Kumekucha: "Msiba wa Taifa" Toleo la 4..

kinachosikitisha zaidi ni kuwa kamwe hatujifunzi chochote kutokana na majanga tunayopata. insurance companies nazo haziwezi kubana wateja wao kwa sababu wao hawawajibiki hata siku moja! hapo hawatalipwa zaidi ya ubani wa ubwabwa na maisha yataendelea hadi janga lingine lije! kama insurance zingelazimika kulipa billions kwama fidia,utaratibu ungekuwepo na ungefuatwa! hii ni 3rd world,banda la uani!
mkjj,thanks for doing ur part
 
Ni kawaida yetu wakuu,hapo tutapeana salamu za rambirambi,tutapeana pole,tutajenga na minara ya kumbukumbu,tutafanya uchunguzi usiokuwa na tija nk,nasima uchunguzi usiokuwa na tija kwa maana kwamba hii si ajali ya kwanza...kwa mwezi huu tu Tanzania inaweza kuwa imepoteza watu wasiopungua 1000 kwa ajali...tena hizi ni zile ambazo tunapata taarifa zake.....kama kawaida viongozi wetu wanatoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na kuwapa pole majeruhi...Najiuliza maswali mengi sana na sipati majibu exactly what happens in Tanzania currently...ni kama kuna laana inakula taifa hili na sisi hatuna habari.....Baada ya kuzama meli ya MV Bukoba serikali ilisema itafanya campaingn safisha usafiri wa majini...ni kweli kwa kipindi cha miezi michache meli na boti kadhaa zilifungiwa kufanya biashara...lakini kama kawaida ya Watanzania baada ya kusahau yale machungu tukarudi kulekule...boti na meli zimechoka,zina kutu na zinabeba watu zaidi ya uwezo wake ambacho ndio inasemekana ni chanzo cha hii ajali ya Zenji...Unaweza kuwalaumu wasafiri kwamba kwanini walikubali kupanda meli ambayo tayari ina mzigo mkubwa..jibu ni wazi NI UMASKINI WA WATANZANIA usafiri wa taabu,ukikosa meli moja unatakiwa usubiri siku mbili au tatu,kwanini watu wasijazane?

MAONI YANGU:
Serikali iiache siasa kwenye uhai wa watanzania,SUMATRA kazi yao ni kukusanya faini tu za watu bila kutimiza wajibu wao..vyanzo vya ajali za barabarani na majini mara nyingi ni mwendo kasi,ubovu wa hivyo vyombo,kubeba mizigo kupita kawaida...........serikali tuchukue hatua,tume zinaundwa na sitashangaa kama hii ajali tume ikiundwa,lakini JE? Tunafanyia kazi maoni ya hizo tume? TUACHE SIASA KWENYE UHAI WA WATANZANIA JAMANI...!!!!

Natoa pongezi nyingi kwa ndugu M/Kijiji kwa kijarida hicho kwa kutupa taarifa za kina zaidi kuliko chanzo kingine chochote hadi wakati huu. Nazidi kutoa pole nyingi kwa ndugu zetu wa Unguja, na Pemba na hata huku Bara kwa kupotelewa na ndugu, jamaa, marafiki, majirani nk. Ni msiba mkubwa na ni wetu sote kama wa-Tz.

Ndugu Only83, umezungumzia SUMATRA katika ajali hii iliyotokea huko Zanzibar, mimi sidhani kama SUMATRA inahusika na usalama wa vyombo vya usafiri huko Zanzibar. Nakumbuka wakati wa mchakato wa kuanzishwa kwa SUMATRA, wa-Zanzibar walicharuka na kupinga kiasi cha kufikia kuwatukana maofisa wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi waliokwenda Zanzibar kujadili wazo hiloi. Baadhi ya viongozi wa Zanzibar wa wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi walidai hawawezi kuburuzwa na Bara katika swala hilo, hivyo waliamua kuanzisha agency yao kama niko sahihi.

Ni kweli kuwa kuna tatizo la siasa katika maswala yanayogusa usalama wa maisha ya watu kama hayo. Na pia hili swala la Muungano bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu, lakini kwasasa siyo wakati mwafaka kulizungumzia sana.

Mwisho nakubaliana na wewe 100 pc kuwa tuache siasa katika maswala ya kitaalamu na yanayohusu maisha na usalama wa maisha ya watu wa Tanzania.
 
niwakati wakuangalia na maeneo mengine sasa!
LAKINI SISIS MATAAHILA TUJIFUNZE MALA NGAPI!
AU NDO HAYA MELI MPAKA IUE NDO TUSIIITUMIE!
 
Ni kawaida yetu wakuu,hapo tutapeana salamu za rambirambi,tutapeana pole,tutajenga na minara ya kumbukumbu,tutafanya uchunguzi usiokuwa na tija nk,nasima uchunguzi usiokuwa na tija kwa maana kwamba hii si ajali ya kwanza...kwa mwezi huu tu Tanzania inaweza kuwa imepoteza watu wasiopungua 1000 kwa ajali...tena hizi ni zile ambazo tunapata taarifa zake.....kama kawaida viongozi wetu wanatoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na kuwapa pole majeruhi...Najiuliza maswali mengi sana na sipati majibu exactly what happens in Tanzania currently...ni kama kuna laana inakula taifa hili na sisi hatuna habari.....Baada ya kuzama meli ya MV Bukoba serikali ilisema itafanya campaingn safisha usafiri wa majini...ni kweli kwa kipindi cha miezi michache meli na boti kadhaa zilifungiwa kufanya biashara...lakini kama kawaida ya Watanzania baada ya kusahau yale machungu tukarudi kulekule...boti na meli zimechoka,zina kutu na zinabeba watu zaidi ya uwezo wake ambacho ndio inasemekana ni chanzo cha hii ajali ya Zenji...Unaweza kuwalaumu wasafiri kwamba kwanini walikubali kupanda meli ambayo tayari ina mzigo mkubwa..jibu ni wazi NI UMASKINI WA WATANZANIA usafiri wa taabu,ukikosa meli moja unatakiwa usubiri siku mbili au tatu,kwanini watu wasijazane?

MAONI YANGU:
Serikali iiache siasa kwenye uhai wa watanzania,SUMATRA kazi yao ni kukusanya faini tu za watu bila kutimiza wajibu wao..vyanzo vya ajali za barabarani na majini mara nyingi ni mwendo kasi,ubovu wa hivyo vyombo,kubeba mizigo kupita kawaida...........serikali tuchukue hatua,tume zinaundwa na sitashangaa kama hii ajali tume ikiundwa,lakini JE? Tunafanyia kazi maoni ya hizo tume? TUACHE SIASA KWENYE UHAI WA WATANZANIA JAMANI...!!!!

Naungana na maoni yako mkuu, Ni muda wa kuweka ahadi uchwara pembeni na kufanya kazi kuhudumia wananchi, kumbukeni ni miaka 50 ya uhuru na ni tukio jingine kubwa baada ya MV. Bukoba ni miaka 15 sasa imetimia gafla Janga jingine hili hapa la Mv.Spice jamani lini serikali itajifunza kutokana na makosa yake, me nilipo zipata hizo taarifa nilitokwa na machozi zikarudi hisi za Mv.Bukoba kwani that time i was in Mwanza mchana wa siku ile mjili ulikubwa na kimya cha ajabu na majonzi vilio huku na kule wakatokae eti hawa wataalamu wetu sijui hawakusoma physics wakaenda toboa Meli nahuku walikanywa wasitoboe na mmlikiwa zile Ferry za kamanga na akawaambia wafanye utaratibu meli kuivuta mpaka pwani ya bwiru serikali ikagoma wao wakashinikiza kutoboa kutoa watu na wakafanikiwa kumtoa mtu mmoja na meli ikaaanza kuzama.

Tokea kipindi hicho serikali haija nunua meli nyingine japo kuwapa moyo wananchi wajue serikali yao na zile kodi walizo kuwa wakilipa zime wezesha japo kufuta baadhi ya muachungu ya Mv Bukoba

My Take;

TUACHANE NA SI HA SA a.k.a GUTTER POLITICS
 
as we mourn our own,kenya loses more than 100 people in a petrol pipeline explosion...
 
niwakati wakuangalia na maeneo mengine sasa!
LAKINI SISIS MATAAHILA TUJIFUNZE MALA NGAPI!
AU NDO HAYA MELI MPAKA IUE NDO TUSIIITUMIE!

Serikali yetu tokea baba wa Taifa alipo ondoka basi tena kila kitu kikifa ndio mazima hakifanyiwi mchakato wa kuja kipya angalieni viwanda navyo ni janga pia watu kukosa ajira ni janga jingine na lina zua janga jingine. serikali yetu yenyewe ati inajua kukaka maeneo na kuya kuza na kuyaita mikoa huku mikoa iliyopo ni taabu kweli kutimizia wananchi sijui ni proactive gani wao wana implement ni yakujichukilia chao mapema na kutuacha karagabao sie watanzania kufia na umaskini alafu inakuja kauli ati jiuleze "Utaifanyia nini nchi yako na sio nchi yako itakufanyia nini" Khaaa kama viongozi tulio nao kila kukicha hawatekelezi majukumu yao na ukiwakosoa tu unakuwa wewe ni mpizani husie penda maendeleo sasa pia ukiandamana au ukikosoa serikali we ni adui wa serikali this is outrageous.

