Kuna Jambo baadhi yetu hatuelewi kuhusu Kikwete...

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
Kutokana na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Urais wake, nadiriki kusema kuwa Bwana Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa watanzania wachache sana waliofanikiwa kutimiza ndoto zao. Ni watu wachache sana ambao katika kuishi kwao huweza kutimiza ndoto zao walizojiwekea, huyu Bwana amefanikiwa kwa hilo na tumpe pongezi zake. Kikwete alikuwa na ndoto ya kuwa Rais tu, na si zaidi wala pungufu ya hilo. Na ni Rais wa Tanzania sasa!


Kutokana na aina ya uongozi wake pamoja na kauli zake za mara kwa mara utagundua kwamba Ndugu Kikwete hakuwahi kufikiria kuhusu kuikomboa au kuwakomboa watanzania dhidi ya Umasikini. Hivyo tunaolalamika kila kukicha kwamba ameshindwa kuongoza nchi basi kuna jambo hatuelewi. Kitendo cha Baba wa Taifa kumuwekea kauzibe mwaka 1995 asigombee naweza kusema ilikuwa ni kumcheleweshea tu Ndugu yetu muda wa kutimiza ndoto zake. Na muda mwingi aliutumia kujijengea mazingira ya kuingia Ikulu mara baada ya Mkapa.


Utaweza kuona ni jinsi gani mbio za Urais 2005 ziligubikwa na kuchafuana pamoja na kashfa ambazo hapo awali hatukuwahi kuzisikia na ziliisha mara tu baada ya Ndugu yetu huyu kupitishwa na chama chake "Tukufu" kuugombea Urais (kutimiza ndoto zake). Baada ya kufanikiwa kutimiza ndoto zake, huyu Ndugu yetu akapumzika (wengine watasema akajisahau) na kupelekea waliomsaidia kwenye harakati kuanza kuchafuka na kutotamanika tena katika jamii. Wao watamlaum (Ila yeye hatajali kwa kuwa alishatimiza ndoto zake, shauri yao).


Katika mahojiano yake akawahi kuulizwa eti kwa nini Tanzania ni masikini, naye kwa mshangao akajibu kwamba hajui. Kimsingi hakuwahi kufikiria kuhusu Tanzania na umasikini wake. Bali aliwahi kufikiria Tanzania chini ya Uongozi wake kama Rais. Kwenye Kampeni akasisitiza watu wampe kura ili ajitahidi kutembeza bakuli zaidi tusije tukafa njaa!! (Haamini kabisa kwamba watanzania tunaweza kuishi bila kuomba misaada) Hakujali ni ahadi zipi atatimiza bali alikuwa tayari kuahidi hata kama ni kununulia kila kijiji ndege yake alimradi ndoto zake zitimie.


Ni mambo mengi sana amekuwa akitenda na yakasemwa juu yake, ila kimantiki tunaomsema tunakosea kwa kuwa yeye anaishi ndoto zake. Alitamani kusafiri kwenda nchi mbali mbali, alitamani sana awe anapigiwa mizinga pamoja na kukwagua magwaride, apigiwe saluti kila anapopita na aitwe Mheshimiwa na watu wote. Hizo zilikuwa ndoto zake na amezitimiza. Sisi tunaolalamika anatushangaa na huenda kimoyomoyo anatuuliza: Hivi ninyi ni ndoto ipi katika maisha yenu mliwahi kutimiza?


Kauli ya Baba wa Taifa kuwa "Tukiona mtu anang'ang'ani kwenda Ikulu, basi tumuogope kama Ukoma" ilikuwa na maana kubwa sana.


Cha msingi tuwe makini huko tuendako tusijikute tunaingia tena huu mkenge wa kuwapa Uongozi mkuu wa nchi watu ambao wanautaka ili tu watimize ndoto zao. Wapo watu ambao ndoto zao kuu ni kuikomboa nchi dhidi ya Umasikini. Hao ndiyo wanaotufaa. Na kubwa zaidi kila mmoja wetu, kwa nafasi yake ashiriki kuikomboa kifikra Jamii yake dhidi ya hawa akina Karunguyeye wanaotumia Nyumba za Ibada pamoja na vyombo vya habari kuhubiri sera zao ili waje kutimiza ndoto zao.


Mapendo.
TANMO
 
We are in a deep shit!!!! Hakuna Mtanzania anayeelewa muelekeo wa nchi, hata akiulizwa waziri mkuu Pinda now hajielewi!!!!! Kuna kauli aliwahi kutoa Sumaye sasa tunazidi kuzielewa!
 
