Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mwizi akija na kukuibia kitu ambacho ulikuwa unakihitaji kwa kiasi halafu akaja kukuuzia ukakataa wewe ni mtu makini. Hitaji la kitu chako likikuzidia utapiga magoti kwa mwizi wako akuuzie? Dowans a.k.a Loliondo ni kampuni ya kilaghai kama ilivyokuwa Richmond. Iliingizwa nchini kwa baraka za JK (akilipa deni x) na kwa msaada wa Ra. Nilishasema kuwa hii mitambo ni lazima inunuliwe. Kununuliwa kwake hakuhusiani hata chembe na hali ya umeme nchini. Kwa maneno mengine deni lazima lilipwe na hakuna wa kulilipa isipokuwa serikali. Kama vichwa vyote vya wasomi wetu vinategemea dowans kuiokoa nchi na tatizo la umeme basi inatubidi tuwaulize walipokuwa watoto walikuwa wanapata lishe ya namna gani.