Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Jana nilimsikiliza Tendwa akijadiliana na Mtangazaji wa TBC pamoja na mambo mengine barua ya onyo aliyoiandikia CDM. Kwa namna alivyokuwa akijibu maswali na kuibua hoja, itakuwa imeonekana dhahiri kwa yeyote aliyemsikiliza ya kuwa mheshimiwa huyo hana upeo wowote; na hivyo kuendelea kubakia kwenye nafasi nyeti kama aliyonayo, kunahatarisha zaidi usalama wa taifa kuliko hayo maandamano ya CDM anayoonekana kuyavalia njuga. Ili kumshinikiza kuachia ngazi napendekeza kufanyike kura za kutokuwa na imani na utendaji wa mheshimiwa huyo hapa jamvini.