Kuna aliyewahi kuingiza gari kutoka Japan?

Mie nataka kununua gari lakini nitakuamini vipi kuwa wewe siyo tapeli kama matapeli wengine? Maana mimi nataka toyota Funcargo lakini hofu imenijaa, waTZ hatuaminiani kabisa!.
 
nataka suzuki samurai 550cc,siyo vitara ni zile za miaka ya 90's nina 5mil.niambie nisubiri muda gani kuipata hapo offisini kwako
 
huko kote sawa kwenye masuala ya fedha inakuwaje usije ukasema tutume japan kwenye acounty yako mzee eleza vizuri biashara yako inamashaliti gani mikataba ikoje sio unatoa no za simu za japan mzee
 
kama unashida na gari la kutoka japan naomba unitafute ni kupe bei ya magari.Unachatakiwa kufanya unaniambia aina ya gari mwaka na rangi unayopenda,nitakupa bei ya kununua FOB kulisafirisha na kuli-clear bandari utakuja kulichukua officen likiwa na namba zake karibu sana.

unawza kunipigia moja kwa moja kupitia na mba hii ya japan +818046886066 au +25575342450 pia barua pepe info@cesmatrade.co.tz malipo yote yatafanyika baada ya kupata gari lako.
 
kama uko serious na gari nipigie simu au email nikupe maelekezo utalipia gari lako baada ya kufika dar
 
Kwa nini mtu asionane na wewe au kufika ofisini kwako bali kuishia tu kutoa mawasiliano ambayo hubadilika mda wowote?
 
nadhani siyo sahihi kuanza kutoa hisia negative kwenye biashara ya mtu, tunahitaji sana wazawa watupatie hizi online business na tufaidike wote, shutuma hizi za kuitana utapeli pasipo ushahidi hazijengi jamii yetu, pia ningeshauri mtoa mada kuwa transparent zaidi ili aweze kujenga trust, unaweza ukaweka short profile ya biashara yako kama vile full names, physical contacts, Registration docs, referees ambao ni wateja uliosha wauzia magari in case one wants to confirm quality of cars which you import, hata banker wako unaweza weka wazi, hii itaongeza imani ya mtu anayedhamiria kukupa biashara

jamani tum-support mwenzetu huyu, sipendezwi na kuona wapakistan wanakwenda japan wanafungua kampuni za magari halafu watanzania tunafungua website zao na kuagiza magari huku tukimwacha mtanzania mwenzetu anatafuta wateja hapati, zama za utapeli w kijinga zinaisha na ninauhakika huyu mdau yupo serious

hayo ni mawazo yangu tu wakuu
 
LAT umeongea ukweli kabisa. Jukumu la kujiridhisha na manunuzi ni la mteja, lakini Muuzaji inabidi aweke wazi kila kitu kinachoonyesha uhalali wa biashara yake. GADAF ameshasema utalipia ofisini kwake baada ya gari kufika dar, sasa sijui hizi tuhuma za utapeli zimetoka wapi?
Only Serious Minds can understand his fellow's mind....
 
Weka maelezo ya kutosha hata kama mtu atatoa pesa zake kwa manunuzi ya gari ajue inakwenda wapi na kampuni yako ipo wapi ina matawi wapi?
 
Gadafi inaonekana anauza magari mkononi,nakushauria gharamia mtu akutengenezee online platform ya kuuzia magari yako.uweze kuweka picha na references za wateja wako.
pia ikiwezekana tuambie ofisi ipo wapi,siku hizi siyo lazima uwepo samora,hata home kwako ni ofisi tosha,tena ikiwa home it is more secure kwani huwezi kuhama ghafla.
if you need a guideline how to move your business online get niPM
mtazamo wangu.
 
Wadau nina shida ya Kuagiza gari ya mizigo kama ya ton 3 toka japan. Nimekuwa nafuatilia kampuni tatu ambazo ni Autorec, tradecarview na japaneseexport car. naomba mnisaidie ni kampuni gani ambayo huwa ni wakweli wa vitu vya ili nisije ingizwa mjini.
 
Speedy! mitandao yote uliyotaja inaaminika ie reliable. Hivyo, songa mbele angalia chaguo lako na zinagatia taratibu zinazohitajika
 
WanaJF,
Nimeona gari nzuri kwenye website ya Autorec ya kule Japan na nikawasiliana nao kuwaeleza dhamira yangu ya kulinunua gari hili. Lakini baada ya mazungumzo yetu, mara email kutoka kwao zikawa hazinifikii. Nikaongea na mdogo wangu anaishi USA ili ajaribu kuwasiliana nao kwa niaba yangu. Majibu kutoka Autorec yanamfikia mdogo wangu bila tatizo lakini copy ya majibu direct kutoka japan hayanifikii. Cha kushangaza mdogo wangu akiforward email kwangu zinanifikia. Cha kushtushwa zaidi siku za karibuni nimepokea simu yenye namba 773800589 wakizungumzia my interest ya kununua gari. Hawa watu siwajui na wala sijawahi kuongea na mtu yeyote kuhusu mpango wangu wa kununua gari. Hivyo nimekuwa na wasiwasi kuendelea na hii deal hata baada ya Autorec kunishauri tuwasiliane kwa fax badala ya emai.. Sasa ombi langu ni kama kuna member yeyote amenunua gari siku za karibu anipe ushauri kuhusu uaminifu wa kampuni hii. Pili je, kuna member ameshapata tatizo kama langu? Saidia tafadhali. Hili gari nimelipenda sana.
 
Ni gari aina gani ndg yangu ? Autorec wana agent wao hapa Dar na ndio huyo aliyekupigia ni lazima apate kamishemi yake !! Jaribu kuangalia Beforward hawana longolongo na bei zao ni reasonable mie naagiza kwa Mara kwa mara
 
Mzee utaingizwa mkenge, mimi pia nliikuta gari nzuri kwenye website ya tradecarview.com nikawasiliana na jamaa yuko Japan ili afuatilie.
jamaa alivyofuatilia akaambiwa atoe pesa na gari ataipata baada ya siku 30.
kumbe ukishawapa pesa hawakupi ile gari uloiyona wanakutafutia mshipa mwengine wanakutumia. Ikifika huku TZ unakuwa huwezi tena kuirejesha Japan. So becareful
 
Ni gari aina gani ndg yangu ? Autorec wana agent wao hapa Dar na ndio huyo aliyekupigia ni lazima apate kamishemi yake !! Jaribu kuangalia Beforward hawana longolongo na bei zao ni reasonable mie naagiza kwa Mara kwa mara

kweli hawa Beforwad hawana longolongo.
 
Ni gari aina gani ndg yangu ? Autorec wana agent wao hapa Dar na ndio huyo aliyekupigia ni lazima apate kamishemi yake !! Jaribu kuangalia Beforward hawana longolongo na bei zao ni reasonable mie naagiza kwa Mara kwa mara

Ni site pekee ambayo ukiipata proper address yao hawanq longolongo.

Ni wazuri wanakuonyesha gari karibu kila kona na bei ni mchekea. Kama ni Autorec tafuta wakala wao waliopo Bongo wakulapue maana jamaa ndiyo nadhani wanaoongoza kwa bei ghari za magari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom