Kumradhi Sengerema Engeneering Group Limited

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,212
4,515
Ndugu wana JF, kwa namana yakipekee kabaisa na kwa moyo mkunjufu ninatoa hoja ya kufuta kauli nilioitoa kwenye mojwapo ya post zangu ambayo nilipost tarehe 12 july, 2012 yenye kichwa cha habari " Wezi wa Tanesco ni Sengerema Engeneering Goup Ltd".

Kama nilivyo andika kwenye hiyo thread, nimekuja kugundua kwamba kulikuwa na miscommunication uliosababisha hali ile ususani kutoka upande wa mafundi wa kampuni tajwa na kwa afisa wa Tanesco niliripoti hii ishu kwake.

Baada ya kufuatilia kwa kushirikiana na Sengerema Engeneering Group Ltd, nimejiridhisha kwamba post yangu haikuwatendea haki hawa jamaa na ninapenda kuchukua fursa hii kuifuta hiyo post na pia kuwaomba radhi kwa usumbufu wa uliojitokeza kwenye image yao ya biahsara.

Ninaomba kutoa hoja.

Niwaombe radhi wana JF kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na post yangu.
 

Salaam kwa wote,
Mimi ninamiliki biashara ya car wash maeneo ya Mabibo kwenye barabara ya kuelekea Loyola opposite na Jambo Garden.
Nilikamilisha taratobu za kuomba huduma za Za umeme na kufanikiwa kulipa kiasi cha 1,175, 500/= kama gharama za kuunganishiwa umeme 06/02/2012. Mpaka leo, sijaletewa umeme zaidi ya nguzo waliouleta karibia miezi miwili iliyopita.
Leo mida ya saa tano na nusu nilipigiwa simu na kijana wangu akinitaarifu kwamba kuna watu kutoka Tanesco wamekuja kung'oa nguzo ikabidi niongee nao kwenye simu, jamaa wakaniambia kwamba wanalazimika kung'oa nguzo kwasababu watu wanalalamika eti serikali haikuwalipa fidia nilipomuuliza maswali mawili matatu nikaona anashindwa kunipa majibu yakuridhisha ikabidi niende kuongeanao ana kwa ana.
Nilishangaa kukuta gari aina ya Canter yenye namba T845 ASH inayomilikiwa na kampuni ya Sengerema Engeneering Group Ltd. Tulibishana matokeo yake walishindwa kung'oa nguzo baada ya kuishiwa hoja ikabidi niende Tanesco Magomeni kufuatilia.
Nilichoambiwa ni kwamba hawa ni independent contractors wa Tanesco ila kuna wakati wanaiba vifaa kama hivyo kwa matumizi yao ya kampuni. Mapokeo ya Tanesco kwa kiasi yamenionyesha picha kwamba watumishi wa Tanesco wanalielewa hili ila ninashangaa hawachukui hatua stahiki kuondokana na watu kama hawa katka uchumi wetu.
Tunakokwenda mbali kweli. Ngoja tuone!
 
safi sana mkuu...ni jambo la kiungwana sana kuomba radhi na kujisahihisha makosa...ni watu wachache sana wenye huu uwezo

sie wanajamvi hatuna kinyongo nawe pamoja sana
 
Ungekuwa muungwana zaidi kwa kueleza hasa ukweli ulivyo....Unavyoiacha hivi inaonekana kama 'umeshikwa mkono' ili ufute kauli. Tuweke wazi tuache kudhania mabaya....Tunajua hii ni Tanzania everything is possible!
 
Dala safi sana kumbe waungwana bado wapo, ama kwa hakika umefanya ulichotakiwa kufanya na kwa wakati muafaka
 
Uwezo wangumwa kifedha unaweza kuwa mdogo ila siwezi kupokea kitu kidogo kwa maslahi ya wachache mkuu!
hata andrew alishikishwa kitu kidogo/alitishwa akaja kufuta kauli yake. Tatizo hatuambiani ukweli ukoje ndo maana tunajiuliza kwanini unafuta kauli?
 
Back
Top Bottom