Kumekucha: Wanakijiji wachoma matrekta 20 ya wawekezaji Babati

Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!

mhh! Mbona unakuwa sura mbili weye! Kule misri ulikokuwa unashabikia walitumia mbinu gani yakhe! Au kwa kuwa presida wa hapa ni nnanihii....
 
Wananchi JF tujiunge kuorginise watu mitaani hasa Dar na kuunga mkono mikoa mingine. Wakati ndio huu wa kubadilisha serkali yetu. CCM hawana nguvu na wanaogopa watu mitaani, tunachotakiwa ni kuunganisha mikono pamoja na kuundamana kwa amani bila kuugopa, tukidai CCM waondoke serikalini.
 
hilo ndo suluhisho pekee la kufanya ili kufikisha ujumbe wetu kwa watawala ya kuwa tumechoka kuwa watumwa ndani ya nchi yetu
 
mhh! Mbona unakuwa sura mbili weye! Kule misri ulikokuwa unashabikia walitumia mbinu gani yakhe! Au kwa kuwa presida wa hapa ni nnanihii....

Hapana mama yangu, Misri ni maandamano ya amani. Walichoma jengo la chama tawala kama symbol ya kuukataa utawala wa chama hicho. Walichma magari ya polisi kama symbol ya kukataa polisi wasiwazuie. Lakini yote haya yalifanyika kwa dola siyo kwa raia kwa hiyo hakuna mtu atakuja kulipa kisasi. Lakini hilo la Babati ni tofauti kabisa. Hadi sasa hakuna raia amepigwa na raia mwenzake huko Misri. Ikitokea nitaikemea kwa sababu ni hatari itapelekea visasi, mauaji ya kimbari.
 
Mzee Jomo Kenyatta: Mwalimu, watu wako wamelala.

Julius K. Nyerere: Mzee, ni kweli. Lakini wakiamka siwawezi.
 
Bado wakulima wa chai kule Lupembe wakianza sijui uo motto utazimwa na nani
 
Wanakijiji wa vijiji 4 huko bonde la Kiru, Babati, Mkoa wa Manyara wamechoma moto viwanda 2 vya sukari, mashamba na matrekta 20 mali za wawekezaji.

Source: Radio One Stereo Breaking News via cellphone.

bila shaka wameshakuwa-inspired na kinachoendelea Egypt
 
Hapana mama yangu, Misri ni maandamano ya amani. Walichoma jengo la chama tawala kama symbol ya kuukataa utawala wa chama hicho. Walichma magari ya polisi kama symbol ya kukataa polisi wasiwazuie. Lakini yote haya yalifanyika kwa dola siyo kwa raia kwa hiyo hakuna mtu atakuja kulipa kisasi. Lakini hilo la Babati ni tofauti kabisa. Hadi sasa hakuna raia amepigwa na raia mwenzake huko Misri. Ikitokea nitaikemea kwa sababu ni hatari itapelekea visasi, mauaji ya kimbari.

Basi upo nyuma ya wakati. Hadi sasa kwa mujibu kituo cha Aljazeera, watu 100 tayari wameuawa na maiti zinaonyeshwa waziwazi.

Haya sasa kemea kama ulivyoahidi.
 
Basi upo nyuma ya wakati. Hadi sasa kwa mujibu kituo cha Aljazeera, watu 100 tayari wameuawa na maiti zinaonyeshwa waziwazi.

Haya sasa kemea kama ulivyoahidi.

Mkuu wangu, kweli niko nyuma, si unajua tena ungeleja haukuwepo kwetu Leo?
Hata hivyo, hao 100 wameuawa na polisi au raia? Kama ni raia, kwa kukanyagana au kukusudia? Mimi niliona Jana usiku polisi wanapiga risasi za moto, waandamanaji wakiteka polisi hawamlipizi kisasi bali wanamlinda. Magari yote yaliyochomwa waliwatoa polisi kwanza ndipo wakachoma. Zaidi mkuu, wanahitaji kupongezwa, kwani maandamano makubwa vile nchi nzima waliokufa 100 tu?
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!

Vita ni vita mura! ya Tunisia nearer to Bongolala land
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!

Vita ni vita mura! ya Tunisia na Egypt nearer to Bongolala land.Manzese,Migo na Ubungo changamkeni.Chomeni hizo IPTL,RICHMUND,AGGREKO na DOWANS Power Plants acha kulala mpaka kieleweke.
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.
Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!

Mkuu Gurudumu una maana,

Mandela na wenzi wake walifanya makosa,
Samora vile vile alikuwa mpuuzi kupigana na mreno,
Mujoma si angetulia tu mpaka kaburu amwonee huruma?
Akina Kimathi walikuwa wachokozi ndiyo maana wakanyongwa...
Pengine na Tunisia wameshinikizwa na wachochezi........?

Inatakiwa binadamu afikishwe wapi ndipo iwe basi?

Naomba kuelimishwa,
 
Mkuu, sasa naamini kwamba uwezo wangu wa kujieleza ni mdogo sana. Mkuu, ninamaanisha hivi;

1. Tuupige vita utawala tusipigane wananchi kwa wananchi. A. Kusini kulikuwepo weusi wanaofaidi ubaguzi, hawakuuwawa. Walifocus kwenye dola tu. Ukumbuke pia hawakupigana na kila mtu mweupe, Hapa nimesikia watu wanasema watavamia wahindi wote upanga na kuwanyanganya nyumba. Tukimaliza hilo, wangoni wagundue kuna umeme kilimanjaro hadi vijijini. Waende moshi kuvunja mfumo wote wa umeme. Hilo likiisha Wagogo wanaoidhi nyumba za tembe wakaunguze moto makazi ya wenzao kule Dodoma Mjini, pengine hata wateketeze jengo la bunge! Etc.

2. Kwenye maandamano ya Tunisia na Misri hayakuwa against persons bali against dola. Lakini inajulikana dunia nzima kwamba wananchi wanapokaidi amri ya polisi kwa amani na polisi wakapewa mamlaka ya kutumia Silaha za moto, lazima kutatokea maafa kidogo. Hii huitwa collateral damage. Hii hata iliidhinishwa na Obama jana alipomwambia Mubarak atumie minimal force! How much force is minimal?

3. Kule Tunisia na Misri kuna watu wanaotofautiana kama Hapa kwetu. Tofauti ya kipato, mafisadi, waliodhulumu raia, wageni kumiliki mali n.k. Lakini waandamanaji hawakuwashambulia hawa. Kama wananchi wangepigana wao kwa wao basi Ben Ali angekuwa madarakani hadi leo. Polisi wangepelekwa siyo kuzima maandamano bali kuua wezi na wavamizi. Hutapata sauti ya kudai serkali itoke madarakani kwa sababu wewe ni mwizi au muujumu uchumi.

4. Lakini kuna wakati serikali ikishagundua nia yenu na inataka kuepuka kutoka madarakani, inatumia mkakati huo ili kuwagawa na pia kubadili aina ya mabadiliko mliyokuwa mnadai. Inakoleza chuki miongoni mwenu mnaanza mapambano wenyewe. Mfano ni Zimbabwe. Mugabe alichoche chuki miongoni mwa weupe wenye ardhi na weusi wasio na ardhi. Ghafula akapata kundi kubwa linalomuunga mkono lililomeguka kutoka upinzani. Kisha kundi hilo likawa linawashambulia wapinzani. Hii hali haikuwepo Tunisia wala Misri. Na tunaambiwa hakuna chama chochote cha siasa kilicho anzisha wala kuratibu yale maandamano.

5. Kwa hiyo kwangu mimi, kupora na kuharibu mali za wanaotunyonya na kutunyanyasa, kuua na kujeruhi raia tunaowachukia, vitatufanya tuwekwe kwenye kundi la wahalifu na siyo watetezi wa haki. Tunapolipiza kisasi kwa waliotutesa, na sisi tunakuwa watesaji. Huwa wanasema dai haki kwa kutumia mikono misafi. Tukishapata ukombozi tunaoutaka swala la kurudisha mali zetu ni la kisera, siyo mabavu na kumwaga damu. Call it redistribution policies.

6. Onyo: ili utawala mpya uweze kutekeleza redistribution policies, ni lazima kung'oa mazagazaga yote ya utawala uliopita. Kama walivyofanya Tunisia, ni kama nchi imezaliwa upya. Tukifanya kosa kama la A. Kusini, tutakuwa tumepoteza muda wetu bure. Wanasiasa na watendaji wengi waliokuwa katika serikali ya kibaguzu waliendelea kwenye serikali mpya. Leo hii wananchi hawajapata walichopigani kwa miaka mingi. Bado ardhi inamilikiwa na wazungu, bado weusi wanapata huduma duni za jamii kuliko weupe, bado ubaguzi wa rangi umejikita, bado uchumi uko mikononi mwa weupe. Mandela aligundua amechemsha, kama Nyerere, akang'atuka na kumtoa Mbeki sadaka. Mbeki akashindwa wananchi wakadhani ni yeye hataki wakamweka Mbeki na Mbeki pia ameshindwa. Tatizo siyo rais bali apatheid mamboleo iliyo iliyojiimarisha kisayansi zaidi kwenye serikali ya weusi kuliko ilivyokuwa kimabavu kwenye serikali ya makaburu.

Kwa hiyo ndugu zangu tupigane kuing'oa dola kwanza, tusiache mazalia, kisha turekebishe sera na uchumi wetu
 
:A S thumbs_down:

Back
Top Bottom