Kuna watu walimchukia sana Jk kwa kuwa nyie mlimpenda sana sasa kuna watu wanampenda sana kwa kuwa nyie mnamchukia sana!
 
TANMO
Huyu ni kiongozi asiyejali kabisa.Yeye kwake muhimu ni kulinda watu wachache kwa gharama ya wengi.

Tatizi lingine ni kuwa ametokana na chama dhaifu sana kwani ndani ya chama karibu kila mtu ni dhaifu na ndio maana hakuna hata wa kumnyooshea kidole.

Mamilioni ya wanachama wa chama hiki wako tayari kumuangalia mtu mmoja afanye mambo ya kukigharimu chama chao nao kumuangalia kama vile mdori.

Kweli hawa jamaa wamelala usingizini na atawaponza siku si nyingi.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kipya hapa, ni nyimbo ileile ya kila siku. Mtasema sana lakini mwisho wa maneno yeye atabaki kuwa Rais mpaka 2015 halafu anapokeza kijiti kwa anaye mtaka yeye.
 
Tanzania hata siku moja haipati Rais ambaye angefaa kua kiongozi halisi...85' alikuja Mwinyi badala ya Dr Salim, 95' Nyerere angejua Mkapa ni dhaifu wa mali asingemwandama komredi Malecela jamaa angeongoza kama Mkapa bila kuboresha na kuotesha mizizi huu mfumo wa ufisadi tulio nao sasa (na kitu kingine Malecela alikua organizer mwenye akili asingeleta mitandao kwenye chama kama dhaifu mkapa aliyetishiwa nyau akaogopa akamwachia RA, EL ana JK waje kuharibu kabisa taifa), 2005 akaja mr Dhaifu badala ya Prof mwandosya au Dr Salim


tusitegemee tena bahati 2015 tutapata boga lingine tena litupotezee miaka yetu 10...

On the other Note nafikiri EL naye ni mtu wa ndoto ya Urais long time na hii ni personal objective yake...ukiuliza vision ya taifa liende wapi ndani ya miaka yake 10 atakua hana jibu.
 
Ni Hakika kila siku inayopita ...MAMLAKA YAKE YA URAIS ... yanapungua na kuhamia ... Kwa Waaadamanaji na Waombolezaji wa wafiwa vifo vya Polisi. Serekali ianishiwa na Mamlaka inapwaya THEN? Ina Overreact na kuwafungulia Polisi wakaitafute na kuirudisha NGUVU NA MAMLKA iliyoptea ...Guess Polisi watairudisaje ...?

The vicious circle goes around again and again ... till doomsday for the Nation ..
 
You have a point lakini bila Lowassa, Kikwete asingekuwa Rais na ndio maana Lowassa anaendelea kuwa nguzo kubwa sana ya CCM from 1993 mpaka sasa; Continuation ya nguvu ya Lowassa itakuwa determined na dynamics lakini muhimu zaidi matokeo ya chaguzi za ndani za CCM mwaka huu wa 2012;
 
Maskini kikwete, amekuwa miongoni mwa maraisi mabutu na kibogoyo. Hana meno hata kidogo.. Jamaa sijui anawaza nini. Nathubutu kusema anapenda maisha la filamu.

Nafiki washauri wake wana nidhamu ya uoga au kichwani mwao hawana kitu. Ndo maana wanashindwa kumpa ushauri.
 
You have a point lakini bila Lowassa, Kikwete asingekuwa Rais na ndio maana Lowassa anaendelea kuwa nguzo kubwa sana ya CCM from 1993 mpaka sasa; Continuation ya nguvu ya Lowassa itakuwa determined na dynamics lakini muhimu zaidi matokeo ya chaguzi za ndani za CCM mwaka huu wa 2012;

Mchambuzi siku zote naungana na wewe katika hoja zako juu ya chama chetu lkn kwa analysis ya haraka haraka hadi sasa inaonyesha hakuna jipya kwenye huo uchaguzi unaousema tungoje matokeo...kitu ambacho kabla ya uchaguzi tayari nusu ya matokeo yameshajulikana nani in nani out je unapinga hilo?naamini unajua ukweli kama mtu unayefatilia siasa, kifupi still hakuna collective goals kama chama shv bali kuna wao na sisi huu uchaguzi hadi sasa umeshindwa kubadili hilo kwa vitendo bali linanenwa kwa maneno subiri move inaendelea
 
Kumbe Nyerere alishaa uona Udhaifu wa mdhaifu mapema!
Kweli mtumzima dawa!
 
