Kumwambia mkewe ukweli sasa kuna mgharimu

@Nyie mnaolilia aya, kwani mnasoma aya ama maneno?

Story ya huyo bwana inahuzunisha, jamaa ni mtu mstaarabu sana, maana kama kaweza kumuhusisha mkewe na kumtaka radhi sidhani kama kuna busara na wema mkubwa kama huu.
Huyo Mwanamama ni kahaba material ambae possibly alijificha ila sasa kapata uwanja wa kufanya na kuyaonyesha yaliyomjaa
ni laana tena laana kubwa kwa bibi zee kama hilo kufanya umalaya hadharani tena kwa mtu aliekuepushia kifo, maana kumwambia kabla hajamuathirisha ni upendo mkubwa sana aliouonyesha huyo bwana
 
Hii kesi ni ngumu sana...ndio maana hadi sasa hajajitokeza mchangiaji aliyejikita kwenye hoj na kutoa ushauri wenye manufaa...pengine utu update wakitoka kijijini watakuwa wamepewa ushauri gani na namna watakavyoupokea. Iila huyu mwanaume naye ni shujaa...sio wengi tunaoweza kuangalia upuuzi mkubwa kiasi hicho kwa macho... it is too much...
 
Dah, hii kesi ngumu sana. Ilikuwa vema ulivomwambia, lakini kuwahusisha hao wazee wanaowaheshimu hapo mnapoishi ni nzuri.
Fupa gumu hili ndiyo maana watu wanakimbilia kudai aya na summary.
 
Duh hata kama ndio kuchanganyikiwa, huyo mmama kazidi at that age aisee!
tena asipoangalia na yeye ataupata, kwa sababu hao wanaume wengine anaoenda nao hawatamwambia kama wanao(ukimwi)
 
Huyu jamaa anahitaji kumpeleka mkewe kwa ushauri nasaha maana inakuwa too much mpaka alete mwanaume ndani ya nyumba hapa na bana kha! hata kama mwanaume kakosa hii adhabu ni kubwa mno

Shida yote ya nini? Kishaleta kidume mpaka ndani usisahau.

Hapa solution ni divorce tu basi! PERIOD!
 
Kosa alilofanya bwana mkubwa hakufuhata taratibu stahili katika kutoa hiyo habari ngumu kwa mkewe, huwa kuna stages lazima kuzifuhata ili kupunguza mshituko kwa recipient. Angetumia hata mshauri nasaa.... hata kama alitaka iwe siri. Na kwa stage waliyofikia kimahusiano sidhani kama itakuwa ni siri tena kama alivyotegemea.

ANYWAY ISHATOKEA .... USHAURI WANGU:

  • Hapo hakuna tena ndoa kwasasa... Mke ameheuka kupitiliza...familia imebomoka... Kilichobaki awapange watoto waweze kuendeleza ujasiliamali aliouanzisha haraka..... Familia isije poromoka zaidi maana mke hawezi tena kuangalia mbali ameshakata tamaa....(Asikatishe masomo ya watoto)
  • Aangalie kwa makini mtoto yupi anaweza chukua jukumu la kuendeleza miradi aliyonayo na aanze kumjenga haraka, kwa mila zetu huwa tunaangalia mtoto wa kwanza ingawa si mara zote chaguo hilo linaleta matokeo chanya - Uaminifu na umakini wa mtoto ndo kitu cha muhimu zaidi na sio ukubwa kiumri.....
  • Asimsahau mkewe - Atafute mshauri nasaha au psychologist kuanza kumsaidia mkewe kisaikolojia anaweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida (Ni wajibu wake kuhakikisha hili linaanza mara moja....Maana yeye ndo chanzo cha tafrani hii yote .... pity You
Nikipiga picha ya formation ya familia yake ilivyokuwa inakwenda vyema....! Inauma saaana.... Mbali na kuwa amekuwa mkweli kwa mkewe hawezi kukwepa lawama za yanayotokea....Anastahili kubeba lawama zooote kabisa.... Sukari aliyokuwa anatafuta nje ndo imeleta janga kwa familia yake...foul play...Is an irreversible lessons kwake na kwetu.... SAD
NAJARIBU KUPIGA PICHA INGEKUWA MKEWE NDO STERLING WA HII MANENO... INGEKUWAJE????????

Kwenda kijijini kwa wazazi sidhani kama itapunguza tatizo.... maana suala la ukimwi huko vjijini kwetu ni Baadoo hasahasa kwa wazee wetu.... mapokeo ya huko yanaweza ongeza machungu zaidi na kwao... Elimu na uelewa baaadoo.
 
Shida yote ya nini? Kishaleta kidume mpaka ndani usisahau.

Hapa solution ni divorce tu basi! PERIOD!

Kwa kweli hata mimi naona bora tu waachane...................

Huyu mwanamke kawa kichaa na kachanganyikiwa kabisa.....................

Asipoangalia ataupata huo ukimwi na yeye
 
jamani kumbe kuna wanawake wakatili kiasi hiki, inasikitisha sana. If possible wanaweza kwenda ht kanisani wakapate ushauri kama kwa wazazi itashindikana ila huyo mama atakuwa amelaaniwa tena hafai kuwa mama kwsbb wamama wanaaminika kuwa wamejaaliwa hulka ya ukarimu na huruma.
 
nimeisoma yote..akili za huyo mwanamke soon naye atalipata gonjwa. Ila source ni huyo mme wake. Wanaume tulizaneni makwenu
 
MPAKA HAPO NILIKUWA NIMELOWA JASHO MWILI WOTE HUKU NASIKIA BARIDI.. NIKAMPA POLE afu nikamwambia arudi nyumbani kwake akaongee na mke wake wakikubaliana wekend waende kijjini kwao wakazungumze na wazazi wao tangia mwanzo mpaka hapo walipofikia wawasikilize wazazi nadhani watawapatia ushauri mzuri sana utakao wajenga, akanambia kwa unyonge nashukuru sana mdogo wangu nitajaribu kufanya hivyo tukawa tumeachana huku mimi siamini baba kama yule aeza kuwa na matatatizo kiasi kile,,,NIMEAMUA KULILETA HUM KAMA NI WW U NGE MSHAURIJE.. Katika maongezi ya huyo baba cjaongeza wala kupunguza kitu labda tu mpangilio.

Hivi kweli 'Maisara' unaamini kabisa matatizo ya ndoa ya watu walioishi pamoja kiasi cha kuwa na watoto wa5, wa kwanza akiwa chuo kikuu...yatamalizwa kwa kuongea na wazazi kijijini? Kama wawili hao na utu uzima wao, huyu kaamua kujifanya mjanja 'kanasa', huyu naye anataka kumuonyesha mwenzie kuwa ni mjanja zaidi yake...kweli wazazi walio kijijini ndio watatue?!
 
Hatariiiiiiii...mi naona waachane tu.mwanaume hamgaie baadh ya mali amuache aende zake..yeye abaki na watoto wake..na kama bado damu yake inachemka yan bado anamatamanio ya ki mwili atapata mwanamke mwenye hali kama yake..

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
huyo mwanamke kapitiliza aisee....

Ila dawa ndogo mume akate matumizi toze ya mke kwa sasa, duka si keshafilisi? Aishie kula tu hapo nyumbani...la kuleta wanaume nalo adili nalo hiyo ni dharau ya hali ya juu..... mke akili ikimkaa sawa aende kupata ushauri nasaha
 
dharau kubwa sana hiyo alofanya, tena huyo mwanaume ana busara, ingekua mie ningemtimua siku hiyo hiyo.... Akajifunze kwanza....


Shida yote ya nini? Kishaleta kidume mpaka ndani usisahau.

Hapa solution ni divorce tu basi! PERIOD!
 
nimevaa kiatu cha hiyo familia na namba sawa ila kimegoma kuingia kabisa jamani ngoja nikatafute namba 45 du my kaka HorsePower njoooo nivalishe kiatu eeeeeeeeeeeeeee
 
Last edited by a moderator:
Elimu ya mama kuhusu gonjwa la ukimwi na kuwajari wahathirika ni ndogo sana.mama apelekwe kwenye ushauri nasaha atahacha ayo mambo ya kijinga.
 
Watu wanaoana wakati hawaamini katika ndoa
Hapa ndio shida huanzia, msuko suko kidogo tu
Ndoa shaghalabhagala
 
Hivi kidogo inaanzia ngapi??


Kweli huyu mama kashindwa fanya kwa usiri hadi alete usoni?

Kuna mibazazi inapata Ukimwi afu inaambukiza wake kwa hiari
Ila kweli 'kama mti hajalala njaa hawezi jua njaa'

huu sio "msuko suko kidogo"
 
Mimi nimemuelewa. Kaka ebu omba Mungu akutie nguvu. Meza dawa za kurefusha maisha ili uweze kulea wanao mpaka pale watakapofikia. Huyo mwanamke mwache,akili zake haziko sawa, atakutafuta na hatakuona.

Wish you the best!
 
Hivi kidogo inaanzia ngapi??


Kweli huyu mama kashindwa fanya kwa usiri hadi alete usoni?

Kuna mibazazi inapata Ukimwi afu inaambukiza wake kwa hiari
Ila kweli 'kama mti hajalala njaa hawezi jua njaa'
hii situation ni kubwa na inahitaji calm head na ushauri from wazazi/padre/psychiatrists. sisemi kafanya vizuri kuleta wanaume ndani lakini she didn't know how to react. Im sure ataona makosa yake na kuomba mume msamaha after consultation hasa ukizingatia mume kamwambia ukweli na kumlinda. sijaelewa 'kama mti hajalala njaa hawezi jua njaa'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom