Kumlinganisha Mrema wa 1995 na Dr Slaa wa 2010 ni sawa na nuru ya Mwezi vs ya Jua

Kuhama hama chama na kuhusika kwa Mrema ktk migogoro kulisababisha watu wengi kurudi nyuma na kukata tamaa kwamba hata vyama vya upinzani vipo kimaslahi binafsi zaidi kuliko kuwajali wananchi. Slaa amerudisha imani kwa wananchi kwamba upinzani ni kujitoa mhanga kwa wachache kwa ajili ya wananchi wengi. Mrema aligombea akiwa hata hajui kiwingereza wakati Slaa amegombea akiwa ni Dr (Phd)
 
Mrema na Mkapa wote walikuwa ni wapya; tofauti na sasa ambapo Dr Slaa amepambana na mtu anayetetea nafasi yake ya urais. NCCR walipata wabunge 19 akiwemo mmoja kutoka ukoo wa Nyerere; ikilinganishwa na 23 wa CHADEMA (kwa sasa), vile vile akiwemo mmoja kutoka katika ukoo wa Nyerere.

Ikumbukwe pia kuwa mwitikio wa kupiga kura mwaka 1995 ulilkuwa ni mkubwa kuliko mwaka huu.

Kwa tathmini yangu, Dr Slaa amefanya vizuri zaidi.
 
Acha uzandiki waberoya -hakuna mpambano kati ya mrema na slaa na kama umetumwa na ccm kufanya mchezo huo nadhani tafuta forum nyingine labda ya michuzi utapata wanaokuunga mkono siyo jf, hapa kuna great thinkers na siyo vibweka. Hatuna mda wa kumlinganisha dr slaa na mrema tofauti zao na similaties zao zipo wazi ila kuzijadili hizo tofauti hakuleti tija wala manufaa yoyote kwa watanzania. Wewe kula hizo hela ulizopewa na ccm then ukae kimya watu wameamuka hawana tena utindio wa ubongo no mental slavery. Dont touch our hero dr slaa
 
Amani iwe kwenu wana GREAT THINKERS! Hebu mtu atukumbushe Mh. Agustine Mrema alipata asilimia ngapi za kura za urais mwaka 1995 ili tuweze kulinganisha na asilimia 26 na ushee alizopata Dr Slaa mwaka huu. Lengo nikufanya rough evaluation ya muitikio wa mageuzi ya siasa kwa Watanzania, na tuweze ku forecast itakavyokua 2015 kama mafisadi hawatafanikiwa kuhonga wasaliti (akina Yuda Iskarioti bado wapo hata hivi leo) wakuvuruga mwenendo mzuri wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla!:israel:

Hesabu za asilimia huwezi kuzitumia kuwalinganisha watu wawili, i.e. Mrema na na Slaa. Mfano, kama mwaka 1995 walikuwa wamepiga kura watu 12, mrema akapata kura 3 ingekuwa ni asilimia 25; Lakini pia kama wapiga kura wangekuwa 100, akachaguliwa na watu labda 20 angepata asilimia 20. Hapa utaona kuwa waliompigia kura ni wengi, lakini asimia imepungua.

Kwa case hii ya Dk. Slaa na Mrema mwaka huu tofauti iko wazi kuwa. Mrema alipata kura 1,800,000 (28%) na hakuna mpinzani mwingine amewahi kuvuka hapo isipokuwa Dk. Slaa, ambaye amepata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34.

Wakati huo pamoja na hamasa ya mageuzi, NCCR-Mageuzi ya Mrema ilipata wabunge 16, na viti maalumu wasiozidi 10.

Mifano Mingine hii Hapa: Ujio wa Augustino Lyatonga Mrema kwenye NCCR ulibadilisha sura ya siasa na kukifanya NCCR kuwa chama cha pili kwa nguvu na ukubwa hapa nchini. Ujio wa Mrema uliififisha sana CHADEMA ambacho ngome yake kuu ilikuwa mkoa wa Kilimanjaro ambapo Ndugu Mrema anatoka pia na hii ilijidhihirisha kwenye uchaguzi wa 1995 ambapo NCCR ilizoa viti vya Moshi Vijijini, Hai, Moshi Mjini, Vunjo na Siha wakati CHADEMA iliambulia kiti cha Rombo. Matokeo ya uchaguzi ya 1995 hayakuwa mabaya sana kwani wapinzani kwa ujumla walipigiwa kura asilimia 40 ingawaje walikuwa na uwakilishi mdogo sana bungeni ambapo kambi ya upinzani ilikuwa na wabunge kama 55 (NCCR-19, CUF-22,UDP-3,CHADEMA-3, WANAWAKE 10) kati ya wabunge 275 wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Linganisha na mafanikio ya sasa ya chadema. Soma hapa