Mchambuzi siku zote naungana na wewe katika hoja zako juu ya chama chetu lkn kwa analysis ya haraka haraka hadi sasa inaonyesha hakuna jipya kwenye huo uchaguzi unaousema tungoje matokeo...kitu ambacho kabla ya uchaguzi tayari nusu ya matokeo yameshajulikana nani in nani out je unapinga hilo?naamini unajua ukweli kama mtu unayefatilia siasa, kifupi still hakuna collective goals kama chama shv bali kuna wao na sisi huu uchaguzi hadi sasa umeshindwa kubadili hilo kwa vitendo bali linanenwa kwa maneno subiri move inaendelea
Ni kweli mkuu, kwani tangia Nyerere aondoke, NEC imekuwa ni chombo kinachotumiwa na watu fulani fulani kulinda utawala wa waliopo, au kwa waliopo nje, kujipanga to succeed utawala uliopo; mengine yote ni secondary, na hata haya ya secondary, NEC ambacho ndicho chombo cha maamuzi ya juu kabisa ya chama, maamuzi yake in the post Nyerere period bado ni kufanikisha kulinda utawala uliopo, au kuwapanga waliopo nje to succeed; in the end, chama ngazi ya taifa kinatumia muda mdogo sana kushughulikia kero za wanachama wa ngazi za chini; ndio maana na wao wamegeuza uongozi huko matawini n.k kuwa miradi ya kujipatia fedha waishi, especially baada ya kanuni mpya baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia ambayo inasema: SHUGHULI ZOTE ZA CHAMA ZITAKUWA NI ZA KUJITOLEA. Mtu unabaki kujiuliza, unajitolea ili kupata nini in return, tuzo?
 
On the other Note nafikiri EL naye ni mtu wa ndoto ya Urais long time na hii ni personal objective yake...ukiuliza vision ya taifa liende wapi ndani ya miaka yake 10 atakua hana jibu.[/QUOTE]

Hapa ni kweli tupu.Lowasa anaota uraisi.Ndio ndoto pekee ambayo hajaitimiza. Alitaka kuwa maarufu na mwenye pesa nyingi, akafanikiwa. Bado uraisi tu. Wewe fikiria tu..,mbali na kashfa zote hizo, hata kama ni za uongo...kwa nini bado unataka tu kuongoza? Duh..i love this country!
 
Nyerere alitawala robo karne,hatukutoka kiuchumi lakini Korea Kusini,Botswana,Malaysia ,na Singapore zilizokuwa sawa kimaskini na TZ mwaka 1960 ZILITAKATA KIUCHUMI,sisi umasikini-mali na umasikini-akili umeongezeka pia,mpo?Kuna mfumo mchafu tangia uhuru na gharama zake ni hizo.
Kila Rais aondokaye madarakani CCM anamwachia dhaifu kuliko yeye ili asiwajibishwe na ili abakie mtu maarufu.Sasa dawa yao ni kuukata huo mzizi-kitovu wa CCM,kwa gharama yoyote,mwenye kujua kusoma na afahamu!
 
Maskini kikwete, amekuwa miongoni mwa maraisi mabutu na kibogoyo. Hana meno hata kidogo.. Jamaa sijui anawaza nini. Nathubutu kusema anapenda maisha la filamu.

Nafiki washauri wake wana nidhamu ya uoga au kichwani mwao hawana kitu. Ndo maana wanashindwa kumpa ushauri.

jamaa hasikilizi ushauri wowote wa maana na manufaa kwa taifa zaidi ya kuogopa aliwaudhi toka 2005 na kujidai hataki kuchukua maamuzi tena yatakayoudhi wachache na kufurahisha wengi...huwezi kua kiongozi wa taifa maskini halafu ukategemewa utapendwa na kila mtu..huu ni ujinga
 
Dream come TRUE for him yet hatuwezi kumpongeza kwani aina ya rais kama yeye hatakiwi nchi yoyote. Ingekua nchi za kifalme basi angefaa kwani mamlaka ya kuongoza nchi tungempatia Waziri Mkuu wa nchi na yy kua ceremonial Figure tu.
 
You have a point lakini bila Lowassa, Kikwete asingekuwa Rais na ndio maana Lowassa anaendelea kuwa nguzo kubwa sana ya CCM from 1993 mpaka sasa; Continuation ya nguvu ya Lowassa itakuwa determined na dynamics lakini muhimu zaidi matokeo ya chaguzi za ndani za CCM mwaka huu wa 2012;
Mchambuzi nafikiri mtoa mada anatuasa tusichague mtu anayetaka kutimiza ndoto yake ya kuwa raisi tu bila kujua majukumu ya uraisi ni yepi? Sasa turudie makosa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom