Kumradhi Mh Zitto Kabwe

Tatizo halikuwa ni ufisadi hivyo huna haja ya kumwomba radhi. Kimsingi hoja kubwa ilikuwa ni kwa namna gani mitamabo ambayo iko kwenye dispute ingeweza kuuzwa au kununuliwa kabla ya dispute iliyokuwa chini ya usuluhishi kwisha? Jingine sheria za manunuzi haziruhusu kununua vitu chakavu au vilivyokwishatumika. Hili ndo tulilombishia huyu Bwana mdogo na siyo jambo jingine. Kama wewe ulimwita fisadi uliteleza kutokana na uchungu wa nchi yako na kutokana na majeraha ya Richmond ambayo yalikuwa bado mabichi. Hivyo hustahili kuomba radhi kwa hilo kwani unampa kichwa cha bure. Mitambo hiyo haiwezi kuuzwa mpaka mgogoro ulioko kwenye usuluhishi uishe.
 
Mhh watu wanabadilika sana! Reasons wanazo wenyewe!

Zitto hakupingwa kwa kuwa alitoa mawazo ya kununua mitambo bali mitambo aliyotaka inunuliwe ni ile ambayo ilikuwa na virusi. Hivyo ilitakiwa isafishwe kwanza ndiyo ije issue ya kuinunua. Kampuni zilizokuwa zinatoa huduma ya umeme zilikuwa nyingi. Je Mitambo ya dowans ndiyo ilikuwa bora kuliko yote? Ilikuwa ikizalisha umeme mwingi kuliko yote?

Zitto alikuwa na uwezo wa kutoa mawazo yake kwa njia nyingine siyo kushauri kununua mitambo ya kifisadi. HAPO ALICHEMKA. HATA TAIFA LIWE KIZANI KABISA ALICHEMKA.

Tuna uhakika gani kuwa huu mgawo unasababishwa na ukame? Maana kwenye report walisema kuwa mgawo umekuja kwa sababu ya ukame na ubovu wa mitambo ikiwemo songas, kihansi mmoja na hare. Kwanini hii mitambo iharibike wakati huu aliopredict Dr. Idrissa? Hapa kuna something fishy.

Ongera kwa couarage yako kwa kuomba msamaha lakini that doesnt change the fact that ile mitambo niya kifisadi, udanganyifu ulitumika hivyo hakuna haja ya kuinunua bali ni kuichukua tu kwani ni mali yetu walituibia hawa. Tumewapa hela za bure.

OPEN YOUR MIND FOR THE SECOND TIME BRO.
 
kma ni kweli ulipost thred y kumtukan mhe.zito nkupongeza kwa uungwana wako wako wa kumuomba radhi kupitia jukwaa hilihili ulilomtumia,
''nchi yetu hivi sasa ipo taabuni shauri ya wajinga wachache wasioona mbali ni kweli yawezekana mitambo ile ni ya kifisadi lakini by that time we had no option lakini watu wakaona labda kama vile kuna watu fulani watamake kwelikweli,huo haukuwa uamuzi mzuri'',
inafsi ni mfuatiliaji mzyri wa television series ya kimarekani ya 24,kuna seasons zingine mfano season 3 au season 7 jack bauer analazimika kufanya mahusiano na magaidi just ili apate anachokitaka na kwa kwetu tulichokitaka ni nchi kuwa kwenye umeme ili shughuli za uzalishaji mali zisisimamae,leo hii nani anaweza kutueleza ni mamiliono mngapi yanapotea kutokana na viwanda au ofisi mbalimbali kuwa hazifanyi kazi?au ghrarama ambazo zinakuwa incurred kwa ajili ya majenereta?
BANIANI MBAYA LAKINI KIATU CHAKE DAWA

Kama ni ujinga unao mwenyewe. Hivi wewe kwa akili yako uko tayari kuwa malaya kwa ajili ya mlo wa siku moja? Kuwa tayari kufa kwa ajili ya kulinda nchi yako. Natumaini ungekuwa umepita japo mgambo ukiachila mbali JKT usingeweza kuandika upuuzi kama huu. Naamini wewe hufikirii mbali kabisa. Unajua matokeo ya kudeal na kitu kilichoko kwenye dispute? Kaa kimya kuliko kupost upuuzi.
 
Nasisi tulioshimoni je? No Dowan even the sun. Better to stay as always

Let the heavens fall upon us. We are ready to die rather than purchasing delapidated and illegally acquired Dowans generators.
 
Mh Zitto, nianze kwa kukiri mimi nilikuwa miongoni mwa wana JF wengi tuliokuzonga kwa kejeri, shutma, kashfa na dhihaka kadha wa kadha kuhusiana na msimamo wako kwenye suala zima la ununuzi wa mitambo ya Dowans.

Mheshimiwa, ulikuwa sahihi kwa kusimamia kile unachoamini ni sahihi. Hii ndio sifa adimu ya kiongozi. Naamini hata wewe mwenyewe ulijua toka mwanzo kuwa uamuzi wako wa kutetea ununuzi wa mitambo ile hautakuwa popular na pengine ni kitanzi cha kisiasa. Lakini kwa ujasiri usiomithilika uliendelea kujenga hoja na wengi tulitia pamba masikioni mwetu na kukuita majina mabaya lukuki. Binafsi nilikwenda mbali zaidi na kukuita fisadi. Hili ndilo limenisukuma kuandika waraka huu mfupi ili kukuomba msamaha kwa maandishi yote machafu juu yako. Naamini tupo wengi wa aina hii lakini wenzangu wanakosa uthubutu wa kukiri na wanajichimbia kwenye keyboard zao.

Taifa leo lipo latika kiza, kwa sababu ya watu wachache waliokataa ushauri wa wataalam. Wale "wapiganaji" wanaona soni nyuso zimewashuka wanatapatapa kutafuta justification ya uamuzi wao mbovu ambao umeligharimu na utaendelea kuligharimu taifa kwa hasara kubwa.

Mheshimiwa watani zangu wazaramo wana msemo ufuatao "akutukanae kilabu cha pombe usisubiri kesho yake na wewe mrudishie matusi yake huko huko kilabu cha pombe" Kwa kuwa kashfa nilizitoa hapa JF nalazimika kuomba msamaha hapa hapa JF na ni matumaini yangu utanisamehe.

Nimalizie kwa kukiri na kusema kuwa Mh, wewe ni hazina ya taifa hili. Kama kiongozi vision yako ni kubwa kuliko umri wako. Pamoja na kuwa wanasiasa wanaepuka sana kujiingiza katika masuala tata kwa kuchelea kushusha credibility zao wewe umeweka utanzania wako mbele bila kuogopa kupoteza umaarufu wako wa kisiasa and spot on, you got it right.

Bravo Mh Zitto na endelea na misimamo yako thabithi yenye manufaa kwa taifa letu.

Mheshimiwa naomba kuwasilisha

"Brother katika watu wajinga ni wewe kabisaaa,unachotetea hapa ni nini?.Kama alivyoandika mtu mmoja miafrica ndo tulivyo.Baada ya kukataliwa mitambo ya dowans hawakujua kama umeme utakatika?.Najua kuwa mitambo mingine inachukua muda kutengeneza, je baada ya kujua kuwa mitambo ya dowans haistaili kutumika na Idrisa akatwambia kuwa,tutaitaji umeme wa dharura kwanini hawakuanza process za kuagiza.Wewe ni mpuuzi na Zito kabwe nae ni mpuuzi ndio nyie mafisadi kabisa.Hatuwezi kununua mitambo ambayo kesi zake bado ziko mahakamani, na bado zinajadiliwa na bunge.
 
DARK CITY LABDA TUBAKI WAWILI HATA MIMI NAKUUNGA MKONO ZITTO HAKUWA SAHIHI. hATUWEZI KUVUNJA SHERI A ZA MANUNUZI KWA KUNUNUA MITAMBO CHAKAVU. pIA KUNUNUA MITAMBO AMBAYO MUSTAKABALI WAKE MPAKA SASA HAUJULIKANI. kUNA SWALI LIMEULIZWA WATU WOOOTE WANAIKANA DOWANS, JE HELA HII ATALIPWA NANI? OFISIS ZAO ZIKO WAPI? KAMA NI CHAKAVU KWA NINI IUZWE BEI KARIBU MARA 2 YA KUAGIZA MIPYA.

