Elections 2010 Kuna haja ya kuwa na sera ya taifa badala ya sera ya chama?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara pasipo kupata majibu as kwa nini kusiwe na SERA YA TAIFA?

Katika vipindi vya Chaguzi za Raisi na Wabunge vyama mbali mabali vimekuwa vikimwaga au kunadi sera ( Ambazo kimsingi ni ahadi ya nini kitafanyika kama wananchi wakivichagua na kuvipa dhamana ya kuongoza Taifa kwa miaka mitano) zao kwa wananchi bila kueleza ni namna gani hizo ahadi zitatekelezwa, na mara nyingi vyama hivyo vimekuwa vikiwaeleza wananchi kila aina ya neno tamu ambalo litamfurahisha mwananchi wa Tanzania.

Kwa Maneno Machache Vyama vimekuwa VIKISHINDANA KWA SERA na Si MIKAKATI.

Baada ya kutafakari hilo nimeona si busara liendelee kukaa katika kichwa changu sasa nakuja kwenu wana bodi nikiwa na yafuatayo

1: Taifa liwe na Sera ambayo itaeleza kwa umakini nini kifanyike katika kipindi Fulani, kiwe cha miaka mitano au miaka kumi au vyovyote itakavyoamuliwa, Taifa lianishe Vipaumbele vyake katika kipindi hicho.

2: Katika kipindi cha Uchaguzi badala ya Vyama kushindana kwa Ahadi/Sera, vishindane kwa MIKAKATI ya kutekeleza hayo yote ambayo Taifa linatamani yafanyike, so Badala ya Wananchi kuimbiwa Maneno matamu, Wagombea na Vyama vyao wakabidhiwe Sera au Mipango na Wanadi Wagombea wao kwa kutueleza ni mikakati gani wanayo katika kuwezesha Taifa kufikia maelengo ambayo yatakuwa yameanishwa katika Sera ya Taifa.

Naomba kutoa
 
Last edited:
Lengo ni kupata viongozi wazuri, Kiongozi Mzuri si Yule anayeweza kusimama jukwaani akasisimua watu, si yule atoae maneno matamu matamu na ahadi nyingi bali ni yule anayeweza kusima na kueleza ni KWA NAMNA GANI anaweza kutekeleza majukumu ambayo amekabidhiwa.

Asante
 
Wakuu hii imekaaje? Naombeni Maoni yenu

Nawakilisha
 
lazima tufahamu kuwa Katiba ya huko tanzania inabainisha wazi kuwa CHAMA NDIO KINASHIKA HATAMU ZA UONGOZI WA SERIKALI.

sasa lazima chama kitunge sera na serikali inafuata sera za chama.
 
Nafkili ingeunganishwa naya mzee Mtei halafu tujadili.... thread nzuri ila ilikosa wachangiaji...jambo la kawaida sana hapa JF.
 
Nafkili ingeunganishwa naya mzee Mtei halafu tujadili.... thread nzuri ila ilikosa wachangiaji...jambo la kawaida sana hapa JF.

Ha ha ha Nashangaa maana kama nakumbuka hii niliipost kwenye Jukwaa la Siasa sasa sijui ni makosa yangu au ya Wakulu (mods) wameamua kuihamishia huku nilikuwa sijashtukia ngoja nicheki na invizibo afanye ze nidifu
 
Back
Top Bottom