Kumuuliza mtu afya yake sio ustaarabu?

Haya bwana, sijui mwanasiasa?
Ntakuwezea wapi

Tuko pamoja

Actually kuzibuka kwangu ni compliment.

Zibuka = husikii, una namna ya kufikiri yako mwenyewe bila kujali noise za nje.Capable of transcending the common dialogue and even starting a paradigm shift/ attaining the required escape velocity.

Highly recommended.

Bila kuzibuka hamna maendeleo.
 
Ujue mie mama yangu half cast wa kizaramo na kizgua
baba yangu ni half cast wa kibelgij na kombai

sasa mie ni quarter cast
kiswahili is my fifth language
yaani ukinipeleka kwenye mangereza umeua

Mie bakwata. Kukonda sio neno zuri sana banaa, eboo!
 
Mtu pekee ambaye naweza ku comment kuhusu mwili wake ni ndugu zangu wa tumbo moja, baba na mama, and my hubby kama hatujaonana for sometime.

Nyie mnaongelea kumuuliza mtu kama amekonda wakati mie nimeshapata tabu in several incidences kumuangalia mtu usoni kwa jinsi alivyokwisha. Yani umeshawahi kukutana na mtu ukatamani kugeuza njia? Si kwa nia mbaya ila kwa vile you feel like you are not able to pretend that everything is okay.

Mfano nilikutana na teacher wangu mmoja amekwisha na ngozi imepauka (ni prof huyo) na alikuwa anamkaribia Capt. Komba kwa unene. But nilishasikia kuwa ana kisukari kile kibaya (si HIV; I hope am right) lakini bado hata yeye amekuwa hapendi tena kuongea na watu kwa sababu wengi wanamwangalia macho ya huruma na maswali na unajua ni ngumu kuanza kuwaambia watu "unajua nina kisukari" ukizingatia hawajakuuliza.

Hivyo huwa napenda kuwakwepa watu wanaotaka kuwa na privacy.
 
in addition, je kumuuliza ntu hali yake ya afya pale inapokuwa 'imedorora sana' ni utu au kukosa utu?


Mkuu FA, kama ni mtu ambaye mmeshibana sana basi hakuna tatizo ila kama hamna mazoea ya karibu basi sio vizuri hata kidogo kumuulizia kuhusu afya yake.
 
@nyumba kubwa
sasa ukimkwepa utajuaje anataka privacy?
Wakati hata hujaongea naye?
 
Mi nshakuwa na experience na watu ambao afya imedorola. Hawataki macho ya watu wala sympathy. Hata ikitokea mkagongana uso kwa uso, basi pretend as if huoni difference; sio unashangaa shangaa.

@nyumba kubwa
sasa ukimkwepa utajuaje anataka privacy?
Wakati hata hujaongea naye?
 
Hapa stamford bridge ni half time blues - 1 Man City - 1.

enhee tuendeleeni na mada
 
Wabongo tuna aina ya utamaduni wetu nadhani vitu vingine ni vidogo vidogo sana ila tumevifanya havihojiki......
Pia msibani kuuulizia kilichomuua marehemu ni ishu...
Nadhani mapokeo tu!
 
Kuulizauliza mambo ya faragha sio vizuri, na sio kwa afya tu bali lolote ambalo ni la faragha kama vile kazi, dini, kuoa/kuolewa, kuachika n.k. Ikiwa unajihisi uko karibu naye sana, kwa nini uulize usisubiri akuambie mwenyewe? Si ustaarabu!

Yuko dada mmoja tulikutana jeshini, yeye alikuwa afande mimi kuruta na tulikuwa marafiki wa karibu sana. Badae tukapoteana miaka. Siku nilikutana naye tukazungumza mengi, nikaishia kumwuliza una watoto wangapi baada ya kuniambia ameolewa. Yule dada alilia sana, halafu akaniambia hana mtoto na hawezi pata mtoto. Nilijuta! Nilitamani ardhi ipasuke, bora ningenyamaza lile akalisema yeye kama alitaka kulisema.

Tunapaswa kuwacha mambo ya kuulizauliza. Subiri uambiwe!
 
We unamuona mtu kakonda halafu unataka umuulize mbona umekonda???

Unategemea jibu gani hapo???
 
......... Kuna Profesa wangu mmoja wa Uchumi alikuwa anasema yeye hawezi hata kumuuliza mtu "unafanya kazi wapi?" Kwa sababu huwjui kama kila mtu ana kazi, na unaweza kum-embarrass mtu asiyetaka watu wajue kama hana kazi.

.

nimependa hiyo sentensi. kwa ujumla si vema sana kumuuliza mtu kitu kama hivyo, hasa endapo unaona kuwa afya yake imedorora its obvious anaumwa au ana tatizo kubwa kwa kumuuliza unakuwa unamuumiza sana. nakumbuka babu yangu aliwahi kuniambia kam kuna mtu ulikuwa nae nyakati fulani halafu mkawa na maisha mazuri pamoja siku atakapoharibikiwa na maisha halafu ukamuona tokea mbali ni bora wewe ujifiche kwa kuwa kwa kukuona kwako atakumbuka mambo mengi ya nyuma, enzi za maisha yake mazuri na ataumia sana, hivyo wakati mwingine ni busara hata kumkwepa mtu huo hasa kama huna msaada wa kumpa.

lakini pia yawezekana matu akawa alikuwa mnene sana na anafight kupunguza uzito, hapo ukiona amekonda ndio unaweza kumuuliza (but it all depends na kukonda kwake kama ni kwa heri au matatizo)
 
Ni muhimu kuheshimu privacy ya mtu. Actually ni tabia mbaya mtu akikuambia anaumwa ukamuuliza anaumwa nini as if unataka kumpatia matibabu. Ni ustaarabu kuuliza 'umepata matibabu?' kwa ajili ya kufungua maongezi. Asipoona haja ya details, u shld respect and not pry. Na sio issue tu ya afya, its rude kuuliza mtu bei ya kila alichonacho (watch, shoes, ring, car aaaghhrr!), kama kaoa, ana watoto wangapi and personal questions. Ukiuliza tu 'how have u been doing?!' Kama anataka atakueleza.

Umenena vyema kabisa, hivi mtu kumuuliza mamboe "personal" inahusu nini? "Hujambo", "mambo" inatosha kabisa.
 
Ni muhimu kuheshimu privacy ya mtu. Actually ni tabia mbaya mtu akikuambia anaumwa ukamuuliza anaumwa nini as if unataka kumpatia matibabu. Ni ustaarabu kuuliza 'umepata matibabu?' kwa ajili ya kufungua maongezi. Asipoona haja ya details, u shld respect and not pry. Na sio issue tu ya afya, its rude kuuliza mtu bei ya kila alichonacho (watch, shoes, ring, car aaaghhrr!), kama kaoa, ana watoto wangapi and personal questions. Ukiuliza tu 'how have u been doing?!' Kama anataka atakueleza.

but utagundua watu wengi hawajui haya
mtu anakuuliza eti umeoa? unasubiri nini??????
au watoto wangapi?mbona unachelewa ongeza ongeza lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom