wanajf kama kuna mtu ana habari za kinachoendelea kuhusu urejeshwaji wa wanyama waliotoroshwa maana isije kuwa makelele ya bungeni ndio mwisho! kama walitoroshwa kimagendo najua hata sheria za kimataifa zitakuwa upande wetu
Subutu! Walishakwenda na maji na wajanja wameshaweka vyao mifukoni.
BAK,Mkuu Jasusi hii ni Serikali iliyobweteka lakini kama ingekuwa ni Serikali makini basi hao wanyama wote wangekuwa wamesharudishwa nchini au kungekuwa na juhudi za wazi kabisa za kuwarudisha wanyama hao nchini.
BAK,
Ninavyosikia kuna mkono wa mkulu hapo. Ngoja kuna siku Maige atafunguka.
Nina Mashaka na hili mkuu. Hawa Twiga watakuwa wameshazoea kula mikate na salad Huko Uarabuni. Leo uwarudishe huku kwetu sidhani hata kama hao Twiga wenyewe watakubali kurudi katika nchii hii iliyojaa mauzauza kila kukicha. Simba watoto wanasafirishwa kwenye makaratasi inasema ni vitoto vya paka.....Aisee Bongo hatari!!!!!!!wanajf kama kuna mtu ana habari za kinachoendelea kuhusu urejeshwaji wa wanyama waliotoroshwa maana isije kuwa makelele ya bungeni ndio mwisho! kama walitoroshwa kimagendo najua hata sheria za kimataifa zitakuwa upande wetu