My Take;
Tuwe na mjadara wa kitaifa tuhoji serikali yetu na timu yake ya majanga wao kazi zao ni zipi waliuweka mfumo wa kile kikosi cha Majanga vipi katika kukabiliana na hali kama iliyotokea Pemba,

Tuanitaji kuiambia serikali maoni yetu na sio ituamulia wajisikiavyo sisi ndio tumewapa dhamana ya kuwa hapo, iweje wa leo waamua kuigawa Tanzania kwa kuiongezea mikoa na wilaya huku tu mikoa na wilaya zilizopo hazijawesha kupata huduma ipasavyo kumbukeni ni zile zile wilaya bali hani majina na mipaka inatengenezwa upya tuu ila huduma duni ndio zitazidi ongezeka kama wameshindwa kwa ilivyokuwa mwanzo iweje wewezi kufikisha huduma kwa kusema wemeongeza mikoa. it doesnt make sense at all kwa mtu mweye upeo wa kuona mbali.
 
Jamani jamani kuna ki2 kimenikera leo ni baada y kuona kwenye taarifa y habari y asubuh ITV appointed president kikwete alivyokwenda kuwaona wahanga walofariki ktk ajali y boti huku akiwa na uso w furaha(kucheka cheka km kawaida yake)badala y kuonyesha uso w huzuni. ninadought anahucka.
 
Hizi hela wanazozimwaga wangeingiza kwenye elimu nadhani Tz ingekuwa mbali kielimu. Mwaga kwenye bodi ya mikopo, taasisi za elimu, researches nk. Sera mbovu ndo zinaleta haya
 
JAMANI TUWE MAKINI NA SERIOUS TUNAVYOJADILI MAMBO MUHIMU YA NCHI NA USALAMA WETU, NI JUZI KWENYE GAZETI moja WALITOA TAKWIMU YA AJALI ZA PIKIPIKI KWA KIPINDI CHA KUANZIA JANUARY 2011 HADI JULY 2011, Walikuwa wanatoa takwimu ya miezi sita, cha kushangaza Walitoa takwimu kuwa ajali za pikipiki kwa Jiji la Dar kwa kipindi Hicho zimegharimu Maisha ya watu 396 Miezi sita!! Pia walitoa takwimu kwa mkoa wa kilimanjaro na kusema kwa kipindi hicho hicho ajali za pikipiki zimegharimu Maisha ya watu 32, Sijajua kwa mikoa mingine!! Kweli kwa karne hii ya 21, miaka 50 ya uhuru, Hizi ajali zote hizi tutaendelea kusema ni mpango wa Mungu? Tuseme kila mkoa walikufa hao 32, tukiondoa dar es salaam, ina maana kwa mikoa yote 25 wametutoka ndugu zetu 32 x 25 = 800 + 396 (Wa Dar) Jumla 1196, Je kuna tafiti zozote za kitaalamu za kutibitisha hawa watu wamefikia muda wao wa kufa? JAMANI SUMATRA TUONEENI HURUMA, MAISHA YA BINADAMU SIO YA MAJARIBIO KUHIVYO, DO SOMETHING KUPUNGUZA HIVI VILIO, SASA MNALIPWA KWA MSAADA UPI MNAOIFANYIA JAMII? KILA UPANDE MMESHINDWA!!!
 
Mimi sidhani kama hawa watu hawajali kwani Watanzania hatupo hivyo!! lakini habari za misiba na ukubwa zimekuwa za kusuasua na ni vigumu kwani Msiba umetokea siku hiyohiyo!. Badala ya kukimbilia ku judge hawa watu ni lazima tujiulize kama TV za serikali zilitangaza muda gani hizi habari na kama huo muda na uhakiki ulitosha kwa wao kukatisha shughuli. Watu hawawezi kufanya uamuzi kwa kupitia blogs pekee ni lazima TV na radio za serikali zitangaze janga na ajali kubwa za taifa kwa muda muafaka. Vilevile tujiulize jeshi na polisi walikuwa wapi? mimi ningejali zaidi hili kuliko watu binafsi wanaofanya shughuli binafsi siku hiyo hiyo ya msiba!!
 
Jamani jamani kuna ki2 kimenikera leo ni baada y kuona kwenye taarifa y habari y asubuh ITV appointed president kikwete alivyokwenda kuwaona wahanga walofariki ktk ajali y boti huku akiwa na uso w furaha(kucheka cheka km kawaida yake)badala y kuonyesha uso w huzuni. ninadought anahucka.

