Kumekucha: Wanakijiji wachoma matrekta 20 ya wawekezaji Babati

Hapana mama yangu, Misri ni maandamano ya amani. Walichoma jengo la chama tawala kama symbol ya kuukataa utawala wa chama hicho. Walichma magari ya polisi kama symbol ya kukataa polisi wasiwazuie. Lakini yote haya yalifanyika kwa dola siyo kwa raia kwa hiyo hakuna mtu atakuja kulipa kisasi. Lakini hilo la Babati ni tofauti kabisa. Hadi sasa hakuna raia amepigwa na raia mwenzake huko Misri. Ikitokea nitaikemea kwa sababu ni hatari itapelekea visasi, mauaji ya kimbari.

Acha kutuyeyusha wewe. Na hawa wanachoma hivyo viwanda kama symbo ya kukataa kuendelea kunyonywa na gabachoris. Nadhani hata wahindi wa Rites nao wanatakiwa wafanyiwe hivyo na watimuliwe kabisa. Wanatulitea marichmond na Dowans bure. Ile reli ya kati ilikuwa inaoperate japo kwa kusuwasuwa kabla kampuni halijabinafisishwa. Kapewa mhindi limelala usingizi wa pono kabisa. Wachapwe viboko wale waende zao India huko.
 
Mkuu Gurudumu una maana,

Mandela na wenzi wake walifanya makosa,
Samora vile vile alikuwa mpuuzi kupigana na mreno,
Mujoma si angetulia tu mpaka kaburu amwonee huruma?
Akina Kimathi walikuwa wachokozi ndiyo maana wakanyongwa...
Pengine na Tunisia wameshinikizwa na wachochezi........?

Inatakiwa binadamu afikishwe wapi ndipo iwe basi?

Naomba kuelimishwa,

Mkuu, sasa naamini kwamba uwezo wangu wa kujieleza ni mdogo sana. Mkuu, ninamaanisha hivi;

1. Tuupige vita utawala tusipigane wananchi kwa wananchi. A. Kusini kulikuwepo weusi wanaofaidi ubaguzi, hawakuuwawa. Walifocus kwenye dola tu. Ukumbuke pia hawakupigana na kila mtu mweupe, Hapa nimesikia watu wanasema watavamia wahindi wote upanga na kuwanyanganya nyumba. Tukimaliza hilo, wangoni wagundue kuna umeme kilimanjaro hadi vijijini. Waende moshi kuvunja mfumo wote wa umeme. Hilo likiisha Wagogo wanaoidhi nyumba za tembe wakaunguze moto makazi ya wenzao kule Dodoma Mjini, pengine hata wateketeze jengo la bunge! Etc.

2. Kwenye maandamano ya Tunisia na Misri hayakuwa against persons bali against dola. Lakini inajulikana dunia nzima kwamba wananchi wanapokaidi amri ya polisi kwa amani na polisi wakapewa mamlaka ya kutumia Silaha za moto, lazima kutatokea maafa kidogo. Hii huitwa collateral damage. Hii hata iliidhinishwa na Obama jana alipomwambia Mubarak atumie minimal force! How much force is minimal?

3. Kule Tunisia na Misri kuna watu wanaotofautiana kama Hapa kwetu. Tofauti ya kipato, mafisadi, waliodhulumu raia, wageni kumiliki mali n.k. Lakini waandamanaji hawakuwashambulia hawa. Kama wananchi wangepigana wao kwa wao basi Ben Ali angekuwa madarakani hadi leo. Polisi wangepelekwa siyo kuzima maandamano bali kuua wezi na wavamizi. Hutapata sauti ya kudai serkali itoke madarakani kwa sababu wewe ni mwizi au muujumu uchumi.

4. Lakini kuna wakati serikali ikishagundua nia yenu na inataka kuepuka kutoka madarakani, inatumia mkakati huo ili kuwagawa na pia kubadili aina ya mabadiliko mliyokuwa mnadai. Inakoleza chuki miongoni mwenu mnaanza mapambano wenyewe. Mfano ni Zimbabwe. Mugabe alichoche chuki miongoni mwa weupe wenye ardhi na weusi wasio na ardhi. Ghafula akapata kundi kubwa linalomuunga mkono lililomeguka kutoka upinzani. Kisha kundi hilo likawa linawashambulia wapinzani. Hii hali haikuwepo Tunisia wala Misri. Na tunaambiwa hakuna chama chochote cha siasa kilicho anzisha wala kuratibu yale maandamano.

5. Kwa hiyo kwangu mimi, kupora na kuharibu mali za wanaotunyonya na kutunyanyasa, kuua na kujeruhi raia tunaowachukia, vitatufanya tuwekwe kwenye kundi la wahalifu na siyo watetezi wa haki. Tunapolipiza kisasi kwa waliotutesa, na sisi tunakuwa watesaji. Huwa wanasema dai haki kwa kutumia mikono misafi. Tukishapata ukombozi tunaoutaka swala la kurudisha mali zetu ni la kisera, siyo mabavu na kumwaga damu. Call it redistribution policies.

6. Onyo: ili utawala mpya uweze kutekeleza redistribution policies, ni lazima kung'oa mazagazaga yote ya utawala uliopita. Kama walivyofanya Tunisia, ni kama nchi imezaliwa upya. Tukifanya kosa kama la A. Kusini, tutakuwa tumepoteza muda wetu bure. Wanasiasa na watendaji wengi waliokuwa katika serikali ya kibaguzu waliendelea kwenye serikali mpya. Leo hii wananchi hawajapata walichopigani kwa miaka mingi. Bado ardhi inamilikiwa na wazungu, bado weusi wanapata huduma duni za jamii kuliko weupe, bado ubaguzi wa rangi umejikita, bado uchumi uko mikononi mwa weupe. Mandela aligundua amechemsha, kama Nyerere, akang'atuka na kumtoa Mbeki sadaka. Mbeki akashindwa wananchi wakadhani ni yeye hataki wakamweka Mbeki na Mbeki pia ameshindwa. Tatizo siyo rais bali apatheid mamboleo iliyo iliyojiimarisha kisayansi zaidi kwenye serikali ya weusi kuliko ilivyokuwa kimabavu kwenye serikali ya makaburu.

Kwa hiyo ndugu zangu tupigane kuing'oa dola kwanza, tusiache mazalia, kisha turekebishe sera na uchumi wetu
 
Wanakijiji wa vijiji 4 huko bonde la Kiru, Babati, Mkoa wa Manyara wamechoma moto viwanda 2 vya sukari, mashamba na matrekta 20 mali za wawekezaji.

Source: Radio One Stereo Breaking News via cellphone.

Wakilipa Dowans au ikigundulika wamelipa Dowans itabidi tutumie hii strategy kwenye vitega uchumi vya wahusika wakuu vinavyojulikana i.e. Caspian etc. Kama Ngeleja ana kitega uchumi chochote kinachofahamika, etc. Kama unafanya kazi kwa hawa wezi wa DOWANS ukisikia wamelipwa inabidi uombe likizo ya muda maana nahisi hapatatosha.
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho![/QUOTE

Jibu la mwisho wasiposikilizwa ndio kuharibu mali na maisha. Labda ungeshauri wafanyeje maana wamejieleza hawakusikilizwa.
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!

Kuna wakati wanatu wanatoa sauti zao kwa nguvu kubwa lakini hazisikilizwi, kuna wakati watu wanawasilisha malalamiko yao wanazugwa tu. Ukifanyiwa ukatili kupita kiasi ukilalamika bila kusikilizwa , ni kawaida kwa watu kureact kwa namna hii. Hata Mbwa ukimpiga sana kuna wakati akishindwa kuvumilia atakugeukia na kuanza kujihami kwa kukurarua.

Si busara, si ubinadamu nakubali, lakini ujue kuwa ndio chaguo la mwisho. More will come mpaka watu watakapoeshimiwa.
 
Wanakijiji wa vijiji 4 huko bonde la Kiru, Babati, Mkoa wa Manyara wamechoma moto viwanda 2 vya sukari, mashamba na matrekta 20 mali za wawekezaji.

Source: Radio One Stereo Breaking News via cellphone.

Watu wamechoka.
 
Ingesaidia kama kuna mtu atatupa taarifa sahihi kutoka eneo la tukio ili tujue nini kilisababisha wananchi kujichukulia sheria mikononi. Ikiwezekana kama tutaweza kupata picha. Pia nini kinachoendelea hadi Leo tangu tukio Hilo kutokea.
 
at last, ndugu zangu wa babati wameamka! people's power...unstoppable!
ukiona hivi ujue wananchi wamechoka kuongea,serikali haishauriki wala kusikia vilio vya watu wake! Serikali ni ya wananchi ,kwa ajili ya wananchi na sio vinginevyo; lakini leo hii imekuwa serikali ya mafisadi kwa ajili ya mafisadi.
Serikali, watch out!! what comes next after this.....
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!

My friend... that's a natural phenomenon... You give what people want.. or they take it by force!!!! Watu wameshatumia njia zote kujieleza!... and yet our viongozi still don't give a damn!!!! Mimi sipendi mambo yaende hivyo... but that is the only option for now!!!! We need our rights!!!.. By any means... necessary!!! AMANDLAH!!
 
Main.jpg

Mwanza RC, Abbas Kandoro, in tight security from Field Force Unit yesterday when he toured the city`s central business district, which was marred by chaos after small scale traders known locally as Machingas refused to vacate the city`s areas.(PHOTO: ippmedia Correspondent)

Verdict:
Si bure sasa Regional Commissioner Abbas Kandoro ameamua kutembea kwa gari la 'deraya' la FFU , sasa viongozi gani wengine wa serikali ya CCM kote nchini nao watamuiga mwenzao huyu ili kujihakikishia usalama?? Mie nadhani wajiuzulu maana wameshindwa kuwaletea maisha bora watanzania hii picha inaonyesha wanatumia kila mbinu kubaki madarakani kwa nuguvu.
 
Wanakijiji wa vijiji 4 huko bonde la Kiru, Babati, Mkoa wa Manyara wamechoma moto viwanda 2 vya sukari, mashamba na matrekta 20 mali za wawekezaji.

Source: Radio One Stereo Breaking News via cellphone.

Hao sio wawekezaji ni ma-Mafia,mbona mnawapamba?The whole world economic system is Mafia .To me it's fine.
 
Hiyo ni sehemu ya demokrasia (popular demoracy).Ukisema sena bila kusikilizwa kinachofuata ni kulazimisha kusikilizwa.CCM hawasikii na wala hawaoni matatizo ya msingi ya wananchi kila kona ya nchi yetu.Sasa wasubiri popular democracy zaidi.Wataisoma mwaka huu
 
My friend... that's a natural phenomenon... You give what people want.. or they take it by force!!!! Watu wameshatumia njia zote kujieleza!... and yet our viongozi still don't give a damn!!!! Mimi sipendi mambo yaende hivyo... but that is the only option for now!!!! We need our rights!!!.. By any means... necessary!!! AMANDLAH!!

Naomba nikiri kwamba mimi sijaelewa tatizo ni nini. Tatizo pekee lililo wazi kwenye hii thread ni chuki ya kisasi. Ilifanikiwa sana Somalia na Ivory Coast. Tatizo la huko Kiru bado sijajua limesababishwa na nini. Bahati mbaya wengi hatuko interested kujua kwa sababu waliofanyiwa ni wahindi. Na hivyo sisi tunaona kwamba justification ya tendo baya iko kwa nani kafanya badala ya kuwa kwenye tendo lenyewe.
 
Back
Top Bottom