Kuna Jambo baadhi yetu hatuelewi kuhusu Kikwete...

mimi nimepata bahati ya kushuhudia awamu zote za urais nadiriki kusema kikwete kafanya mambo makubwa kushinda marais wote waliomtangulia nazungumza hivyo kwa mifano ifuatavyo;
1 .elimu ya sekondari; amejenga shule za kata karibu nchi nzima na sasa matunda yake yanaonekana sasa hivi karibu
kila kijiji kuna angalau wanfunzi wawili wanasoma shahada ya kwanza achilia mbali certificates na diploma hao ndo
kibao hawana idadi nasema hongera kwa hili kiwete kwani nafamilia yetu imetoa mwanafunzi yuko chuo kikuu toka
ya kata.
2.CHUO KIKUU DODOMA; hapa mheshiwa sijui nisemeji ila kwa lugha rahisi umekata kiu ya maelfu ya watanzania wengi
ambapo kabla ya hapo vyuo vilikuwa vichache sana na ili uingie chuo kikuu kwa masoma ya arts by 2005 ilikulazimu
uwe umefaulu div one pts 3-7. kinyume na hapo utasikia tu watu huwa wanasoma chuo kikuu. kwa kuongezea kulikuwa
naubaguzi wa hali ya juu katika vyuo vikuu vinavyomilikiwa na tasisi za kidini ilikubidi uwe unaendana na dhehebu la
chuo unachotaka kusoma na form za maombi ya chuo zilikutaka upitishe kwenye viongozi wa kidini mtaani kwako mpk
kwa askofu wa jimbo.sasa haya mambo yamekuwa historia narudia kusema hongera baba kikwete uliliona hilo.

3.BARABARA; umefanya maisha ya watanzania yawe bora na rahisi kwani umejenga mtandao mkubwa wa barabara
za lami karbu nchi nzima sasa watu wanauhakika kula sangra toka mwanza, mchele wa kyela na maprachichi ya
tukuyu popote utakapo kuwa ndani ya tanzania kwa uraisi kabisa kwani mazao yanasafirishika barabara zipo hongra
jk
4.KILIMO ;umemwaga matrector jamani wakulima wadogo leo hii wanamiliki matrekta tena kwa bei ya kutupa hakika
jk tutakukumbuka ruzuku za mbolea mpka sasa tanzania imekuwa soko la kuuza mazao ya chakula katika nchi
zinazotuzunguka ajabu na kweli nikikumbuka enzi za mchonga natamani afufuke ayashudie haya.

5.AFYA; umeboresha vituo vya afya karibu kila kituo cha afya umetoa upendeleo kwa madakitari wanaosoma shahada
mbalimbali wapate asilia mia za mikopo. hakuna kama wewe jk.

ukumbuke unadaiwa trion ishirini na ushee.
 
Presenter umeonyesha a high level of thinking, you really talked a "talk" as shaka ssali used to say,
 
Kutokana na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Urais wake, nadiriki kusema kuwa Bwana Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa watanzania wachache sana waliofanikiwa kutimiza ndoto zao. Ni watu wachache sana ambao katika kuishi kwao huweza kutimiza ndoto zao walizojiwekea, huyu Bwana amefanikiwa kwa hilo na tumpe pongezi zake. Kikwete alikuwa na ndoto ya kuwa Rais tu, na si zaidi wala pungufu ya hilo. Na ni Rais wa Tanzania sasa!


Kutokana na aina ya uongozi wake pamoja na kauli zake za mara kwa mara utagundua kwamba Ndugu Kikwete hakuwahi kufikiria kuhusu kuikomboa au kuwakomboa watanzania dhidi ya Umasikini. Hivyo tunaolalamika kila kukicha kwamba ameshindwa kuongoza nchi basi kuna jambo hatuelewi. Kitendo cha Baba wa Taifa kumuwekea kauzibe mwaka 1995 asigombee naweza kusema ilikuwa ni kumcheleweshea tu Ndugu yetu muda wa kutimiza ndoto zake. Na muda mwingi aliutumia kujijengea mazingira ya kuingia Ikulu mara baada ya Mkapa.


Utaweza kuona ni jinsi gani mbio za Urais 2005 ziligubikwa na kuchafuana pamoja na kashfa ambazo hapo awali hatukuwahi kuzisikia na ziliisha mara tu baada ya Ndugu yetu huyu kupitishwa na chama chake “Tukufu” kuugombea Urais (kutimiza ndoto zake). Baada ya kufanikiwa kutimiza ndoto zake, huyu Ndugu yetu akapumzika (wengine watasema akajisahau) na kupelekea waliomsaidia kwenye harakati kuanza kuchafuka na kutotamanika tena katika jamii. Wao watamlaum (Ila yeye hatajali kwa kuwa alishatimiza ndoto zake, shauri yao).


Katika mahojiano yake akawahi kuulizwa eti kwa nini Tanzania ni masikini, naye kwa mshangao akajibu kwamba hajui. Kimsingi hakuwahi kufikiria kuhusu Tanzania na umasikini wake. Bali aliwahi kufikiria Tanzania chini ya Uongozi wake kama Rais. Kwenye Kampeni akasisitiza watu wampe kura ili ajitahidi kutembeza bakuli zaidi tusije tukafa njaa!! (Haamini kabisa kwamba watanzania tunaweza kuishi bila kuomba misaada) Hakujali ni ahadi zipi atatimiza bali alikuwa tayari kuahidi hata kama ni kununulia kila kijiji ndege yake alimradi ndoto zake zitimie.


Ni mambo mengi sana amekuwa akitenda na yakasemwa juu yake, ila kimantiki tunaomsema tunakosea kwa kuwa yeye anaishi ndoto zake. Alitamani kusafiri kwenda nchi mbali mbali, alitamani sana awe anapigiwa mizinga pamoja na kukwagua magwaride, apigiwe saluti kila anapopita na aitwe Mheshimiwa na watu wote. Hizo zilikuwa ndoto zake na amezitimiza. Sisi tunaolalamika anatushangaa na huenda kimoyomoyo anatuuliza: Hivi ninyi ni ndoto ipi katika maisha yenu mliwahi kutimiza?


Kauli ya Baba wa Taifa kuwa “Tukiona mtu anang’ang’ani kwenda Ikulu, basi tumuogope kama Ukoma” ilikuwa na maana kubwa sana.


Cha msingi tuwe makini huko tuendako tusijikute tunaingia tena huu mkenge wa kuwapa Uongozi mkuu wa nchi watu ambao wanautaka ili tu watimize ndoto zao. Wapo watu ambao ndoto zao kuu ni kuikomboa nchi dhidi ya Umasikini. Hao ndiyo wanaotufaa. Na kubwa zaidi kila mmoja wetu, kwa nafasi yake ashiriki kuikomboa kifikra Jamii yake dhidi ya hawa akina Karunguyeye wanaotumia Nyumba za Ibada pamoja na vyombo vya habari kuhubiri sera zao ili waje kutimiza ndoto zao.


Mapendo.
TANMO

Mkuu una utani na AMIRI eeh! Sasa subiri kitakachokupata. Najua system iko humu ndani inafanya sana. Ukienda msalimie MWANG........
 
Aaaaaaaaaah mtukufu ........., muheshimiwa, mkuuu wa kaya upoooooooooooooooooooo!!!!

Ni wengi kumbe hatukukuelewa dhamira yako ............... siku nyingine haturudiii tena,
Maana dizaini yako wanaopiga jaramba tushaanza kuwaona, na tunazidi kumuomba Mungu ili kosa lisijirudiee!!!!!!!!
 
Hivi nyinyi watu mnaoandika pumba kila kukicha mnatokea mikoa gani?Kwanini mnashindwa kutumia akili za kichwa tu na kujua kuwa mnachokiandika ni pumba muachane nacho coz we,re going to ignore u from there.Ngoja nijaribu kupambanua kidogo hapa chini ambapo akili yako imeshindwa kufika.i,ll touch some points from ur threeeeeeed
1.Kikwete alipoulizwa (kwanini Tanzania masikini akajibu=sijui)Hapa ametumia hekima kutoa jibu hilo,asingekuwa na hekima angejibu TANZANIA MASIKINI KWA SABABU JULIUS NYERERE AMEITIA NCHI KWENYE UMASKINI KWA KUKAA MADARAKANI 23 YEARS BILA MAFANIKIO,Ametumia mali za nchi kulijenga kanisa katoliki badala ya kujenga taifa,ametumia mali za nchi yetu akijaribu kuzikomboa nchi za afrika,ameiingiza nchi yetu ktk vita vya kanisa katoliki vya kagera,kuwafilisi matajiri wa kiislam na kudumaza uchumi wa nchi,kudumaza elimu mikoa ya waislamu wengi akidhani anawakomoa waislamu bila kujali kuwa hao ni part ya population ya taifa hili ambao taifa linawategemea kama nguvu kazi na uzalishaj na shughuli mbalimbal za maendeleo,.AIDHA,Angeweza kusema tanzania ni mackini kwasababu rais aliyepita kabla yake mwenyekiti wa makanisa Benjamn mkapa ameiuza nchi na mali zake kupitia UBINAFSISHAJI.Pia utawala wa mkapa umezaa mafisadi ambao kikwete kawarithi na kujaribu kuwashughulikia.
2.ALITAMANI KUWA AWE ANAENDA NCHI MBALIMBALI=Huu ni uchizi tu wa mtoa maada hii,labda alikua amevmbirwa nyama ya nguruwe...j kkwete b4 urais alikua wazir wa mambo y nje,alishatmbea dunia nzima,iweje useme aligombea urais ili apate fursa ya kutembelea nchi mbalimbali?
3,WOSIA WA JULIUS NYERERE(TUKIONA MTU ANANG,ANG,ANIA KWENDA IKULI TUMWOGOPE KM UKOMA)1.Yeye mwenyewe ameng,ang,ania ikulu 23yrs licha y kushindwa kuendesha nchi na kuwapa umaskini watanzania wasiostahiki.
Pili,kwa kupitia kauli hii,ni wakati wa kumkataa dr.SLAA NA CHADEMA Kwani wao ndio wanaong,ang,ania kwenda ikulu hata kwa kumwaga damu,kwahiyo wakiwatangazia kule kanisani mambo ya kumkubali SLAA ww waambie nyerere amekataza kumchagua slaa,
4.WATU WNAOTUMIA VBAYA MEDIA NA NYUMBA ZA IBADA ILI WACHAGULIWE;;;Haya pia yanamuhusu dr.SLAA na chadema so ushauri wangu ww na wenzako muhamasihane kumpinga kwani ubovu wote munauona,,,wekeni imani pembeni mjali maslahi ya taifa.
nextime uje na maada iloenda shule,otherwise jst shut up.
 
JK lives his dream! he does things without thinking and he gives his people position regardless of their records. He is just like King Pharaoh
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom