Kuna mipango iliyosukwa Lema akigombea ubunge kuenguliwa na tume!

naiamini timu ya cdm nashauri tu kuwa pitieni hukumu vizuri kutegua mitego ya serikali na ccm
 
Nikweli hukumu hiyo inautata kwa kutaja vifungu vyote viwili, kwahiyo wanasheria wa CDM wawe makini kupitia hukumu hiyo. hata hivyo hata mimi nikisimamishwa kugombea nitashinda
 
Mii nashauri wasikate rufaa, twende kwenye uchaguzi ila lema asigombee. Badala yake atumike kujenga chama kama afanyavyo Dr. Slaa na mpambanaji Mwita mwikwabe
 
Tuna mweka mpambanaji mwengine lema atatumika kwenye M4C
Mkuu MAONO yangu ni kwamba CDM haikati rufaa hasa ikiwa Lema amepigwa ban. Kuna tetesi kuwa uongozi wa juu wa CDM hauko comfortable na Lema hivyo hii ni nafasi yao ya kumweka nje japokuwa watu wa Arusha hasa vijana wako vizuri tu na Lema. Kada ya kati na juu ya watu wa Arusha pia hawako comfortable na Lema. Nina Maono kwamba hatakata rufaa bali wataingia kwenye uchaguzi na kumsimamisha mtu mwingine hivyo watakuwa wamefanikiwa kumweka kando Lema na wao kuwa comfortable. Hayo ni maono yangu kutokana na uchunguzi wangu.

Siasa ni mchezo mchafu.
 
Nikweli hukumu hiyo inautata kwa kutaja vifungu vyote viwili, kwahiyo wanasheria wa CDM wawe makini kupitia hukumu hiyo. hata hivyo hata mimi nikisimamishwa kugombea nitashinda
Hukumu ya maandishi imeishatoka?
 
mimi nashangaa sana ...mtu wausalama wa taifa ametumwa afanye kazi in favour of ccm halafu anaanza kupayuka siri za kazi aliyotumwa ... inawezekana kweli au ni hisia za watu

anyways lisemwalo lipo kama halipo linakuja
 
Ninaunga mkono hoja ya CDM kukata RUFAA. Kwanza watauthibitishia umma wa Watanzania kuwa wanajali sana kuhusu gharama kubwa za kuendesha chaguzi ndogo - pesa ambayo ingeweza kuelekezwa kuboresha huduma za kijamii kama vile kuwanunulia watoto wetu madawati ya kutosha ili wasipinde migongo wakingali makinda. CDM chukua njia ya kukata rufaa kwanza, uchaguzi mdogo uje baada ya kujaribu hiyo.:suspicious:
 
Ninaunga mkono hoja ya CDM kukata RUFAA. Kwanza watauthibitishia umma wa Watanzania kuwa wanajali sana kuhusu gharama kubwa za kuendesha chaguzi ndogo - pesa ambayo ingeweza kuelekezwa kuboresha huduma za kijamii kama vile kuwanunulia watoto wetu madawati ya kutosha ili wasipinde migongo wapkingali makinda. CDM chukua njia ya kukata rufaa kwanza, uchaguzi mdogo uje baada ya kujaribu hiyo.:suspicious:
Naona umesema kujaribu. Lakini mkuu wanaweza wakakata rufaa kisha Majaji wa Rufaa wakakazia hukumu.
 
Magamba kila wanalolipanga kabla haijakaa sawa limenaswa!

Mungu yupo upande wetu
 
Naona umesema kujaribu. Lakini mkuu wanaweza wakakata rufaa kisha Majaji wa Rufaa wakakazia hukumu.

Inategemeana na msingi wa rufaa. Nadhani kinachogomba kwenye hiyo hukumu ni kwamba Lema amekuwa convicted kwa makosa ya kutumia lugha ya udhalilishaji au lugha mbaya ambapo adhabu yake ni kutengua matokeo. Kifungu alichotumia Judge kutoa hukumu ni cha makosa ya Rushwa ambapo mtu akihukumiwa kwa kifungu hicho, maana yake ni kwamba anavuliwa ubunge na hawezi kugombea tena mpaka baada ya miaka 5.
 
CCM kwa kutumia mihimili yote ya dola wamekuwa wakijitahidi kubaka demokrasia. Ni wakati muafaka Chadema kulitambua hilo kwa kuachana na mahakama kwani imetumika kukandamiza vyama vya upinzani nchini. Je kesi isiyokua na msingi wowote ya madiwani wa Chadema inasubiri nini mahakamani kupatiwa ufumbuzi katika mahakama. CCM wana mawazo finyu kuwa Lema ndiye anakibeba chama cha demokrasia na maendeleo ni maoni yangu kwa cdm kujipanga na kumsimamisha mtu mwingine kugombea jimbo la Arusha na kudhihirisha kuwa ina hazina ya kutosha ya viongozi.
 
Ni kweli,kaa chonjo sana, ama kifungu kilichotumika ni kile kinachomuzuia mp kutogombea ndani ya
miaka mitano, without appeal it will be difficult to the ex mp to stand as a candidate.
 
Back
Top Bottom