Kuna haja kwa kampuni ya TIGO kubadili jina hili la matusi?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
TIGO mtaani kwa sasa ni neno tata kwani linafarakanisha watu kutokana na jina hilo kutumiwa kwa matusi,hili linaishusha hadhi na watu waoheshimiana huogopa kuwa na mtandao huo kuogopa kutaja neno hilo.Je ili kulinda heshima ya kampuni si vema kubadili jina hilo kuachana na matusi?Hivi ni nini chanzo cha neno hilo kutumika kama matusi?Wanajamvi changieni.
 
Mkuu ni kweli ila nafikiri tatizo haiko kwa kampuni ya tigo kwa sababu wakati wanalianzisha lilikuwa safi ila tu binadamu na rotten minds zetu. Am sure hata wakija na lingine watu wakiamua wanaweza kulifananisha na kitu kingine. Kuwaambia wabadili ni kuwaonea tu

mtazamo wangu
 
Tigo limekaa vibaya. Hata wakitafsiri voda vibaya haliwezi kuleta tafsiri mbovu. Tigo wabadili jina tu
 
Tutabadilisha hadi tutachoka, hakuna haja yoyote.
 
Tuseme wabadili jina, na hilo nalo likichukuliwa na washashi wakamaanisha kitu kibaya itakuwaje? Itabidi wabadili tena?

Hapa tatizo ni kuwa huwezi kuzuia lugha isiyo rasmi, laiti kama mtu angekuwa anaandika au kutumia neno Tigo vibaya katika mazingira rasmi Tigo wangeweza kuwa na kesi ya kuhusu hatimiliki na alama ya biashara.
 
Inabidi wabadilishe staili tu kama vile Mzee Kenyatta alivyofanya kule Mombasa.

Mzee Kenyatta akitoa hotuba yake mjini Mombasa, watu wakawa wanamshangilia na kusema mzee sisi tupo nyuma yako.

Kenyatta akawajibu " Nyinyi watu ya Mombasa mnafanya nini nyuma yangu, sema twende bega kwa bega. Hapana kaa nyuma angu".
 
Kwa nini neno TIGO limepewa tafsri ya matusi?someone help me-ilkuwaje hata neno TIGO likapewa maana hiyo na siyo neno VODA au neno lolote?
 
Nakumbuka kwanza ilikuwa mobitel, watu wakaita wasichana wadogo wadogo vimobiteli. Then Ikaitwa BUZZ, wababa wapenda vimwana wakaitwa mabuzi. Inaitwa tigo, tayari ishapewa tafsiri nyingine. Nawahakikishia hata ikipewa jina jingine bado watapewa tafsiri mpya. Cha msingi si kubadili jina ila kubadili FIKRA!! Namsapoti Mchungaji Mwema, tubadili fikra, si jina!! Mchungaji Mwema, chunga kondoo wako vizuri.
 
This thread shows how much people are not serious and concentrating on issues. It disappoints to see the way our thinking resources are applied.
Do we still need someone to blame?
mkuu kweli kabisa.....siku hizi JF hamna great thinking.....thread za kipuuzi puuzi kila siku.....alafu kumezuka siku hizi kila kitu udini..kuna watu sijui wametumwa kila kitu wenyewe wanasema ni udini....najua nia yao.....
....msione watu mnaowaulizia wamepotea... ni wapo lakini wanasoma upupu wenu na kusikitika....

....tubadilike thread za upupu hazifai.....kuna thread ambazo mpaka mtu unajiuliza hii ni JF?
 
Kwa nini neno TIGO limepewa tafsri ya matusi?someone help me-ilkuwaje hata neno TIGO likapewa maana hiyo na siyo neno VODA au neno lolote?

tigo awali walikuja na kaulimbiu yao isemayo togi-mtandao ulioenea zaidi pwani. na si unajua pwani kumejaa mambo ya kuruka ukuta?
 
Wanajamii naomba niwape chanzo cha jina la tiGo kutafasiwa vibaya.

kwenye tangazo lao linapomalizika ile O inafanya kama kubana jicho na hicho ndio chanzo kwa hiyo napendekeza TiGo wangeondoa hiyo O kwenye jina lao na kuitwa tiG.

Vile vile kama na nyie mnakaa katika mazingira ya tafsiri pia voda ile V ni tatizo.
 
kwani hilo neno la tigo ni kiswahili au lugha gani mpaka lilete tafisiri mbaya.
kikubwa ni utashi mdogo wa watanzania kutafsiri maneno kwa maana isiyo eleweka.

Neno Tigo lipo kwenye kamusi gani au sisi ndio tunaliendekeza mpaka liwe neno baya?

Hakuna haja ya kampuni hiyo kubadili jina lake.
 
Back
Top Bottom