Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,066
- 4,085
Serikali itumie eneo la wazi chuo kikuu UDSM kujenga stand, isitake ugomvi na walala hoi
Moja ya upangaji wa mji, ni kuwepo kwa huduma za jamii. Stendi ya kutosha ni moja ya huduma muhimu za jamii. Ni kwa bahati mbaya kuwa miji mingi yetu (Tanzania) ilitangulia kabla ya Afisa mipango miji. Hivyo katika kupanga, watu lazima wahamishwe, na hii inapo kugusa, lazima uumie, na kulalamika ni lazima. Wakati mwingine, ili kukwepa lawama, serikali huhamisha miji, na ndiyo maana unasikia miji kama "Old ....." Kwa kuwa Dar haiwezi kuhamishwa, basi lazima serikali ukubali lawama hizo. Najua inauma sana, lakini haina dawa.Huwezi kupanga mji kwa kuondoa wakazi ambao mji wao umepangika vizuri kama Ubungo. Lengo lao ni kupanua Stand ya Mkoa ili kupata maslahi kwa matumbo yao kama ilivyo sasa bila kujali hasara na usumbufu kwa wakazi.
happiness win mawazo yako yanaweza kuwa mazuri ila unayasema sehemu ambayo tunaosoma sio tunaopanga mipango ya maendeleo; unaweza kuwasilisha mawazo yako kwa baadhi ya madiwani unaofahamu au wewe mwenyewe kagombee udiwani ili ukatetee kile unachokiamini
Moja ya upangaji wa mji, ni kuwepo kwa huduma za jamii. Stendi ya kutosha ni moja ya huduma muhimu za jamii. Ni kwa bahati mbaya kuwa miji mingi yetu (Tanzania) ilitangulia kabla ya Afisa mipango miji. Hivyo katika kupanga, watu lazima wahamishwe, na hii inapo kugusa, lazima uumie, na kulalamika ni lazima. Wakati mwingine, ili kukwepa lawama, serikali huhamisha miji, na ndiyo maana unasikia miji kama "Old ....." Kwa kuwa Dar haiwezi kuhamishwa, basi lazima serikali ukubali lawama hizo. Najua inauma sana, lakini haina dawa.
Wajenge stand ya juu mpya...
Fly over stand!!!!!!!!
huo ni mpango wa kuwahamisha wapiga kura wa Mnyika wakikubari tu wanahamishwa kabla hata ya 2015
mimi huwa sielewi wanaopanga mambo ya maendeleo huwa ni wasomi au walevi?
Miradi ya wakubwa hii.
Unafikiri utabadili mipango ya serikali kwa kujadili hapa jf
Upanuzi utakuwa nyuma ya stand ila kibadado itamegwa kidogo kwa pembeni kwa lengo la kunyoosha vizuri hiyo stand yao.
Wewe upo jikoni nini maana unaeleza kama vile unafahamu mpango mzima! Nakumbuka mkuu wa mkoa Sadick this year alisema stand itahamishwa ubungo kupisha mabasi ya mwendo kasi hapo ebu tueleze kuhusu hili Hapiness.
Hapo kuna wenye maslahi yao hasa wenye magorofa Unungo, Sinza na Manzese watakua wamefanya fitina ili wasipate hasara stand ikihamishwa maana wamewekeza kwa pesa nyigi mahoteli yao !
...halafu baba mwenye nyumba huuuyoooo nje anaenda msibani nyie mvuruane hukuuuu mpaka basi.Hizo ni dalili za mawazo finyu kwani bado tuna sehemu zenye nafasi kubwa kwa ajili ya kujenga stand kama madau mmoja alivyo pendekeza KILUVYA.Huku ni kutafuta uraji tu.Kwa kumbukumbu zangu eneo hilo la UBT ni mali ya UDA labda kama umiliki wake ulibadilishwa.Nchi hii kila siku jambo jipya la maudhi,dah yaani kichwa kinauma sana!