahali,Na kaka mtu hakuwa na hisia yoyote mbaya, Yule shemeji alikuwa hawezi toka kwenda mahali kama rafiki yangu hayupo. Kwa bahati mbaya Kaka ya rafiki yangu na mkewe walishafariki siku nyingi KWA UKIMWI na rafiki yangu ni mzima wa Afya. Maanake ni kwamba kama rafiki yangu angekuwa na mahusiano na shemeji yake na yeye angekuwa muhathirika.
Usiwaze Vibaya juu yao.Wivu wa aina hiyo sio mzuri unaweza haribu mahusiano katika Familia.
 
sifa ni nyingi kwa kweli
aliwai kusema anaumbo zuri hatapa usumbufu wa wanawake
ana tabia nzuri mkewe hatapata raha
ana juhudi ya masomo na ana akili darasani
ana upendo
na hii ni kama biashara ya kila siku mimi kusikiliza masifa ya bwana mdogo
mpaka inakera

Kwa sifa hizo... mkeo kaanguka vibaya...
Lakini haina maana ana mpango...ila tu ina maana shem wake akikaza buti...
 
Pole sana mkuu.

Usijipe pressure sana na jaribu kufuatilia swala hilo kiutu uzima.

Huenda kama wanavyosema wengine mkeo anakupa msg fulani kwa kumsifia mdogo wako labda anaona una mapungufu fulani ambayo wakati mwingine ni vigumu kukwambia akiogopa kukudhi. Jaribu kujichunguza kama una sifa kama hizo anazozisifia toka kwa mdogo wako then kama huna huenda ndio anazozitaka kwako. Kitu kingine wanawake wengi wanapenda waume zao wawe na upendo, usikivu, kuonyesha wanawajali na mambo kama hayo, ni rahisi sana kwa wanaweke kurubuniwa au kujikuta amefanya sivyo kwa mwanamume ambaye anatabia kama hizo. Jichunguze utagundua ni ujumbe wako au la. Huenda ukawa ni mkali sana, huna utulivu hata unapokuwa na mkeo, uko busy kupita kiasi, na kdlk.
 
Jema lipi? Tukichukia ndugu wa mume;tuna roho mbaya,tukiwapenda mnatu suspect! Kwa nini hujiamini? Kama vp badilika ufuate yale mazuri ambayo wife ameyaona kwa dogo.
 
Vikwazo,mimi sijui wewe kabila gani,lakini kwetu sisi wahaya kuna kitu tunaita 'okushanzila' meaning kutania.Kwetu ni ruksa kabisa dogo kumtania mke wa kakake ila ni marufuku kaka kumtania mke wa mdogo wake maana yeye anachukuliwa kama baba.Wewe tuliza ball,endelea kumtunza mdogo wako,achana na insecurity , na kisha shukuru kuwa mkeo na mdogo wako mpendwa wanaishi in harmony maana ziko thread kibao humu MMU ambazo zinahusu nyumba kukosa amani kisa shem na wanandugu ni paka na panya na mme anashindwa aegemee wapi.

mkuu ushauri wako umezingatia
sio kwamba ni najaziba au hasira ila nina walakini nahisi kuna ndivyo sivyo ila kusema ukweli wote nawaamini japo sina hakika kama wanaweza kuniibia
 
Jema lipi? Tukichukia ndugu wa mume;tuna roho mbaya,tukiwapenda mnatu suspect! Kwa nini hujiamini? Kama vp badilika ufuate yale mazuri ambayo wife ameyaona kwa dogo.