MIMI KWANGU NI AFADHALI MGAO KULIKO KUNUNUA DOWANS

Hey Shangazi,
Nimeipenda font hiyo!..lol
 
Tatizo ni ukosefu wa mipango endelevu katika nchi yetu...hatuna vipaumbele vya taifa, tunakurupuka na kuzima moto wakati wote...ni aibu pamoja na hali tulizopitia, uzoefu wa tatizo la umeme nchini kwetu mpaka leo tunashida ya umeme...hivi hakuna watu wakufanya mipango katika shirika la umeme??? Umeme ni basic comodity/service kwa kila mtu hakuna mtu ambaye atakataa kutumia umeme kama ana access nao...why dont we invest heavily into it...
Dr.idris was a presidential apointee na walikuwepo watu wenye uzoefu kwenye shirika la tanesco ambao walikuwa na uwezo wa kuliongoza lakini kwa kutaka kuingiza siasa jk alimteua huyu bwana wa uchumi kuongoza shirika la uhandisi.....lilikuwa ni kosa sana...idris was not the right person to run the company..and i hope this time no such mistake is repeated on his successor...
Zitto i hope u r not going to say shits on ur meeting...hatuwezi kuhalalisha wizi eti kwakuwa utatusaidia tusife njaa..misimamo mengine haina tija....
 
Mimi nafurahia angalau kuona kuna watu wako serious wanapotoa hoja, humu JF kuna watu wamejaa vidudu vichwani mwao kila wanapoandika wenzao huona ni utani, mara nyingi huua hata hoja ya msingi kabisa na kuendekeza madudu, hata wengine hujisifia eti wao hawaandiki ila ni watching dogs. Inakera kweli! Mimi nadhani ukitaka kuwa watching dog kaa kimya usibweke hovyo bila vina.

Kuna mambo mengine ni ya kiutani na hivyo wanaochangia nao wanachangia kiutani, labda kuwafanya watu wacheke kidogo na waendelee mbele kwa furaha. Lakini kuna mijitu inakatisha kila mahali na kukatisha tamaa mwendelezo wa uchangiaji, hivi kuna ugumu gani kutambua hoja nzito na hoja za vichekesho?

Nampongeza sana mtoa hoja MASATU kwa kujieleza bayana. Kwa kuwa ameona kuwa aliharibu na sasa anasafisha kupitia njia zilezile. Huo ndio uungwana. Nina hakika Zitto akisoma atamsamehe hapo hapo, kwani ni mwanasiasa anayejua anafanya nini, hata kama ni kijana kiumri, kakomaa kisiasa maana ameyapitia mawimbi hayo. Nilitegemea wengine wangejiunga kutambua mchango wa Masatu na kutubu kama na wao wameona. Sasa tuko gizani Tanzania, bado kuna watu wanachukulia utani japo Taifa linadhurika na giza hili. Nadhani kama kungekuwa na umoja wa kimawazo JF ingejengeka vizuri zaidi kuliko watu wanavyoyachukulia mambo yanapoletwa kujadiliwa.

Wakati fulani niliona wanatanzanet fulani wakikandia sana JF kwamba hakuna jambo la maana. Kumbe ndio natambua kwamba mtu akisoma warukiaji watatu mfululizo wenye hoja zisizo na mwelekeo unaofanana na hoja ya msingi anaweza kishia majumuisho hayo. JF ina michango ya maana na tena mizito kweli, tena inasomwa na watu wengi wenye mamlaka na wanayafanyia kazi. Lakini virukia njia vikiharibu wanaweza vipi wenye dhamana kuchjumuisha mawazo yetu ili wafanye tunachowashauri kufanya?

Kama mtu hajui kubainisha hoja nzito na vichekesho, ni bora akae chini ajifunze kuandika, maana JF inahitaji hoza za watu wote zisomwe.

Leka
 
Masatu unaona sasa ulivyojivua nguo kwenye hii post yako? sasa kulikuwa na faida gani kuwa kuwadi wa zitto?Matokeo yake ww na zitto wako wote mmevuliwa nguo.Soon utaelewa ni kwa nini Zitto alitetea kununuliwa kwa ile mitumba na utaona aibu, halafu utakuja kutuomba sisi msamaha.
Nashukuru huyu mtu walimpiga stop kugombea uwenyekiti CHADEMA, ni kama ndumilakuwili.. time will tell tutaijua tu rangi ya huyu kijana.
 
Mimi nafurahia angalau kuona kuna watu wako serious wanapotoa hoja, humu JF kuna watu wamejaa vidudu vichwani mwao kila wanapoandika wenzao huona ni utani, mara nyingi huua hata hoja ya msingi kabisa na kuendekeza madudu, hata wengine hujisifia eti wao hawaandiki ila ni watching dogs. Inakera kweli! Mimi nadhani ukitaka kuwa watching dog kaa kimya usibweke hovyo bila vina.

Leka

Mimi sitaki kukaa kimya, kwani nikikaa kimya hata hicho kidogo nilichonacho moyoni bila kuchangia nitakuwa sijajitendea haki wenzangu pia.

Mimi kwa upande wangu DOWANS sikubaliani nayo bora tukae gizani.
 
Hivi wale walio on the ground (whatever the hell that means) wanaamini kuwa tukinunua hiyo mitambo tnka kampuni e feki ya dowans ndiyo giza litatoweka TZ? Kama hii ndiyo imani basi tuna tatizo kubwa zaidi.
 
Naamini tupo wengi wa aina hii lakini wenzangu wanakosa uthubutu wa kukiri na wanajichimbia kwenye keyboard zao.

Taifa leo lipo latika kiza, kwa sababu ya watu wachache waliokataa ushauri wa wataalam.

Sidhani kama mko wengi wa aina hii, mie nafikiri ungeisemea nafsi yako mwenyewe kuliko kusemea nafsi za wengine. Taifa halipo kwenye giza kwa sababu uliyoitoa hapo juu, Taifa liko kwenye giza kwa sababu ya wachache ambao wanataka kuendelea kujaza matumbo yao. Taifa liko kwenye giza kutokana na uzembe wa Tanesco na Serikali yetu, Mdau unachosahau ni kwamba it is not the first time Tanzania ipo kwenye mgao, Ni miaka kama 15 iliyopita au zaidi. Sasa Zitto si kaja juzi tu, "Dont give him the credit" alichemsha hata ukimtetea; Kitendo cha kukubali kununua mitambo ya Dowans ni kukubali kwamba Richmond ilikuwa right. And that is exactly what they wanted Taifa liingie gizani ili kuwepo na presha ya kununua mitambo ya Dowans. We will not buy them to give them satisfaction, Serikali itafute njia mbadala. Utashangaa hata miaka 10 ijayo bado tatizo la umeme litaendelea kuwepo.
 
Ah, nchi hii kila kukicha comedi tuuu,haya sijuwi kesho itakuwaje!!!
 
wataalamu hawakushauri tununue mitambo ya wizi, walio toa uamuzi wa kununua mitambo ya wizi ni idrisa akisaidiwa na baadhi ya wapambe ambao wengine hatujajua nini ili kuwa interest yao. walicho sema wataalamu ni kununua mitambo in general, specific ilikuja kwa watawala au viongozi, ku-source hiyo mitambo ya wezi, ambao mpaka leo hii aliyekuwa analipwa hizo hela hatuambiwe, kwanini? kama hakuna kitu cha ajabu?

Wacha kucheza na maneno hapa, wataalamu walikuwa wazi kuwa mitambo ya kununuliwa ni ya Dowans simple kwa kuwa ndiyo iliyokuwa available.

Mbona unatufanya Watanzania sote hatuna maana ukiwapamoja na wewe kwa kusema kuwa mchezo huu wote ulikuwa wa mtu mmoja na kwa sababu ya mtu mmoja huyo si serikali na Rais wake, si Bunge na wapiganajiwake Si Jamiiforum ikiongozwa na August, walioweza kungamuwa ubaya wa huyu mtu na kutafuta njia mbadala na kuepukana na mgao.

Wacha Bwana! kama tulishindwa kwa kila hali na kamati ya Bunge ikithibitisha kuwa hatuwa zifaazo zimechukuliwa lakini tatizo bado lipo ni dhahiri kuwa wataalamu walikuwa sahihi na kama si hivyo basi kwa umoja wetu na tutafute suluhisho badala ya lililopendekezwa na Fisadi Rashid (kwa maoni yako, kwani mimi sioni kuwa alistahili lawama)
 
Mimi nafurahia angalau kuona kuna watu wako serious wanapotoa hoja, humu JF kuna watu wamejaa vidudu vichwani mwao kila wanapoandika wenzao huona ni utani, mara nyingi huua hata hoja ya msingi kabisa na kuendekeza madudu, hata wengine hujisifia eti wao hawaandiki ila ni watching dogs. Inakera kweli! Mimi nadhani ukitaka kuwa watching dog kaa kimya usibweke hovyo bila vina.

Kuna mambo mengine ni ya kiutani na hivyo wanaochangia nao wanachangia kiutani, labda kuwafanya watu wacheke kidogo na waendelee mbele kwa furaha. Lakini kuna mijitu inakatisha kila mahali na kukatisha tamaa mwendelezo wa uchangiaji, hivi kuna ugumu gani kutambua hoja nzito na hoja za vichekesho?

Nampongeza sana mtoa hoja MASATU kwa kujieleza bayana. Kwa kuwa ameona kuwa aliharibu na sasa anasafisha kupitia njia zilezile. Huo ndio uungwana. Nina hakika Zitto akisoma atamsamehe hapo hapo, kwani ni mwanasiasa anayejua anafanya nini, hata kama ni kijana kiumri, kakomaa kisiasa maana ameyapitia mawimbi hayo. ''Nilitegemea wengine wangejiunga kutambua mchango wa Masatu na kutubu kama na wao wameona. Sasa tuko gizani Tanzania, bado kuna watu wanachukulia utani japo Taifa linadhurika na giza hili. Nadhani kama kungekuwa na umoja wa kimawazo JF ingejengeka vizuri zaidi kuliko watu wanavyoyachukulia mambo yanapoletwa kujadiliwa''.

Wakati fulani niliona wanatanzanet fulani wakikandia sana JF kwamba hakuna jambo la maana. Kumbe ndio natambua kwamba mtu akisoma warukiaji watatu mfululizo wenye hoja zisizo na mwelekeo unaofanana na hoja ya msingi anaweza kishia majumuisho hayo. JF ina michango ya maana na tena mizito kweli, tena inasomwa na watu wengi wenye mamlaka na wanayafanyia kazi. Lakini virukia njia vikiharibu wanaweza vipi wenye dhamana kuchjumuisha mawazo yetu ili wafanye tunachowashauri kufanya?

Kama mtu hajui kubainisha hoja nzito na vichekesho, ni bora akae chini ajifunze kuandika, maana JF inahitaji hoza za watu wote zisomwe.

Leka

Hivi umesoma post walizoandika wenzako au na wewe ndo mkupukaji? Hatujamlaumu masatu bali tunachosema hakustahili kuomba radhi kwa sababu hatukihitaji na wala hatuhitaji kununua mitambo chakavu tena iliyletwa kinyemela na mtu asiyefahamika (kitapeli). Acha kusupport upuuzi.
 
Wacha kucheza na maneno hapa, wataalamu walikuwa wazi kuwa mitambo ya kununuliwa ni ya Dowans simple kwa kuwa ndiyo iliyokuwa available.

Mbona unatufanya Watanzania sote hatuna maana ukiwapamoja na wewe kwa kusema kuwa mchezo huu wote ulikuwa wa mtu mmoja na kwa sababu ya mtu mmoja huyo si serikali na Rais wake, si Bunge na wapiganajiwake Si Jamiiforum ikiongozwa na August, walioweza kungamuwa ubaya wa huyu mtu na kutafuta njia mbadala na kuepukana na mgao.

Wacha Bwana! kama tulishindwa kwa kila hali na kamati ya Bunge ikithibitisha kuwa hatuwa zifaazo zimechukuliwa lakini tatizo bado lipo ni dhahiri kuwa wataalamu walikuwa sahihi na kama si hivyo basi kwa umoja wetu na tutafute suluhisho badala ya lililopendekezwa na Fisadi Rashid (kwa maoni yako, kwani mimi sioni kuwa alistahili lawama)

Toka huu ushauri wa kununua mitambo ya dowans utolewe muda kiasi gani umepita? kwa nini hao wataalamu wasiwe na plan B? Nani anayecheza na watu hapa?
 
Hivi wale walio on the ground (whatever the hell that means) wanaamini kuwa tukinunua hiyo mitambo tnka kampuni e feki ya dowans ndiyo giza litatoweka TZ? Kama hii ndiyo imani basi tuna tatizo kubwa zaidi.

Mkuu pengine sijasoma post zako zote, ushauri wako ni nini katika wakati kama huu? we all know long term strategies, na zimesemwa tangu JK akiwa huko huko, tukarogwa akapewa urais.

Kuhusu Tanesco tunajua hamna kitu pale, unaweza ukamchukua mtoto wa darasa la nne akaongoza Tanesco.

However, Poor innocent people are dying out there what is the solution NOW!

Your contribution on this matter at hand will be greatly appreciated
 
Walio muita Zitto fisadi hawana budi kumwomba msamaha kwa vile alisimamia mawazo yake.Na hata hivyo mimi binafsi sioni kama mawazo yake ya kununua dowans ni viable soln.

Kitu kilichotakiwa kufanyika ilikuwa niku m-fire Idrisa baada ya kutamka giza ,maana amekuwepo ktk uongozi huo mda mrefu kwa hiyo hilo tatizo walitakiwa kuliona miaka ya nyuma mingi nakulitafutia tsuluhu.Na kama hawakuweza kuliona hilo tatizo basi Hawakufaa kabisa kuwa viongozi .

Technical mistake kitendo cha kuendelea kumbakisha Idrisa pale ina maana alijitahidi kwa kila namna ili kuhakikisha tu kile alichokisema lazima kinatokea.

ni uzembe wa hali ya juu kutomwajibisha Idrisa momentarily baada ya kauli yake.
 
Mkuu pengine sijasoma post zako zote, ushauri wako ni nini katika wakati kama huu? we all know long term strategies, na zimesemwa tangu JK akiwa huko huko, tukarogwa akapewa urais.

Kuhusu Tanesco tunajua hamna kitu pale, unaweza ukamchukua mtoto wa darasa la nne akaongoza Tanesco.

However, Poor innocent people are dying out there what is the solution NOW!

Your contribution on this matter at hand will be greatly appreciated

Mkuu kwa haraka sana unanikumbusha mshikaji wangu mmoja ambaye tulimkanya kutotembea na msichana jina kapuni ambaye alisadikika ni mgonjwa wa Ukimwi. Majibu yake yalikuwa mazito sana na yenye kuumiza mara tatu.. alibwabwaja kama vile tumemshika mkono..
'Ohhh! kwani nyie mna hakika gani kama mimi ni mzima?.. hata hivyo mnataka niwakanyage nyie au?..Wanaume wazima badala ya kuja na ushauri wa maana mnaanza kusema watu wengine wakati afya zenu wenyewe matatani..Mwenye kiu mimi, mwenye kupenda mimi nyie yanawahusu kitu gani kwani Ukimwi nini sii ugonjwa tu kama maradhi mengine!..Sote tutakufa khakuna atakaye ishi milele..Kama ni cost za mazishi nikifa acheni nife nitazikwa na city!'

Tukifikia hapa mkuu wangu nadhani ipo haja yetu sisi kukaa pembeni na kuitazama picha nzima ya Dowans!..

Hata hivyo nitamalizia kwa kukukumbusha vitu vichache sana! ni kweli mwenye kusikia uchungu wa maumivu leo hii ni wewe uliyepo on the ground, lakini kumbuka tu haya yafuatayo..

Wananchi tulipokea hotuba ya waziri Ngereja tarahe 11 December mwaka 2008 pia hotuba ya Mh. rais wetu Jakaya Kikwete ktk kuufunga mwaka 2008 ambao wote walitamka kwamba seriikali haitanunua mitambo ya Dowans hivyo wanajiandaa na ununuzi wa mitambo mipya iki ni pamoja na kuboresha mabwawa yetu ili yaweze kuzalisha umeme wa ziada (short term strategy)..
Hawa ni viongozi wa juu ktk utawala wetu na wasemapo hawa sidhani kama kuna hoja tena au mjadala wa Tanesco au Dowans...na bila shaka walifikia maamuzi hayo kwa kushauriwa na wataalam maanake yaonyesha watu mnafikiria tu kwamba Dr. Idrisa ndiye mwenye wataalam..Wakatuondoa wasiwasi uliofuatia maneno ya Idrisa kwamba taifa litakapo ingia kizani tusimlaumu yeye.

Kufuatia maneno hayo, Mzee Mwanakijiji kama nakumbuka vizuri alimshauri rais wetu JK kuwasimamisha kazi Dr.Rashid na waziri Ngereja mara moja kwa sababu hawa ndio walikuwa kiini cha mchezo huo mchafu wa vitisho kwa wananchi wakati nafasi ya kufanya ufumbuzi ipo na ilikuwepo kwa muda..Hata hivyo, matokeo yake Serikali haikufanya kitu!

Hivyo basi Ushauri wetu wakati tupo kizani, ni kuwa huu ndio wakati wetu sote Watanzania kuonyesha kutoridhika na Utawala uliopo. Kutoridhika na mikakati mibovu ambayo inaturudisha nyuma kimaendeleo badala ya kulalama na mitambo ya Dowans ambayo haiwezi kuondoa tatizo la Umeme nchi ila ni kipozeo cha upungufu uliotokea.

Nitarudia kusema mtambo wa Dowans ni Kibatari ambacho hatukihitaji.. kwa afya ya uchumi wetu na usiri uliojengeka nyuma ya mitambo hiyo ni sawa na taifa zima tumekubali kupokea Rushwa, kinyume cha kiapo cha imani ya kila Mtanzania. Mkuu wakati Dar mnaingia katika mgao wa Umeme kuna wilaya na vijiji huko bara vimeanza kupata umeme kwa mara ya kwanza huo umeme unatoka wapi?.

Aidha, rais Kikwete a step down kwa sababu kashindwa kutimiza ahadi yake kwa wananchi (rejea hotuba yake ya kufunga mwaka 2008, au Dr. Rashid na Ngereja wachukuliwe hatua kali na mipango mipya na yenye uhakika inafuatwa.

Leo tutanunua mitambo ya Dowans na itakuja haribika kama mitambo mingine ambayo hadi leo hii imesimama haifanyi kazi..ni mchezo ule ule wa TRA kuwa na vichwa ambavyo vimesimama na vinatakiwa ukarabati lakini serikali imeshindwa kuwawezesha engineer wetu.

Je, unafahamu kwamba leo hii kwa zaidi ya miaka 20 tunazalisha umeme chini ya kiwango au uwezo wa mitambo tuliyokuwa nayo kwa asilimia 40 au zaidi?.. Tutaendeshaje uchumi wa nchi ikiwa sehemu kubwa ya nguvu za Umeme wetu haifanyi kazi leo tunakuja tegemea Dowans kuwa mkombozi..
 
Mimi sitaki kukaa kimya, kwani nikikaa kimya hata hicho kidogo nilichonacho moyoni bila kuchangia nitakuwa sijajitendea haki wenzangu pia.

Mimi kwa upande wangu DOWANS sikubaliani nayo bora tukae gizani.

Hili alosema Masatu haliweza kutoka hivi hivi bila kutegemea kitu. Labda amenusa kuwa karibia Mh Zitto atatafuta mtu wa kuwa meneja wa kampeni. Na kama hii kazi anayofanya ya kupigia debe Dowans ikifanikiwa, unaweza kupiga hesabu mwenyewe kamba 10% ya zaidi ya 60bn ni kiasi gani. Hata isipopita, downpayment inatosha tu. Ni rahis mtu kuomba kazi njia hii!!
 
Back
Top Bottom