Kumradhi wana JF

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Habari zenu wana JF, mimi ni mgeni humu ndani. Nasikitika niliingia bila kubisha hodi pengine kwa sababu ya Giza hivyo sikuweza kuuona mlango uliko, nikaamua kupitia dirishani kwa kuwa madirisha ya humu ni mapana sana. Naombeni mnisamehe kwani sasa ndo nimeuona mlango. Hakuna aliyekamilika isipokuwa ni MUNGU pekee. Nawashukuruni sana kwani licha ya kutambua kuwa nimepindukia halafu nikapitia dirishani bado mmenivumilia.
 
Ahahahaaah!! Mkuu Gazeti umenichekesha sana eti madirisha ni mapana sana ndio maana hukuona mlango.. By the way karibu sana!
 
Karibu saana, nakumbuka uliingia mzima-mzima na makeke.
Karibu saana.
 
Ulivyoshusha nondo za nguvu kule ktk jukwaa la uchumi nikajua wewe mwenyeji,kumbe una kamba mguuni !!!!, lakini ujio wako unafaida sana.
Karibu.
 
MKUU,karibu,ila endelea kutambuwa kuwa jf ina watu wa kila aina,so usishangae ktk jambo lolote lile utakalo liona lipo kinyume na ulivyo tegemea,kwa mfano uchangiaji wa threads na hata jinsi vinjwa vya threads vinavyo kuwa tofauti na threads zenyewe,hehehehe basi ni raha sana

KARIBU BANA
 
Habari zenu wana JF, mimi ni mgeni humu ndani. Nasikitika niliingia bila kubisha hodi pengine kwa sababu ya Giza hivyo sikuweza kuuona mlango uliko, nikaamua kupitia dirishani kwa kuwa madirisha ya humu ni mapana sana. Naombeni mnisamehe kwani sasa ndo nimeuona mlango. Hakuna aliyekamilika isipokuwa ni MUNGU pekee. Nawashukuruni sana kwani licha ya kutambua kuwa nimepindukia halafu nikapitia dirishani bado mmenivumilia.
Karibu sana!
Najua una mengi utatufunulia...bila shaka una mengi.
Gazeti la chama ama la sirikali?
 
jambo Gazeti, karibu sana,wala usihofu pole pole ndo mwendo,karibu sana ila zingatia kanuni.Madirisha nimapana kumbe umeona..........hha ha ha........
 
asante mkuu kwa kukumbuka kwamba ulivyoduri ujio wa pili hukupiga hodi
 
Back
Top Bottom