Kuna mantiki gani mfanyakazi wa serikali kutolipa kodi?

The Jicho

Member
Sep 11, 2010
16
1
Wana JF
Hivi majuzi waziri wa fedha akisoma budget alitaarifu kuwa posho zitakazolipwa wafanyakazi wa serikali hazitakatwa kodi. Pamoja na ukweli kwamba hazijawahi kukatwa kodi je kuna sababu gani ya kumkinga mfanyakazi wa serikali na baadhi ya kodi? Je hao walioko serikalini ndio wazalendo zaidi kuliko sisi? Ufisadi wa aina hii umekuwepo kwa mda mrefu kwa mfano kodi ya gari anayolipa mtumishi wa serikali ni kidogo kuliko ninayolipa mimi. Kwa nini kuna set up kama hizi bado sielewi? Kwa nini serikali iwe na uchungu na kisection fulani tu cha watu wake (walioko serikalini )je hawa wengine si wananchi? Kwani hizo posho wanazipata wapi si ni kodi zetu sisi tunaolipa kodi? kwa nini wao wasilipe? Je uzalendo ni kulipa kodi au kutolipa kodi? Je Rais analipa kodi na kama halipi ni kwa nini? Na kama hawa wote hawalipi kodi kwa nini tunasumbuka kujiuliza tutapanua vipi wigo wa kodi? Au nyie wana JF mnalionaje hili?
 
Acha zako wewe!kuna mlipa kodi kama mfanyakazi?!nadhani unaleta utani wewe,na sasa tunataka wafanyabiashara walipe kodi bila kujali wameingiza faida kiasi gani,na wakulima wote walipe kodi ya kichwa!
 
Anatengeneza matabaka nchini, kwani anadhani trick ya "divide and rule" itawasaidia huko mbeleni!
 
Mshahara wenyewe wanalipwa laki mbili,so hyo extra duty allowance ikitozwa kodi c watakufa njaa,waacheni waendeshe maisha.
 
Hivi hiyo posho inayozungumziwa ni ipi? Mimi ni mfanyakazi serikalini level ya senior na sina posho yoyote zaidi ya mshahara hivyo nashangaa!!!!!Kazini kwangu najua wakuu wa maidara ndio wanaposho, sasa kwanini wanajumuisha wafanfnykzai badala kuweka wazi walengwa ni wakina nani?
 
Hebu uwe unaweka mada zilizofanyiwa utafiti. Kwa taarifa yako wafanyakazi ndo walipa kodi wakubwa kwani mshahara wao wa kila mwezi unakatwa kodi tena kubwa sana na kuwaachia kimshahara ambacho hakikidhi mahitaji. Ukilinganisha na wafanyabiashara ambao mapato yao hayapo accessible kutokana na mfumo uliopo. Anaweza kuuza hata milioni 10 asitoe hata senti ya kodi. Hizo posho ambazo mara nyingi wanafaidi walio kwenye menejimenti ni kwa kufidia mishahara yao ambayo haikidhi. Kwa hiyo msiwasakame, komaeni na wafanyabiashara na watu wengine ambao mapato yao hayako accessible kuweza kukatwa kodi.
 
Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi sio kwa wale ambao mishahara yao inatosha. Huu ndio ukweli duniani kote. Kinyume na kulipa kodi ni ufisadi. Kwa nini serikali ya ccm inakuwa na mawazo ya kifisadi tu?
 
Nani kakwambia posho zilikuwa hazikatwi kodi? Zilikuwa zinakatwa tena kubwa sana wakati wakubwa pamoja na wabunge hawakatwi kodi kwenye posho zao kubwa,Wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kwenye mishahara yao halafu viposho vidogo wanavyopata wewe unataka vikatwe kodi? Acha zako hizo!!!
Wana JF
Hivi majuzi waziri wa fedha akisoma budget alitaarifu kuwa posho zitakazolipwa wafanyakazi wa serikali hazitakatwa kodi. Pamoja na ukweli kwamba hazijawahi kukatwa kodi je kuna sababu gani ya kumkinga mfanyakazi wa serikali na baadhi ya kodi? Je hao walioko serikalini ndio wazalendo zaidi kuliko sisi? Ufisadi wa aina hii umekuwepo kwa mda mrefu kwa mfano kodi ya gari anayolipa mtumishi wa serikali ni kidogo kuliko ninayolipa mimi. Kwa nini kuna set up kama hizi bado sielewi? Kwa nini serikali iwe na uchungu na kisection fulani tu cha watu wake (walioko serikalini )je hawa wengine si wananchi? Kwani hizo posho wanazipata wapi si ni kodi zetu sisi tunaolipa kodi? kwa nini wao wasilipe? Je uzalendo ni kulipa kodi au kutolipa kodi? Je Rais analipa kodi na kama halipi ni kwa nini? Na kama hawa wote hawalipi kodi kwa nini tunasumbuka kujiuliza tutapanua vipi wigo wa kodi? Au nyie wana JF mnalionaje hili?
 
Acha zako wewe!kuna mlipa kodi kama mfanyakazi?!nadhani unaleta utani wewe,na sasa tunataka wafanyabiashara walipe kodi bila kujali wameingiza faida kiasi gani,na wakulima wote walipe kodi ya kichwa!

truly speaked. 14% ya mshahara anayolipa mfanyakaz as kodi ni kubwa sn, kwa mshahara wng wa 1.2m nalipa kodi karib laki mbil per month, a huge amount
 
Back
Top Bottom