Mbali na mafanikio hayo, Slaa amefanikisha kupata wabunge wa majimbo 22, na kura za kutosha kupata viti maalumu zaidi ya 30. Kura zake za urais zitawewezesha kupata ruzuku ya kutosha, bila shaka haitapungua sh milioni 200 kila mwezi.
 
Kwakweli ni aibu ilioje kwa wana JF kukwepa kujibu swali mnakimbilia kukashfu. Wether mrema ni Sane au Insane. Jibu hoja ya mwanzilishi wa thread hii halafu utetezi ufuate. Kumbeza Mrema kwa sababu tu unampenda sana Slaa si sahihi.
 
Mbona hata wewe hujajibu hoja ya msingi kama muanzisha thread alivyouliza na unakimbilia kulalamikia mitazamo ya watu wengine.
Jaribu kujibu hoja kwanza ndipo uwakosoe na wenzako.
 
Hesabu za asilimia huwezi kuzitumia kuwalinganisha watu wawili, i.e. Mrema na na Slaa. Mfano, kama mwaka 1995 walikuwa wamepiga kura watu 12, mrema akapata kura 3 ingekuwa ni asilimia 25; Lakini pia kama wapiga kura wangekuwa 100, akachaguliwa na watu labda 20 angepata asilimia 20. Hapa utaona kuwa waliompigia kura ni wengi, lakini asimia imepungua.

Kwa case hii ya Dk. Slaa na Mrema mwaka huu tofauti iko wazi kuwa. Mrema alipata kura 1,800,000 (28%) na hakuna mpinzani mwingine amewahi kuvuka hapo isipokuwa Dk. Slaa, ambaye amepata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34.

Wakati huo pamoja na hamasa ya mageuzi, NCCR-Mageuzi ya Mrema ilipata wabunge 16, na viti maalumu wasiozidi 10.

Mifano Mingine hii Hapa: Ujio wa Augustino Lyatonga Mrema kwenye NCCR ulibadilisha sura ya siasa na kukifanya NCCR kuwa chama cha pili kwa nguvu na ukubwa hapa nchini. Ujio wa Mrema uliififisha sana CHADEMA ambacho ngome yake kuu ilikuwa mkoa wa Kilimanjaro ambapo Ndugu Mrema anatoka pia na hii ilijidhihirisha kwenye uchaguzi wa 1995 ambapo NCCR ilizoa viti vya Moshi Vijijini, Hai, Moshi Mjini, Vunjo na Siha wakati CHADEMA iliambulia kiti cha Rombo. Matokeo ya uchaguzi ya 1995 hayakuwa mabaya sana kwani wapinzani kwa ujumla walipigiwa kura asilimia 40 ingawaje walikuwa na uwakilishi mdogo sana bungeni ambapo kambi ya upinzani ilikuwa na wabunge kama 55 (NCCR-19, CUF-22,UDP-3,CHADEMA-3, WANAWAKE 10) kati ya wabunge 275 wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Linganisha na mafanikio ya sasa ya chadema. Soma hapa

Mbali na mafanikio hayo, Slaa amefanikisha kupata wabunge wa majimbo 22, na kura za kutosha kupata viti maalumu zaidi ya 30. Kura zake za urais zitawewezesha kupata ruzuku ya kutosha, bila shaka haitapungua sh milioni 200 kila mwezi.

Kweli kabisa, lakini tukija katika hili la mageuzi ya kisiasa ni lazima pia tukubali kuangalia siyo tu idadi ya kura walizopata wagombea na asilimia ya kura zote BALI pia idadi ya wapiga kura waliojitokeza ukilinganisha na wale walio na uwezo au wanaofuzu kupiga kura. Voter turnout ya mwaka huu whilst in absolute terms ilikuwa ni kubwa pengine hata kushinda ya chaguzi zilizopita ila asilimia ya watu wlaiopiga kura ukilinganisha na waliostahili kupiga kura ilikuwa ni ndogo. Hii kwa namna moja au nyingine inaashiria kupoteza mwamko, imani katika mfumo mzima wa uchaguzi, dhuluma kwa wapiga kura n.k

Low voter turnout katika uchaguzi huu ndio kitu muhimu hapa
 
hesabu za asilimia huwezi kuzitumia kuwalinganisha watu wawili, i.e. Mrema na na slaa. Mfano, kama mwaka 1995 walikuwa wamepiga kura watu 12, mrema akapata kura 3 ingekuwa ni asilimia 25; lakini pia kama wapiga kura wangekuwa 100, akachaguliwa na watu labda 20 angepata asilimia 20. Hapa utaona kuwa waliompigia kura ni wengi, lakini asimia imepungua.

Kwa case hii ya dk. Slaa na mrema mwaka huu tofauti iko wazi kuwa. Mrema alipata kura 1,800,000 (28%) na hakuna mpinzani mwingine amewahi kuvuka hapo isipokuwa dk. Slaa, ambaye amepata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34.

Wakati huo pamoja na hamasa ya mageuzi, nccr-mageuzi ya mrema ilipata wabunge 16, na viti maalumu wasiozidi 10.

Mifano mingine hii hapa: Ujio wa augustino lyatonga mrema kwenye nccr ulibadilisha sura ya siasa na kukifanya nccr kuwa chama cha pili kwa nguvu na ukubwa hapa nchini. Ujio wa mrema uliififisha sana chadema ambacho ngome yake kuu ilikuwa mkoa wa kilimanjaro ambapo ndugu mrema anatoka pia na hii ilijidhihirisha kwenye uchaguzi wa 1995 ambapo nccr ilizoa viti vya moshi vijijini, hai, moshi mjini, vunjo na siha wakati chadema iliambulia kiti cha rombo. Matokeo ya uchaguzi ya 1995 hayakuwa mabaya sana kwani wapinzani kwa ujumla walipigiwa kura asilimia 40 ingawaje walikuwa na uwakilishi mdogo sana bungeni ambapo kambi ya upinzani ilikuwa na wabunge kama 55 (nccr-19, cuf-22,udp-3,chadema-3, wanawake 10) kati ya wabunge 275 wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania. (linganisha na mafanikio ya sasa ya chadema. soma hapa

mbali na mafanikio hayo, slaa amefanikisha kupata wabunge wa majimbo 22, na kura za kutosha kupata viti maalumu zaidi ya 30. Kura zake za urais zitawewezesha kupata ruzuku ya kutosha, bila shaka haitapungua sh milioni 200 kila mwezi.

now i realize this forum is truly the home of great thinkers.
 
Mrema hana ishu yeye si mpizani wa kweli na hata mjengoni utaona atakavyo kuwa against wenzake wa upinzani.Slaa ni kichwa jamani lazima tukubali.
 
AMANI NA IWE KWENU WANA GREAT THINKERS
KWANZA NAOMBA NIWAHAKIKISHIE WADAU WOTE WA HII FORUM KUWA HAKUNA MAHALI PENGINE POPOTE KUNA WATU WENYE UWEZO WA KUCHAMBUA MADA KWA KINA KWENYE INTERNATE (ONLINE) HAPA TANZANIA KAMA ILIVYO KWENYE JUKWAA HILI. HONGERENI SANA WADAU KWA CHAMBUZI ZENYE AKILI.

SUMMARY OF THE PRELIMINARY RESULTS
KWA UFUPI TUMEGUNDUA KUWA DR. SLAA YUKO JUU YA MH. MREMA NA HIVYO TUNAWEZA KUMHESABU KAMA KINARA WA JUU KABISA KTK MEDALI YA SIASA ZA MAGEUZI HAPA NCHINI TANGU KUANZISHWA KWA VYAMA VINGI. TUMEGUNDUA KWAMBA TUKIEGEMEA ASILIMIA HATUTAPATA JIBU SAHIHI BALI TUTUMIE IDADI YA KURA NA IDADI YA VITI VYA UBUNGE. HIVYO BASI KWA KURA 2,271,941 ZA DR.SLAA DHIDI YA KURA 1,800,000 ZA MH. MREMA NA VITI 26 TOKA MAJIMBONI VYA DR. SLAA DHIDI YA 16 VYA MREMA NI ISHARA TOSHA KUWA WILBROAD PETER SLAA (PHD) NDIYE CAPTAIN WA KUAMINIWA WA JAHAZI HILI LA MAGEUZI HAPA TANZANIA.

