Fernandes Rodri
JF-Expert Member
- Apr 11, 2009
- 518
- 240
Ni sawa kabisa kutujuza . Kwa viwango vyetu eti kwetu Tanzania huyo mama ni celebrity, ingekuwa UK angepewa cheo pengine angeitwa Baroness , lakini kwetu celebrities ni WEMA NA MWENZIWE SINTA.
huyu mama alikuwa mmiliki wa majumba kadhaa maeneo ya masaki, mikocheni na mbezi jijini daressalam hata uingereza alikuwa na majumba, aliendesha biashara zake kwa mafanikio makubwa.
Alianza na biashara ya kuuza kuku na kutengeneza tambi mwanzoni mwa miaka ya 80 kabla ya kujikita na kununua viwanja na kujenga majumba na kisha kuyapangisha
kama wiki mbili zilizopita alivamiwa na wezi nyumbani kwake masaki inasemekana wezi walimpiga pamoja na mlinzi wake wakachukua kama kiasi cha zaidi ya bilioni 1 alifariki baada ya siku 5 kutokana na majeraha aliyopata katika hospitali ya navy masaki
siku moja kabla ya tukio alikuwa ametoka kuuza nyumba yake mojawapo anayomiliki kwa makadirio ya sh 800 milioni na kwenda na ela za mauzo hayo nyumbani kwake
marehemu ameacha mtoto mmoja anayeitwa pamela ambaye alimsomesha kwenye vyuo bora kabisa uingereza na kupata masters in economics na kufanikiwa kupata kazi nzuri uingereza
alikuwa mfano wa kuigwa kuwa alikuwa mfanyabiashara mwanamke aliyefanikiwa kwa jitihada zake hasa ikizingatiwa sio rahisi kwa tanzania ya leo mwanamke kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kama chake
Pamela Shoo ni mchungaji huku UK