mimi hapa naondelea ile ya kupenda kabisa kabisa yaani mpaka basi hata hakuna siku unamwaga story zangu au mtoto wetu
kuwachukia ni vibaya lakini kama unapenda ile ya ndani kwa kweli nayo sio nzuri
 
hakuna mchezo wowote mchafu kaka,unajua kina dada wanapata mda mwingi wa kuwa na familia nyumbani hivyo upelekea kumjua kili mmoja na tabia zake ndani ya nyumba,kutokana na mambo uliyo yasema hakuna kitu cha namna hiyo,nacho amini ni kwamba jinsi unavyompenda mkeo ndo yapelekea uwaze mambo tofauti,kama anafanya vizuri katika masoma atawewe unaona,nyumbani pia kama ni mwelewa unaona pia hacha apewe sifa zake naimani atafanya vizuri zaidi na ataishi kwa amani maana kaka nashemeji yake wanampenda na ndiyo kitu anacho amini,amini kama angekuwa anafanya kinyume nasifa anazopewa ungeona na wangekuwa paka na panya,pia naisi mkuo ni mtumwenye kupenda maendeleo ya mtu,nakushauri upotezee kuliko kutaka kutaka kuondo amani ndani ya nyumba yako.
 
Pole sana mkuu.

Usijipe pressure sana na jaribu kufuatilia swala hilo kiutu uzima.

Huenda kama wanavyosema wengine mkeo anakupa msg fulani kwa kumsifia mdogo wako labda anaona una mapungufu fulani ambayo wakati mwingine ni vigumu kukwambia akiogopa kukudhi. Jaribu kujichunguza kama una sifa kama hizo anazozisifia toka kwa mdogo wako then kama huna huenda ndio anazozitaka kwako. Kitu kingine wanawake wengi wanapenda waume zao wawe na upendo, usikivu, kuonyesha wanawajali na mambo kama hayo, ni rahisi sana kwa wanaweke kurubuniwa au kujikuta amefanya sivyo kwa mwanamume ambaye anatabia kama hizo. Jichunguze utagundua ni ujumbe wako au la. Huenda ukawa ni mkali sana, huna utulivu hata unapokuwa na mkeo, uko busy kupita kiasi, na kdlk.

hiyo nyekundu nitaifanyia kazi ina ukweli mwingi sana lakini ni mambo ya kuweka mshiko sawa, sasa kama ni tatizo sijui kama kutokuwa nao alitakuwa tatizo?
ninaifanyia kazi, kuhusu usikivua namsikilia sana huku nikiwa na mambo mengine yanaendelea na sijawai kumkatalia wala kumcheleweshea haki yake yoyote ile.
mara nyingi uwa nasimamisha shunguli zangu kama naitajika,
mimi nahisi hizi foleni za hapa mjini nazo zina hatarisha ndoa yangu au muda wa kujumuika na familia.
sijajua nifanye utatuzi gani maana kufika UKONGA inaweza kuchukua masaa manne hiyo ni saa mbili
mimi naanza kuota upara kwa mawazo kazi na ndoa duh
 
TUKICHEKA NA CCM TUTAVUNA MABUHA.
"Freedom is never voluntarily given by the oppressor;it must be demanded by the oppressed".
Martin Luther King, Jr

http://www.lifeofmshaba.com
wanaoteseka na ufisadi ni wanawake na watoto

@ KIKWETE HATOKE MAGOGONI HATUFAI

Aisee im out

wewe una lako jambo today i wil play cool lakini kama utaendelea
moto utawaka nadhani unanisoma
potezea thread zangu tafadhali
ushazoea kutafuatia watu BAN
unaweza sana hiyo biashara hapa jf
 
Bro, kwani mdogo wako anafanya nini hapo nyumbani kwako? ana umri gani? yeye anasema nini kuhusu shemeji yake? Na yeye anamwaga sifa? ukimwangalia kwa kumkazia macho usoni yukoje? Just remember the guilt are always afraid!

yuko UDSM
anamika 22
 
sina hakika sana kama hajawai huko nyuma lakini kwa ufahamu wangu hapana ,
kutoka na msukumo wa mawazo kama hizo hoja mbili hapo juu ndio maana nimekwama, nikweli sitaki kutumia hisia kufanya mahamuzi ya aina yoyote.
kumwambia nashindwa sitakii kufanya kitu ni kakijutia,
nimekuwa nafikilia kufanya hivyo lakini nakwama kwa kugopa kama nitakuta nilikuwa na hisia mbaya tu.
kuna kijana nilita kujaribu kumtumia kama mpelelezi lakini nasiki ni rafiki sana na mdogo wangu.
kwa sasa mimi nafikiri kumtoa dogo hapa home bila kusema kiti ila kwa kutengeneza story
sijui kama itasaidia

nakushauri haya mawazo yako usimwambie mtu,sababu inaweza kuwa nafasi ya shetani kugeuza amani kuwa vita,mim naona kama hao wanapatana tu,kungekua na jambo baya asingekua anamsifia mbee yako lkn sipati hisia zozote mbaya kutokana na ulichoeleza labda kama kuna la zaid,mm wkt nasoma na mdogo wa mume wa dada yangu wa kiume tulikua tunasoma boarding,wkt wa likizo tulikua tunakaa kwa dada yangu wote,huyu shemeji yetu na dada yangu na mim na housegirl wa dada tulikua tunampenda huyu shem wetu sbb alikua anatuchekesha sana,na dada yangu alikua anamsfia sana sbb alikua na heshima,ila shemeji yangu hakua na hisia mbaya,japo sijui moyoni mwake,na huyu shem wetu alikua akiwa na date na msichana dada yangu alikua anampa hadi hela za kufanikisha kidate chake,kwa kweli tulikua tukikutana inakua furaha sana,hivyo naona ni kitu kama kinachofanana na hiyo,ww fuatilia kimya kimya lkn usijilazimishe kuona kitu ambacho akipo maana ni vyema mtu na shemeji yake wakipendana kukliko kila siku ungekua unasikia malalamiko.
 
Siku hizi shetani ameshika kasi, kwa hiyo sikushangai kuhisi mdogo wako anaweza kuwa anakumegea wife. Wewe mkeo wamjua vizuri na unaweza jua anapotoa hizo sifa ni za juu juu tu au zimeambatana na feelings.

Chakujifunza kwa wengine ni kuwa si vizuri kumsifia mtu wa jinsia nyingine mbele ya mwenza wako, tena mbaya zaidi kama unarudia rudia kama wimbo. Maana naona mtoa mada ameconclude kuwa hizo sifa ni contrast ya yeye alivyo.

If you love someone you should care for his/her feelings and the best way is to think before talking.
Fikiria mumeo anakwambia mke wa fulani anajua sana kupika. Utamuelewaje? Tena anakwambia almost daily. Maanake wewe hujuhi kupika.
 
Pole sana ndg yangu kwa hali hiyo, lakini pia nikupongeze kwa kutochukua uamuzi haraka.
Swali langu kwako;
Je, mkeo ni mama wa nyumbani? Na mdogo wako hana kazi, biashara wala haendi shule?Na je hapo kwako hakuna watu wengine zaidi yenu hasa muda wa asbh hadi jiono? Kama majibu ni ndiyo, ndiyo maana mkeo ana muda mwingi wa kukaa na mdogo wake, na anamjua vilivyo maana muda wote wako nyumbani pamoja.

Nionavyo mimi;
Huenda mkeo hana maana mbaya kabisa kuhusu kumsifia kwake mdogo wako, ndiyo maana anadiriki kukuambia, kama angekuwa na mahusiano, sidhani kama angethubutu kumsifia mbele zako.

Kwa upande mwingine, inawezekana anazuga tu, ila wewe angalia mazingira ya nyumbani kwako yalivyo utapata jibu hasa ukimuangalia mdogo wako alivyo siku hizi na umri wake pia utakuambia kama anaweza kufanya kitu kama hicho.
Alternatively, mpeleke likizo mdogo wako kwenu kama miezi miwili au mitatu kisha umsikie mkeo baada ya kuondoka yeye anasemaje, utapata jibu. Pole sana

kuna biashara anasimamia lakini inafunga saa mbili jioni ila sio muda wote huko hapo
dogo huko shuleni kwa sasa ila anaishi hapo nyumbani na niushauri wangu yeye kuishi hapa nyumbani japo kuna wakati anaweza hasiwepo hapa home hata kwa siku tatu nne kwa shughuli zake za masomo
 
Siku hizi shetani ameshika kasi, kwa hiyo sikushangai kuhisi mdogo wako anaweza kuwa anakumegea wife. Wewe mkeo wamjua vizuri na unaweza jua anapotoa hizo sifa ni za juu juu tu au zimeambatana na feelings.

Chakujifunza kwa wengine ni kuwa si vizuri kumsifia mtu wa jinsia nyingine mbele ya mwenza wako, tena mbaya zaidi kama unarudia rudia kama wimbo. Maana naona mtoa mada ameconclude kuwa hizo sifa ni contrast ya yeye alivyo.

If you love someone you should care for his/her feelings and the best way is to think before talking.
Fikiria mumeo anakwambia mke wa fulani anajua sana kupika. Utamuelewaje? Tena anakwambia almost daily. Maanake wewe hujuhi kupika.

mkuu ni sahihi kabisa huo ndio utata wenyewe kila siku nasikiliza nyimbo za sifa kwa mdogo wangu,
ndio maana sasa napata mashaka kidogo hivi ni sifa za kawaida kweli au zinatokana na kitu furani maana sio
kusema mimi niondoe wasiwasi kumbe na liwa au nikurupuke na kuuliza harafu ni umbuka na mimi hivto vitu viwili vinanikera
 
nakushauri haya mawazo yako usimwambie mtu,sababu inaweza kuwa nafasi ya shetani kugeuza amani kuwa vita,mim naona kama hao wanapatana tu,kungekua na jambo baya asingekua anamsifia mbee yako lkn sipati hisia zozote mbaya kutokana na ulichoeleza labda kama kuna la zaid,mm wkt nasoma na mdogo wa mume wa dada yangu wa kiume tulikua tunasoma boarding,wkt wa likizo tulikua tunakaa kwa dada yangu wote,huyu shemeji yetu na dada yangu na mim na housegirl wa dada tulikua tunampenda huyu shem wetu sbb alikua anatuchekesha sana,na dada yangu alikua anamsfia sana sbb alikua na heshima,ila shemeji yangu hakua na hisia mbaya,japo sijui moyoni mwake,na huyu shem wetu alikua akiwa na date na msichana dada yangu alikua anampa hadi hela za kufanikisha kidate chake,kwa kweli tulikua tukikutana inakua furaha sana,hivyo naona ni kitu kama kinachofanana na hiyo,ww fuatilia kimya kimya lkn usijilazimishe kuona kitu ambacho akipo maana ni vyema mtu na shemeji yake wakipendana kukliko kila siku ungekua unasikia malalamiko.

ni kweli kabisa,
ila avatar yako utata
anyway poa
 
Pole sana ndg yangu kwa hali hiyo, lakini pia nikupongeze kwa kutochukua uamuzi haraka.
Swali langu kwako;
Je, mkeo ni mama wa nyumbani? Na mdogo wako hana kazi, biashara wala haendi shule?Na je hapo kwako hakuna watu wengine zaidi yenu hasa muda wa asbh hadi jiono? Kama majibu ni ndiyo, ndiyo maana mkeo ana muda mwingi wa kukaa na mdogo wake, na anamjua vilivyo maana muda wote wako nyumbani pamoja.

Nionavyo mimi;
Huenda mkeo hana maana mbaya kabisa kuhusu kumsifia kwake mdogo wako, ndiyo maana anadiriki kukuambia, kama angekuwa na mahusiano, sidhani kama angethubutu kumsifia mbele zako.

Kwa upande mwingine, inawezekana anazuga tu, ila wewe angalia mazingira ya nyumbani kwako yalivyo utapata jibu hasa ukimuangalia mdogo wako alivyo siku hizi na umri wake pia utakuambia kama anaweza kufanya kitu kama hicho.
Alternatively, mpeleke likizo mdogo wako kwenu kama miezi miwili au mitatu kisha umsikie mkeo baada ya kuondoka yeye anasemaje, utapata jibu. Pole sana

Jenga imani kwa mke na mdogo. kama ana tabia chafu mdogo ukimfukuz watafanya wengine. so, uwe na subira ndugu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom