Kuna Chuo Chochote Kinatoa Mafunzo Namna Ya Kuongea Mbele Ya Kadamnasi?

Hakuna chuo cha namna hyo ndg yng ila vyuo vng ukienda utakuta utaratbu wa PRESENTATION bcoz inasaidia kuongeza confidence mbele ya watu so ukmalza hapo wanaamin mtu utakua na uwezo wa kuongea mahal popote pale even mbele za watu!.
 
Tafuta kitabu kinaitwa 'The art of public speaking' sikumbuki mtunzi lakini ni mhindi, nilikinunua Ubungo bus terminal Dar es Salaam. Lakini pia kuongea mbele za watu lazima uwe na cha kusema, yani uwe na uelewa na unachohubiri, otherwise utachemsha, I mean ni lazima ujenge tabia ya kujisomea ili kuwa na wide knowledge na vivid examples.
 
Practice makes perfect...we jiamini na uwe unaongea tu jiweke kimbelembele kwenye matukio utaweza....ha ha ha ha hiyo kali ya 'msiba oyee'
 
Heshima wakuu...
Nauliza kama kuna chuo chochote hapa nchini kinachotoa mafunzo ya namna ya kuongea mbele ya kadamnasi. Hii inatokana na namna watu mbalimbali tulivyo waoga kuongea mbele ya watu hasa katika sherehe au msibani.
Kuna kisa kilinitokea msibani baada ya kumaliza kutoa heshima kwa mwili wa marehemu na kuwa tayari kusafirishwa, niliombwa nitoe neno la shukrani. Lakini niliweza kukwepa na kumtupia jamaa mmoja aliyekuwa jirani yangu, lakini kumbe yeye ndiye alikuwa mbovu kuliko mimi. Alianza kwa kusema "MSIBA OYEEE"......shukrani kwa mzee mmoja aliyeokoa jahazi.
Naombeni elimu ya namna ya kujiamini nisije kupatwa na aibu kama hiyo........

Njoo SUA utajua kuongea mbele ya kadamnasi
 
Njoo SUA chukua Bsc agric. extension utapata mbinu na namna ya kuongea mbele za watu mkuu
 
Back
Top Bottom