Kuna athari zozote kama mtu akiaamua kuacha ualimu na kufanya hivi?

ENANTIOMER

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
1,419
804
Mdogo wangu alihitimu 'bachelor of science with education' mwaka 2015, hivyo ni miongoni mwa wanaosubiri ajira za ualimu.

Ana mpango wa kuomba kusoma diploma fulani ambayo kwanza ina 'Government Sponsorship', pili ajira serikalini baada ya kuhitimu ni 100%; na tatu diploma hiyo ina maslahi zaidi ya digree ya ualimu.

Matokeo ya kujiunga na diploma hiyo yanatarajiwa kutoka mwezi wa 7, ambao yeye atakua alishapangia shule ya kufundisha.

Alikua anafikiria kua, iwapo atachaguliwa kujiunga na hiyo diploma, basi ataacha ualimu hata kwa kutoroka na kwenda kusoma hiyo diploma.

Anaomba kujua kama kutoroka kwake ualimu kutatawezasababisha athari zozote katika ajira yake mpya (serikalini) baada ya kumaliza hiyo diploma.

Asanteni.
 
iwapo atajaza taarifa zake za awali hapo atakapochaguliwa ualimu,ktka system ya utumishi atakuwa tayari kashaingizwa hivyo akitaka kuajiriwa tena kwa hiyo diploma yake mfumo utakataa,utasema tayari kashaajiriwa,cha kufanya labda aupotezee kabisa ualimu,aangalie maslahi yake yatakuaje
 
asante sana mkuu.
itabidi awe mwalimu tu, maana hana uhakika kama atachaguliwa kujiunga na hiyo diploma.
bahati mbaya matokeo ya kuchaguliwa kujiunga na hiyo diploma, yanatarajiwa kutoka wakati ajira za walimu zilishatoka kitambo sana. anaweza akaacha kuripoti ktk kituo chake cha ajira za ualimu, baati mbaya kwenye ile dipoma asichaguliwe.
 
vipi, hakuna njia salama ya kuacha kazi ktk system ya utumishi na baadae kupata kazi ktk system ya utumishi pia?
 
Mkuu ajira za walimu mpaka bajeti ya serikali ipite..kwahyo inawezekana hyo ishu yake ikatoka kabla ya ajira

ikitoka kabla ya ajira, itakua vizuri kwa upande wake. ila kutoka kabla ya jiraa, means ajira zitachelewa sana, hali ambayo sio nzuri kwa anaosubiri
 
Asubili kwanza km atapangiwa ajira aende akaongee na baadhi ya wakuu wake km watamuelewa anaweza kwenda kusoma na mwisho wa siku akimaliza anaenda kubadili kazi, kuna Mwalimu mmoja nimeshuhudia alitoka kufundisha na kwenda kusoma diploma ya udaktari wa mifugo na yupo mwaka wa mwisho, hivo anategemea akimaliza aende kubadili
 
iwapo atajaza taarifa zake za awali hapo atakapochaguliwa ualimu,ktka system ya utumishi atakuwa tayari kashaingizwa hivyo akitaka kuajiriwa tena kwa hiyo diploma yake mfumo utakataa,utasema tayari kashaajiriwa,cha kufanya labda aupotezee kabisa ualimu,aangalie maslahi yake yatakuaje
ni diploma gani hyo? unaongea kisirisiri wakati unataka ushauri wetu..au na sisi tukupe ushauri kisirisiri...then cha msingi asiende kureport ata kama atapangiwa kama kweli anauhakika na hyo diploma yake...
 
Asubili kwanza km atapangiwa ajira aende akaongee na baadhi ya wakuu wake km watamuelewa anaweza kwenda kusoma na mwisho wa siku akimaliza anaenda kubadili kazi, kuna Mwalimu mmoja nimeshuhudia alitoka kufundisha na kwenda kusoma diploma ya udaktari wa mifugo na yupo mwaka wa mwisho, hivo anategemea akimaliza aende kubadili
asnte sana. nitamshauri afanye hivyo. japo kukaa kituoni kwa mwezi mmoja kisha kuomba ruhusa, inaweza kua na ugumu kidogo
 
ni diploma gani hyo? unaongea kisirisiri wakati unataka ushauri wetu..au na sisi tukupe ushauri kisirisiri...then cha msingi asiende kureport ata kama atapangiwa kama kweli anauhakika na hyo diploma yake...
tatizo hana uhakika kama atachaguliwa kyk hiyo diploma. anataka kuomba kupitia nacte.
 
asnte sana. nitamshauri afanye hivyo. japo kukaa kituoni kwa mwezi mmoja kisha kuomba ruhusa, inaweza kua na ugumu kidogo
Ndio ni ngumu ila watu wanafanya kwa kupitia mlango wa nyuma, kuna watu wanagawana mishahara na mabosi wao ilimradi tu wakasome. Kuna watu waliajiliwa na cheti wakaenda kusoma diploma, wakaenda kusoma bachelor na kazini hakuwahi kufanya kazi
 
kipindi hiki cha huyu mwenye makufuli, sijui kama itawezekana. akifanya hivyo atakua jipu
 
Kila kiongozi ana majukumu yake, mh nae ana majukumu yake so sio kila kitu yeye tu. Mfano kuna ajila zilitoka mwaka jana za diploma ila hadi sasa waliobaki kazini ni wachache kuliko wanaosoma, haya kuna ajira zimetoka mwez wa 2 mwaka huu still walipata hizo ajira wapo walibaki makazini na wapo waliopo machuoni. Kila kitu kina mipaka yake
 
kwa ushauri wangu....kwa sababu amesoma science na science ina soko... bac anaweza kuacha ajira atakayopangiwa... kwa sababu hata asipopata hyo diploma? ualimu anaweza akaomba hata private schools na akapata vizuri kabisa bila shida yoyote.... kama anaweza asubirie tu hiyo diploma
 
Kila kiongozi ana majukumu yake, mh nae ana majukumu yake so sio kila kitu yeye tu. Mfano kuna ajila zilitoka mwaka jana za diploma ila hadi sasa waliobaki kazini ni wachache kuliko wanaosoma, haya kuna ajira zimetoka mwez wa 2 mwaka huu still walipata hizo ajira wapo walibaki makazini na wapo waliopo machuoni. Kila kitu kina mipaka yake
nimekuelewa sana mkuu. ajali kazini
 
Back
Top Bottom