:yield::yield:............NA MSHINDI KWA SASA NI DAKTA SLAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:yield::yield:
 
Hesabu za asilimia huwezi kuzitumia kuwalinganisha watu wawili, i.e. Mrema na na Slaa. Mfano, kama mwaka 1995 walikuwa wamepiga kura watu 12, mrema akapata kura 3 ingekuwa ni asilimia 25; Lakini pia kama wapiga kura wangekuwa 100, akachaguliwa na watu labda 20 angepata asilimia 20. Hapa utaona kuwa waliompigia kura ni wengi, lakini asimia imepungua.

Kwa case hii ya Dk. Slaa na Mrema mwaka huu tofauti iko wazi kuwa. Mrema alipata kura 1,800,000 (28%) na hakuna mpinzani mwingine amewahi kuvuka hapo isipokuwa Dk. Slaa, ambaye amepata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34.

Wakati huo pamoja na hamasa ya mageuzi, NCCR-Mageuzi ya Mrema ilipata wabunge 16, na viti maalumu wasiozidi 10.

Mifano Mingine hii Hapa: Ujio wa Augustino Lyatonga Mrema kwenye NCCR ulibadilisha sura ya siasa na kukifanya NCCR kuwa chama cha pili kwa nguvu na ukubwa hapa nchini. Ujio wa Mrema uliififisha sana CHADEMA ambacho ngome yake kuu ilikuwa mkoa wa Kilimanjaro ambapo Ndugu Mrema anatoka pia na hii ilijidhihirisha kwenye uchaguzi wa 1995 ambapo NCCR ilizoa viti vya Moshi Vijijini, Hai, Moshi Mjini, Vunjo na Siha wakati CHADEMA iliambulia kiti cha Rombo. Matokeo ya uchaguzi ya 1995 hayakuwa mabaya sana kwani wapinzani kwa ujumla walipigiwa kura asilimia 40 ingawaje walikuwa na uwakilishi mdogo sana bungeni ambapo kambi ya upinzani ilikuwa na wabunge kama 55 (NCCR-19, CUF-22,UDP-3,CHADEMA-3, WANAWAKE 10) kati ya wabunge 275 wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Linganisha na mafanikio ya sasa ya chadema. Soma hapa

Mbali na mafanikio hayo, Slaa amefanikisha kupata wabunge wa majimbo 22, na kura za kutosha kupata viti maalumu zaidi ya 30. Kura zake za urais zitawewezesha kupata ruzuku ya kutosha, bila shaka haitapungua sh milioni 200 kila mwezi.

asante...wewe umejibu swali na kujenga hoja iliyoambatana na maelezo stahiki.tofauti na wengine wameishia malumbano tu.
 
Kweli kabisa, lakini tukija katika hili la mageuzi ya kisiasa ni lazima pia tukubali kuangalia siyo tu idadi ya kura walizopata wagombea na asilimia ya kura zote BALI pia idadi ya wapiga kura waliojitokeza ukilinganisha na wale walio na uwezo au wanaofuzu kupiga kura. Voter turnout ya mwaka huu whilst in absolute terms ilikuwa ni kubwa pengine hata kushinda ya chaguzi zilizopita ila asilimia ya watu wlaiopiga kura ukilinganisha na waliostahili kupiga kura ilikuwa ni ndogo. Hii kwa namna moja au nyingine inaashiria kupoteza mwamko, imani katika mfumo mzima wa uchaguzi, dhuluma kwa wapiga kura n.k

