Kuna aliyewahi kuingiza gari kutoka Japan?

Kwa kuongezea, malori, mabasi na pickups (pamoja na d/cabin) hazina kodi ya uchakavu. Yaani unaweza kuleta la mwaka wowote na kodi zake ni 25% import duty, 20% VAT. Nipo kwenye process ya kutoa d/cabin ya 1993. Kwa sasa pale TRA hapafai kabisa...magari mengi wana "uplift" bei ..BALAA TUPU!!
 
Kama hauna haraka waachie kila kitu hawa ila kama una haraka hawa jamaa hawafai, mi niliagiza gari july 2007 nikalipata february 2008, nitaka ku cancel transaction wakaniambia wanakata 20% ya CIF niliyolipia yaani ilikuwa nuksi. Ila magari yao ni quality sana hawa jamaa.


....Asante, Mkuu. DuH! Miezi Sita ni mingi sana! Kweli labda uwe na haraka nalo! Na ukiagiza mwenyewe huwa roughly inachukua muda gani mpaka kuingia hapo bandarini?
 
Wafanyakazi wanasamehewa VAT (20%) tu, lakini shida utakayopata kujaza na kusainiwa hizo fomu hata huo msamaha hauna maana, kodi zilizobaki wanalipia. Hata matrekta halikadhalika.
Note:
1. Cars/trucks used less that 10 yrs:Kodi zake ni, 25% import duty, 20% VAT, 5%or 10% (depending of the engine size), so taxes ni 50% or 55% of CIF value. Plus, port charges.

2. Kama imetumika zaidi ya miaka 10, then ongeza 25% tax (scrap tax) on top of 50% or 55%. Jumla 75 - 80% of CIF.

Ukitaka kufuata utaratibu huna haja ya kuhonga mtu. Ila ukitaka kodi zipungue kidogo hapo ndio akili mumtwi.

Mkuu natofautiana na wewe hapo kny matrekta.....! Matrekta yapo kny category ya Agricultural inputs so VAT ni exempted sawa na other capita inputs nyingine!

Pia suala la wafanyakazi wa serikali ni kweli kuna exemption ya VAT ambapo usumbufu wake ni kuwa unatakiwa uwe na importation documents incl proforma invoice ambayo utaipeleka pale hazina then, huko nako kuna mchakato unaohitaji muda kidogo na ndiko wanakoandika cheque kwenda TRA ya amount ya kodi uliyotakiwa kulipa, then wewe unalipa kodi nyingine na kutoa gari lako!

NB. Sio magari yote yanayoagizwa na wafanyakazi yanaqualify kwa exemption, like VX na other expensive cars haziqualify!
 
....Asante, Mkuu. DuH! Miezi Sita ni mingi sana! Kweli labda uwe na haraka nalo! Na ukiagiza mwenyewe huwa roughly inachukua muda gani mpaka kuingia hapo bandarini?
Toka Japan mpaka Dar ilichukua mwezi mmoja tu. Tatizo ni kwamba hawa jamaa wanajua kila kitu kuhusu bongo, ukiagiza gari ambalo ni chini ya miaka 10, mfano kwa mwaka huu gari yoyote kuanzia mwaka 2000 itakuwa haina uchakavu (penalt ya scrap) wanaweza kuwahishia, Ila ni 30 days meli kuondoka Japan mpaka kuingia Dar
 
Habari za leo.

Naomba mwenye uelewa juu ya gharama za uagizaji wa gari kutoka Japan. Information nilizopatiwa kuhusu gari yenyewe ni kama ifuatavyo:

Mode: Nissan Wingroad
Year: 2000
Kms: 92,000
Engine: 1.5
Trans: Automatic
FOB: US$1,500/-

Tafadhali naomba mwenye kufahamu gari inayouzwa bei hiyo mpaka niisafirishe, kulipia kodi zote na kuitoa bandarini (Dar es Salaam) nitatumia kiasi gani cha fedha.

Kama nitakuwa nimepost mahali ambapo si pake naomba muihamishie mahala husika.

Asanteni sana,

Chaka
 
Chaka,

Tafuta thread alianzisha member anaitwa Dullymo.....kule kumeelezwa kila kitu kuhusu uagizwaji wa magari...au unataka tukusaidie kuitafuta?
 
Chaka,

Tafuta thread alianzisha member anaitwa Dullymo.....kule kumeelezwa kila kitu kuhusu uagizwaji wa magari...au unataka tukusaidie kuitafuta?
Nimejaribu lakini sijaipata. Kama kuna short-cut ya jinsi ya kutafuta previous threat nitashukuru kama nitaelekezwa.

thanks,
Chaka
 
Nissan wingroad???? ndio maana i decided to remain old school ford roadster 1932...gademu
 
NL,

Kama ulikuwa hujajua, au kuambiwa na mwanaJF yeyote, basi leo nitaweka hazarani hapa kwamba wewe jamaa ni kichwa, and you are always there to offer quick and reliable solutions to any requesters!

Big up Mkuu, and i admire you for your assistances!

Keep Moving pal!

Ha!ha!ha!ha!ha! PJ....tinasaidiana tu mkuu.......mambo ya Agape mzee!
 
ndugu nakushauri uachane nayo hiyo gari kwa sbb utatozwa gharama kubwa kwa sababu ya import duty itakuwa kubwa kwani hilo liko kwenye kundi la magari chakavu. tafita gari ya kanzia mwaka 2001.
 
Kuna kampuni moja ya japan niliipata hapa hapa kwa wanajamii eti wana bei nafuu.kumbe bei zao zipo f.o.b badala ya c.i.f dsm
nikafikiri kweli ni nafuu ah wapi bei ni ileile tu ndugu zangu.
 
Kuna kampuni moja ya japan niliipata hapa hapa kwa wanajamii eti wana bei nafuu.kumbe bei zao zipo f.o.b badala ya c.i.f dsm
nikafikiri kweli ni nafuu ah wapi bei ni ileile tu ndugu zangu.

Bei ni ile ile na ipi?
Wauzaji wote wanakwambia kama Bei ni CIF au FOB! na hata kama ni FOB utapewa kikokotoo kukusaidia kutokana na wapi unalipeleka gari lako. Ukweli ni kwamba kununua moja kwa moja JP ni nafuu, ila ukubali risk ya kuletewa gari tofauti, gari bovu, au kupoteza kabisa pesa, ukiogopa bassi wape faida kwa kuwachangia wasioogopa. Hata hivyo si lazima wote tuagize magari JP, wenzetu watakula wapi?!!!

Mimi naona sehemu nzuri ya kununua gari online ni tradecarview, unakutana na wauzaji wengi na machaguo kibao, nzuri zaidi siku hizi wana PAYTRADE unalipa kupitia kwao, na hawaachii pesa mpaka shipment iwe confirmed!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom