Kuna haja ya kurudisha Ngoma ya Mdundiko hapa Dar……….Hebu angalieni enzi hizo………..

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393

[video]http://www.voanews.com/swahili/news/Sunday-magazine/Mdundiko-Ngoma-yenye-jazba-100138659.html[/video]

Hebu tazameni Ngoma hii ya Mdundiko, iliyorekodiwa miaka ya 80s, enzi hizo mdundiko ukiwa ndio umeshika kasi katika jiji hili la Dar. Hapa mtawaona kina Preta, Ummi-Kuluthum, Mwanajamiione, Firstlady, Cantalisia, Mamndenyi, NATA, BlackBerry, Smile, Nyumba Kubwa, King'asti, AshaDii, RussianRoulette, Kabakabana Mwali, BAGAH, bila kuwasahau kina Rejao, Bishanga, The Boss, Kongosho, Losambo, Erickb52, TANMO, Kitalolo, King Kong III Sizinga, MziziMkavu, na wengineo wengi tu…………………….
 
Last edited by a moderator:
Umenikumbusha hii....

Kamtoroka mume wake kafuata mdundiko...
kamtoroka mume wake dafuata mdundiko..

sitakii.. sitakii.. mpaka ngoma ikoleeee
Sitakii.. sitakii.. mpaka ngoma ikoleee... hahahaha...
 
Mtambuzi si kuna baadhi ya sehemu nasikia mila bado inadumishwa? lol
Wiki iliyopita nilikuwa maeneo ya Tandika nikakutana nao bwana.............Nakwambia walinipagawisha mbaya, maana walinikumbusha enzi hizo miaka ya 80s nikiwa ndio nimetia timu hapa Dar,...........Ilikuwa nikiuona Mdundiko ukipita hapo Mwananyamala nilipokuwa nikiishi, nilikuwa naufuata mpaka Msasani.................

Kuna haja ya kuurudisha Mdundiko kama wenzetu wa Brazil na Samba lao au Trindad and Tobago na Matamasha yao.........
 
Umenikumbusha hii....

Kamtoroka mume wake kafuata mdundiko...
kamtoroka mume wake dafuata mdundiko..

sitakii.. sitakii.. mpaka ngoma ikoleeee
Sitakii.. sitakii.. mpaka ngoma ikoleee... hahahaha...

AU
Nipeni kiti nikae nimfundishe mwanangu, undugu wa siku hizi kila mtu kila mtu na mwanae..................
Wape wapeeee vidonge vyao, waklitema wakimeza shauri yao..................LOL
 
mdundiko raha sana bana.....unapagawisha sana....na pia mdumange siku hizi siuoni....
mdumange ndio ulinipatia ndoa.....
 
mdundiko raha sana bana.....unapagawisha sana....na pia mdumange siku hizi siuoni....
mdumange ndio ulinipatia ndoa.....

Hahaaaaa ...mbona ndoaaaa... Mi nahiari umauti kuliko kukosa kucheza gombe sugu..
 
Dah!nakumbuka miaka ya 1999 niko sekondari nilikua likizo tukawa tumenda manzese kununua mitumba tukapita mitaa ya katikati kule midizin tukakutana nao tukaufata bila kujua tukajikuta tuko tandale tunaelekea mwananyamala!yan unanoga na unatembea bila kuchoka!wazirudishe bana!
 
Mdundiko ulikuwa ndio ID ya Dar enzi hizo...............Siku hizi umeadimika, lakini kama ungeboreshwa ingkuwa kama vile Samba la Brazil................Maana watu tungejimwaga mbayaaaa.............Hebu mcheki Preta hapo kwenye Youtube anavyijimwaga................Utapenda...........LOL
 
Kumbe eh..................Muone vile!

hahahhahah!!!hiyo huangalii wanaelekea wapi wewe uko makini na kijungu tu huku unakuta mshkaji wako naye kakitolea macho!!ukijikwaa tu yeye ndo anakuwa mgongoni mwake!kama mnatokea kinondoni unahamaki mpo buguruni na kandambili umezishika mkononi kijasho kinakutoka
 
Kuhusu mdundiko, hebu ni wasimulie.

Tatizo langu ni kwamba nimezaliwa na kukulia Dar ya enzi hizoo. Haya mambo ya mdundiko wa miaka ya 80 hata mimi yalinitatiza na kunipa wazimu. Mimi langu lilikuwa ni "gombe sugu" na kidogo kwa kuangalia lakini si kwa kucheza "tokomile" Watu wa "vanga" walikuwa wananiudhi nyimbo zao zilijaa majungu na masengenyo wakati mwingine hadi kwa waliowaita wanapigwa jungu.

Hapo kati kidogo wakaja wandengereko na sanaa yao ya "madogori" mtaani kwentu kulikuwa na mzee mmoja maarufu sana kwa madogori alikuwa anaitwa,Mzee Nyangatika. Lakini mwisho wa matatizo ni mdundiko. Hii kitu ingejaribiwa kufanywa na kuingizwa kwenye ile hali ya kitamasha tamasha kama ya matamasha ya Brazil, nadhani ingekuwa bomba sana.
 
[video]http://www.voanews.com/swahili/news/Sunday-magazine/Mdundiko-Ngoma-yenye-jazba-100138659.html[/video]

Hebu tazameni Ngoma hii ya Mdundiko, iliyorekodiwa miaka ya 80s, enzi hizo mdundiko ukiwa ndio umeshika kasi katika jiji hili la Dar. Hapa mtawaona kina Preta, Ummi-Kuluthum, Mwanajamiione, Firstlady, Cantalisia, Mamndenyi, NATA, BlackBerry, Smile, Nyumba Kubwa, King’asti, AshaDii, RussianRoulette, Kabakabana Mwali, BAGAH, bila kuwasahau kina Rejao, Bishanga, The Boss, Kongosho, Losambo, Erickb52, TANMO, Kitalolo, King Kong III Sizinga, MziziMkavu, na wengineo wengi tu…………………….

Hawa kwenye video si wale watu wa "Lambada"?
Ninawapenda watu wa S. Amerika na Carrebeans kwani full kujimwaga.
Uko sahihi mkuu, iko haja sio Mdundiko kurejeshwa tu bali hata "kuuingizwa kwenye katiba" - lol.
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu mdundiko, hebu ni wasimulie.

Tatizo langu ni kwamba nimezaliwa na kukulia Dar ya enzi hizoo. Haya mambo ya mdundiko wa miaka ya 80 hata mimi yalinitatiza na kunipa wazimu. Mimi langu lilikuwa ni "gombe sugu" na kidogo kwa kuangalia lakini si kwa kucheza "tokomile" Watu wa "vanga" walikuwa wananiudhi nyimbo zao zilijaa majungu na masengenyo wakati mwingine hadi kwa waliowaita wanapigwa jungu.

Hapo kati kidogo wakaja wandengereko na sanaa yao ya "madogori" mtaani kwentu kulikuwa na mzee mmoja maarufu sana kwa madogori alikuwa anaitwa,Mzee Nyangatika. Lakini mwisho wa matatizo ni mdundiko. Hii kitu ingejaribiwa kufanywa na kuingizwa kwenye ile hali ya kitamasha tamasha kama ya matamasha ya Brazil, nadhani ingekuwa bomba sana.
umeona eh............Ndio maana najaribu kupiga chapuo hapa...........hata mimi mtaani kwetu kulikuwa na wapogoro wacheza ngoma ya kwao kila jumamosi na jumapili.............hapo utapata pombe za kiasili na vibinti vilikuwa havikosi..........Ilikuwa raha kweli kweli.........
 
Back
Top Bottom