Low voter turnout katika uchaguzi huu ndio kitu muhimu hapa[/QUOte
Nani kakudangaya kuwa turnout thsi year ilikuwa ndogo? Nadhani ilikuwa kubwa kukaribia ya mwaka 2005, the easy way ya kupunguza kura za upinzani ni kusema turnout ilikuwa ndogo? This year, kila ngome ilikuwa fired up, chadema, ccm indpendents etc, iweje only 42% ndio waliopiga kura? it does not make any sense
 
kuhama hama chama na kuhusika kwa mrema ktk migogoro kulisababisha watu wengi kurudi nyuma na kukata tamaa kwamba hata vyama vya upinzani vipo kimaslahi binafsi zaidi kuliko kuwajali wananchi. Slaa amerudisha imani kwa wananchi kwamba upinzani ni kujitoa mhanga kwa wachache kwa ajili ya wananchi wengi. Mrema aligombea akiwa hata hajui kiwingereza wakati slaa amegombea akiwa ni dr (phd)

sio lazima uongee kiingereza ndio uiletee maendeleo nchi yako!!! China hawaongei kiingereza, scandinavia wanajenga nchi zao kwa lugha zao, ujerumani, ufaransa, japan nk. Sasa kudai mtu akiongea kiingereza ndio ameelimika! Huo ni ulimbukeni na kujidhalilisha!!!
 
Unajua idadi ya wachina wanaosoma nje ya nchi yao au unaongea tu! Na je wewe una level gani ya teknolojia kiasi kwamba unaweza kujitegemea? Na pia wajua ugunduzi mwingi wa nguvu uchapishwa kwenye majarida (journals) za kiingereza. Kwa hiyo wewe unataka kujifunga na kiarabu tu?
 
Imenilazimu nijibu hoja hii, kwanza kabisa mwaka 1995 ulikua ndo mwaka wa kwanza wa uchaguzi wa vyama vingi. Watanzania walikua na shauku kubwa sana ya kuona maana ya vyama vingi. Kumbuka Mrema mwaka 1995 alikua ndo mtu maarufu kuliko mtu yoyote CCM. Alitumia nafasi yake ya Waziri wa mambo ya ndani na unaibu waziri mkuu kujulikana Tanzania nzima.Kama CCM ingempitisha Mrema angeshinda kwa kishindo, ila alijua hana lake akajitoa. Baada ya uchaguzi wa CCm ilimpitisha mtu asiokua na umaarufu na ambae alikuwa hakubaliki, Mkapa. CCm ilitakiwa kwa wakati ule impitishe Kikwete au Lowasa kumkabili Mrema. Pamoja na hayo Mrema hakutoa upinzani mkali kwa kua hakuweza kufanya kampeni ya uhakika bali ya vitisho na alionekana mbumbumbu sana hasa kwenye mdahalo wa urais.
Kwa upande mwingine mwaka 2010, CCm imempitisha Rais wa nchi mtu maarufu kuliko wote ndani ya CCM na mwenye uzoefu, Kikwete. na maajabu amepata kura ndogo kuliko alizopata 2005. Inaonyesha kuwa DR. Slaa amefanya kampeni nzuri sana na ya nguvu. Sijawi ona Rais anapunguza zaidi ya asilimia 40 ya kura alizopata kwa uchaguzi wa mwanzo. Nampa pongezi Dr. Slaa. Kumlinganisha Dr. Slaa na Kikwete ni ujinga na hakuna uhusiano wa aina yoyote, Dr. Slaa ameshinda kwa mbali sana. Kwanza ameweza kupunguza kasi ya Rais wa nchi na mtu maarufu kuliko wote CCM, na pia ameweza kuimarisha CHADEMA mikoa mbalimabali, tuseme mgombea angekua MKapa na uhakika, CCm ingeshinda kwa kwa asilimia 50 au 52. Tukumbuke pia suala la udini lipo. Kama ingekuani Dr. Slaa na Kikwete wapo baadhi ya wajinga wanaoamini udini wangepigia CUF kwa kua Mkapa ni Mkrist na kwa kiasi CCM ingeathirika sana. Kumbuka kuna wengi wamempigia Kikwete kura japo ni wapinzani kwa kuogopa Dr. Slaa labda ni padri. Nawakilisha
 
Kutokana na kuposha mara kwa mara na kutoa taarifa ambazo hana uhakika nazo, Dr.Wilbroad Slaa ameonekana kupoteza mvuto kwa baadhi ya watu.

Kwa kuwa kila taarifa anayotoa kwa mbwembwe inapingwa na kukanushwa hadharani, jamii kubwa sasa inaonekana kumpuuza sana Dr.Slaa kwa sasa na hii huenda ikampunguzia umaarufu wake na watu kumfananisha na enzi za Augustino Mrema alipokuwa akitoa mabomu kama haya ya Slaa.
 
Back
Top Bottom