Kumlazimisha Nassari kuomba radhi ni bora zaidi kuliko kumtetea!

Hivi karibuni mbunge wa Arumeru Mashariki J. Nassari alikaririwa na vyombo vya habari akitoa matamshi fulani (yanayoonekana kama ya kichochezi) juu ya kanda ya kaskazini kujitenga na kumzuia raisi kufika/kuitembelea Arusha. Kauli hizo za Nassari kwa kiasi chake sio nzuri na wala hazipaswi kutamkwa na kiongozi yeyote na haswa haswa kutoka CHADEMA (kumbuka CHADEMA inahusishwa na ukanda).
Wengi wamejitokeza haswa hapa JF kumtetea Nassari huku wengine wakirefer kauli nyingine mbovu zilizowahi kutolewa na viongozi mbalimbali. Mi naamini kumtetea Nassari hatumsaidii wala hatumjengi kisiasa, jambo la msingi ni wote tukubali kuwa Nassari alikosea na kama tunampenda basi tumlazimishe aombe radhi na kufuta kauli na sio kumtetea wakati kosa lipo wazi na linaonekana kwa kila mtu.

Upuuzi wa kiwango cha daraja la kwanza
 
Kijana Nassari kuwa muungwana waombe radhi wa Tanzania kwa kauli yako. Viongozi wakuu wa CDM kuweni makini ni hawa vijana wenu jaribuni kuwa mnakagua hotuba zao kabla hawajapanda majukwaani.
 
hivi kijana wa miaka 28 ambae hata miezi miwili haijapita toka kawa mbunge anaweza akaongea kitu kikaonekana cha kichochezi?? sioni sababu ya nasari kuomba msamaha mbona lusinde, mkapa na wasira hadi leo hii hawajaomba msamaha...huu uonevu wa mchana kweupee sio mzuri
 
Acha ulofa, mtu akiikosea jamii aiombe radhi na wala si funika kombe mwanaharamu apite, aombe radhi vinginevyo nitakidharau rasmi chama cha chadema.

Jamii ipi aliyoikosea? Mbona Nape na vilaza wengi walishaidharau CDM? WENYE AKILI ZAO WANAVUA GAMBA NJE NA NDANI NA KUVAA GWANDA NDANI NA NJE.

Mimi naungana na Nassari kwa mantiki, maudhui lafudhi lengo na kauli nzima mahali pale na wakati ule.

Magamba nawashauri mzipitie kauri zenu zinazokinzana na mnachotaka kutuaminisha. eg Maisha bora kwa kila Mtanzania, Rais wa 2015 anajulikana na JK na hatatoka kaskazini Onyesheni mfano kuomba radhi maana ni kauli tata sana kulinganisha na hali halisi na katiba ya Tanzania
 
Heri kuteleza mwili kuliko kuteleza ulimi.

Kumbukeni ngome ivumayo sana ...
 
Naamini sio busara kufanya au kuongea kitu eti kwa sababu na fulani aliwahi kufanya.
Binafsi ni shabiki na mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania (ila sio member wala shabiki wa chama chochote kile cha siasa duniani)
nimeona Joshua Nassari kakosea na anahitaji kuomba radhi bila kuangalia au kusema mbona fulani na fulani walisema hivi na hivi na hawakuomba msamaha!
Naamini hii sio kwa faida ya yeyote yule bali ni faida yake yeye binafsi.
 
Hata kwa wale mnaoona kakosea, basi kiukweli hajaanguka, labda kuteleza.

Kwangu mimi hajatetereka, yuko fit na hana haja ya kuomba msamaha.

Utaifa wetu ni wa kiunafiki na wenye nidhamu ya woga ya kutokujadili mustakabali wa nchi vile inavyotakiwa.Upande mmoja ie kwenye issue hii, magamba na wana cdm wengi wanakubaliana, lakini kwenye issue za kuongoza Taifa na ufisadi nk, ni ccm wenyewe, cdm hawana say...Ndo wao(ccm), wenye kutuamulia issue zenye kuligusa taifa, ndo wametufikisha hapa!

Wengine tunafikiri beyond that...

Wenye kusema na waseme, lakini Taifa linahitaji watu wenye msimamo.
 
Hata Mimi sijufurahishwa na kauli ya Nassari na una unapofananisha issue yake na watu Kama jussa ambaye watz tumempuuza unataka Nassari na yeye apuuzwe? Naunga mkono hoja ya kuomba radhi kwani cdm kuna watu makini wa kauli zao. Dr Slaa Nakuomba umpe assigment kamanda Myika ya kumsuka Dogo Nassari maanahofia kuendelea kubwabwaja.
Anahitaji Political treatment kabla hajazidiwa
 
Acha ulofa, mtu akiikosea jamii aiombe radhi na wala si funika kombe mwanaharamu apite, aombe radhi vinginevyo nitakidharau rasmi chama cha chadema.

