Kuna Mwana JF yeyote aishiye Dar au karibu Anafanya Drip Irrigation? Ningependa kumtembelea

Doltyne

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
440
170
Habari zenu wana JF,
Nafanya utafiti wa kutaka kujiridhisha kwanza kabla sijaanza kulima kwa kumwagilia kwa matone...
Nimeshalifanyia utafiti wa kina hili swala, sasa nipo katika stage ya kutembelea mashamba/bustani za wanaotumia njia hii ya umwagiliaji ili niweze kupata majibu ya kutosha na kujiondolea utata wa uelewa.
Je, Kuna Mwana Jamii yeyote anayefanya Drip Irrigation, be it in a large scale au hata kabustani...
Nimeshaenda BALTON, nimeona kila nilichokuwa nataka kuona, nimeshatembelea mkulima mmoja kanieleza ya kwake, sasa Natafuta wengine ili niweze kupima na kuchuja pumba na chuya...
Pili, Ningependa kujua Kama Kuna yeyote anayefanya Greenhouse Farming katika ukanda wetu huu wa pwani, Amekutana na changamoto gani na amejikwamuaje na ana mikakati gani...

Natanguliza shukran za dhati.
Kama Kuna mtu anafanya hii kitu apost hapa chini ili wengi wafaidike, na kama uko tayari kunialika basi ni PM.
 
Mimi nilifuatilia mpaka wizara ya kilimo walinisaidia. Hebu jaribu kuwasiliana na ofisi za kilimo za wilaya sijajua uko wilAYA gani. Ulizia miradi ya DADIPS watakupa details za drip irrigation. Ila vitendea kazi na utaalam wanatoa hao Balton Ltd wako arusha.
 
Shukran sana Wana JF, Huko kote nimeshapita na nimeshapata taarifa za kutosha kabisa... Ninachohitaji sasa hivi ni kutembelea wakulima nione wamefanikiwaje na wametumia mbinu gani... nk....Kilimo cha kuelezewa tofauti na cha kufanya
 
Back
Top Bottom