Inawezekana wewe ndiyo lofa ila hujijui! Kwa Nasari ameikosea jamii ipi? mbona hata uelewi mada? yeye kusema tuunganishe mikoa ndo kuikosea jamii? Unafikiri kwa akili zako fupi angekua amefanya kosa CCM na Polisi wenu mngemwacha hadi leo? Si alienda polisi mwenyewe akahojiwa, mbona kama alitenda kosa mlimwachia? Mngemweka rumande basi coz ndiko wenye makosa wanakokaa! Hakuna kuomba radhi mtu wala samahani, kama kakuudhi wewe basi nenda kwenye vyombo vya sheria ili umshtaki. La sivyo fungeni midomo yenu na hoja zenu sizizokua na mashiko.
 
Nakumbuka mjadala uliozuka baada ya kesi ya Mpiganaji Lema. Baadhi yalikuwa haya:
"Kama ni matusi, mbona Lusinde alitukana zaidi?" na katika mjadala huu wa Mh. Nassari, wengine wamekariri kauli za viongozi wa CCM "Wache wale majani lakini ndege itanunuliwa", "Asiyetaka kulipa nauli ya kivuko apige mbizi" na mengine mengi katika kulinganisha makosa. Watanzania, tusishindane kwa kulinganisha makosa, tushindane katika kutenda mema, au kutumia busara, angalau.

Sisemi Mh. Nassari kakosea au kapatia aliyoyasema, ninachotaka kusema, tusichukue mifano ya "Wao wanafanya kwa nini na sisi tusifanye? Wao wamefanya makubwa zaidi ya hayo kwa nini sisi letu dogo limekuwa nongwa?" Kadri CDM itakavyokuwa inajiepusha na kurudia makosa ya CCM ndivyo inavyojijengea hadhi mbele ya wananchi. Wananchi si wapumbavu, wanaona, wanasikia, wanaishi kila siku katika mateso kwa yale yanayosababishwa na CCM. Tuwaache wananchi waamue, wao ndio wa kuwategemea na ndio waamuzi wazuri katika demokrasia.

Ama kuhusu Mh. Nassari kuomba radhi, hapa ni muhimu busara kutumika ndani ya Chadema na sio kwa shinikizo la wapinzani wao. Kumtaka aombe radhi yeye mwenyewe ni kumsulubu. Katika malezi, ikiwa mtoto kakosea, ni wazazi/walezi wanaoomba radhi kwa niaba ya mtoto wao. Na hilo la mwanzo, tayari Mh. Mbowe hili ameshalifanya na Mh. Nassari mwenyewe ameshalitolea maelezo. Mengineyo yote yaliyobakia na yatakayokuja, "ni upepo tu, utapita."
 
jamani kunya anye kuku akinya bata kaharisha!! Mary nagu alitoa matamshi ya kibaguzi arumeru mashariki hakuna yoyote aliemwambia kitu. Lusinde nae aliongea matusi mpaka mate yakamkauka mdomoni hakuna aliesema! Dogo janja amekazia tu imekuwa nongwa. Hakuna kuomba msamaha nasarri meseji sent

..acheni kufanisha ujinga wa nassari na watu wengine,sijawai sikia mtu anasema tugawe hii inchi na kumkataa rais hasionekane arusha haya maneno kayasema nassari sioni haja ya kumuita mh.huyu dogo ni mjinga aige mfano wa viongozi wake wa juu au wabunge wenzake wa chadema,sijawahi sikia zitto akisema rais hasionekane kigoma au sugu akisema asionekane mbeya au mnyika akisema hata dr.slaa na mh.mbowe hawajawai kusema haya maneno,kama mnamdanganya huyu dogo mtampoteza
 
Kwani hata uko anapoenda si huwa analindwa?Ama nguvu ya umma inawapa mchecheto?

Ni lazima mujuwe hiyo kitu!Kwamba kuna nguvu ya umma, rais wa nchi nzima lakini in reality anatumikia magenge ya majambazi, wapi na wapi, kuna watu hawataki hiyo maneno tena mkuu!Maneno kama "Mafisadi wakikamatwa watayumbisha nchi" sasa nchi ni ya nani?

Kama mnataka mabadiliko(na hii si magamba kwasababu hamyataki mabadiliko), basi lazima kuwepo na jambo litakalowatisha watawala, ni nguvu ya umma, kwasababu katiba bado.

Ukiwa rais wa wananchi wote shida iko wapi?
 
Acha ulofa, mtu akiikosea jamii aiombe radhi na wala si funika kombe mwanaharamu apite, aombe radhi vinginevyo nitakidharau rasmi chama cha chadema.

Kamlazimishe Lusinde awaombe radhi watu wa Arumeru-Mashariki kwanza,na tena mbona umechelewa kukidharau mkuu!? after all ur nothing but loser!
 
..acheni kufanisha ujinga wa nassari na watu wengine,sijawai sikia mtu anasema tugawe hii inchi na kumkataa rais hasionekane arusha haya maneno kayasema nassari sioni haja ya kumuita mh.huyu dogo ni mjinga aige mfano wa viongozi wake wa juu au wabunge wenzake wa chadema,sijawahi sikia zitto akisema rais hasionekane kigoma au sugu akisema asionekane mbeya au mnyika akisema hata dr.slaa na mh.mbowe hawajawai kusema haya maneno,kama mnamdanganya huyu dogo mtampoteza

Wewe unadhani mpaka wamwambie Rais kuwa 'asionekane' huku au kule ??
Vitendo ndio vinazungumza zaidi ya maneno.
Wewe hujui kuwa huyo Rais alipigwa mawe Mbeya, tena sio mara moja, yeye Nahodha, na wengineo.
Vipi hapo unajifanya hujui ???
 
wote mnaongea sana ila wote hamjajaliwa kuwa na uwezo wa kuona mbali. naomba msubiri kuona miujiza muda si mrefu...........................hata wana wa israel wakiwa jangwani walikataa mane wakisema heri wangekuwa misri maana walikula nyama............................unadhani Nasari arikurupuka? jibu ni HAPANA. CDM wanafanya siasa za sayari nyingine siyo hiii tunaishi.........................huwezi kuwaelewa ila wanaona mbali...................CCM bado wanasogezwa king ila wao bado hawajajua hilo........................kila japo liko planned na lina maana kwao.......

Cjaifuatilia hii habari vizuri zaidi ya kuangalia michango pamoja na muanzisha thread.... ila palalisote huu ulioweka hapa ni upuuzi....
Tuache mapenzi ya kijinga yaliopitiliza na kusahau kuwarekebisha wakosaji.....kwa nilivyosoma muanzisha thread jamaa hana budi KUFAFANUA au KUOMBA RADHI....Rabishhhhh
 
Wewe unadhani mpaka wamwambie Rais kuwa 'asionekane' huku au kule ??
Vitendo ndio vinazungumza zaidi ya maneno.
Wewe hujui kuwa huyo Rais alipigwa mawe Mbeya, tena sio mara moja, yeye Nahodha, na wengineo.
Vipi hapo unajifanya hujui ???
Wanajuwa, ndo hilo nililolisema, unafiki.
 
Hivi karibuni mbunge wa Arumeru Mashariki J. Nassari alikaririwa na vyombo vya habari akitoa matamshi fulani (yanayoonekana kama ya kichochezi) juu ya kanda ya kaskazini kujitenga na kumzuia raisi kufika/kuitembelea Arusha. Kauli hizo za Nassari kwa kiasi chake sio nzuri na wala hazipaswi kutamkwa na kiongozi yeyote na haswa haswa kutoka CHADEMA (kumbuka CHADEMA inahusishwa na ukanda).
Wengi wamejitokeza haswa hapa JF kumtetea Nassari huku wengine wakirefer kauli nyingine mbovu zilizowahi kutolewa na viongozi mbalimbali. Mi naamini kumtetea Nassari hatumsaidii wala hatumjengi kisiasa, jambo la msingi ni wote tukubali kuwa Nassari alikosea na kama tunampenda basi tumlazimishe aombe radhi na kufuta kauli na sio kumtetea wakati kosa lipo wazi na linaonekana kwa kila mtu.

Nassari nakutaka uwe muungwana tu, maana majibu yako ya leo kuhusu kauli zako ni yakuzungukazunguka kwani utaheshimika sana na utaonekana muungwana kama utaomba radhi Wanzania kwa kauli zako za NMC.Mimi ni muumini wa CDM na viongozi wake kwani ni watu makini sana na ni watu wa kujenga hoja sio kukurupuka kwani nimekunote tangu siku utatoa shukrani baada ya kuchaguliwa ulitoa maneno ambayo kama ya kitoto. halafu nihisi hujui kuwa wewe ni mbunge na kutoka CDM ambacho kiko pazuri katika harakati za kukomboa nchi, sasa wewe unaleta kauli za kijinga ambazo unawasababishia viongozi wa juu kutafuta namna ya kuondokana na aibu hii ya kauli zako za kitoto.
Ndugu viongozi wa juu wa CDM naomba kumfunda huyu dogo ili asije akaleta balaa na ajue kwamba yuko kwenye chama makini na tumaini la watanzania. Mnyika mpe darasa dogo maana naona mkimuacha atakuwa kama Lusinde au Jussa.
Nawasilisha
 
tuachane na ushabiki usiona na maana kwa akili ya kawaida mtu uwezi kutetea kauli mbovu alizonena otherwise your simple minded
 
Back
Top Bottom