Yeah it was bad!!! Mwili wangu ulipata baridi nilipomuona rais wangu anachekacheka na shati lake la mauamaua kwenye msiba wa kitaifa! Viongozi wenzie wamevaa black yeye na shati la maua maua kama anakwenda disco uwiiiii!
 
Swali la msingi ni kuwa mnafikiri kweli tumejifunza? Leo hii ziwa Tanganyika meli ya Mv. Lihemba bado iko katika huduma; Lake Victoria Mv. Victoria nayo iko katika huduma. Kwa taifa ambalo limezungukwa na maji mengi na watu wake wanategemea usafiri wa majini ni jambo la kushangaza kuwa hatuna mfumo mzuri wa usafiri wa majini. Ndio matokeo ya pande mbili za kitu kile kile - ufisadi na ubepari.
 
Hongera Mwanakijiji kwa ufanisi wako, ila hili taiafa linatuumiza sana sisi choka mbaya na tusubiri tume bubu itakayoundwa kwani hii nchi ishakuwa ya tume na kufanya .........., nashindwa hata kumalizia
 
Inasikitisha sana nikikumbuka ilivyokuwa kwenye MV Bukoba mwaka 1996 ni tofauti kabisa na Mv Spice ya 2011 sijafahamu mpaka sasa wale wa MV Bukoba walikuwa ni binaadamu na hawa wa Mv Spice walikuwa ni wanyama!

Tofauti ya 1996 na 2011 ni Ben na Jakaya!! Uwezo wa kuhendle issues uko tofauti. Hii kitu kama JK hatakifanyia kazi naona dalili za mpasuko kuongezeka. Hivi mpaka sasa ameshasema kitu................. au amendelea na ile safari yake ya USA kusaka ujiko???
 
<font size="4"><font color="#FF0000">CCM Kampeni zake kutafuta ukubwa Igunga, VODACOM kuendekeza hela zaidi na Miss Tanzania kuvutiwa zaidi na kuanika mapaja hata kwa siku za msiba mzito kama huu nchini mwetu wananchi tunasema vitendo vyenu kamwe HAVIKUBALIKI hata kidogo!!!!!!!!!!!</font></font>
<br />
<br />
sikuona mapaja siku ile. Usiwe default minded
 
Leo nimesikia eti wapiga mbizi kutoka afrika ya kusini wanaelekea kwenye eneo la tukio kuona kama bado kuna watu ndani ya meli! Hivi kweli Tanzania hatuna jeshi la majini? Yaani miaka 15 iliyopita tuliomba wapiga mbizi wa africa ya kusini mv bukoba ilipozama na leo hii tena tunafanya kilekile?
hivi yule mpiga mbizi tuliokuwa tunamuona sabasaba enzi zile tuko watoto bado yupo?
 
Sijaelewa tume imeundwa ya nini?
Tume iliyoundwa ni ya kutuliza hasira na haina uhusiano wowote wa kiufundi au kitaaluma. Huu ndio mwendo wa serikali yetu kufanyia kazi matukio na si kubuni mbinu za kukabiliana na matukio.

Naseama ni tume isiyo na uhusiano na tukio kwasababu tayari tunaambiwa mmiliki alikuwa hajulikani, na mara tunasikia kepteni wa meli hakuwa nwenyewe bali dei waka. Ni kutokana na mambo kuwa ya kificho ndio maana hata vyombo vya taifa vilizuiwa kutoa taarifa kwani serikali JMT na SMZ zilijua ni bomu.

Hakuna sababu ya tume! tuna polisi, SUMATRA, bandari Dar na Unguja, tuna waongoza meli. Hawa wote wana majibu ya tukio.
1.Meli imesajiliwa wapi na nani. (2)Meli ina ukubwa gani na uwezo gani kuchukua abiria na mizigo(3) Abiria wangapi walipakia Dar(4)mizigo kiasi gani ilipakiwa Dar(4)Ikiondoka dar captain alikuwa ni nani (5) Ilipoondoka dar hali ya usalama ilikuwaje(6)ilipofika Unguja iliongeza abiria kiasi gani na mizigo kiasi gani(7) nani wakala wa tiketi Dar na Unguja na makusanyo hayo yalikuwa yanalipiwa kodi kwa utaratibu gani.(8) Nani aliondoa meli Zbar
(9) Nani alikuwa na wajibu wa kuangalia idadi ya abiria na mizigo (10) Chombo kilifanyiwa service lini na nani kwa mara ya mwisho
(11).......n.k n.k

Kuunda tume maana yake kuwa na muda wa kulindana si kutafuta ufumbuzi, kama ni ufumbuzi uzembe huu kama ule wa MV Bukoba ungeshapatiwa dawa na usingejirudia. Kila mara huwa nasema tume maana yake ,To buy the time , to quel the anger and protect the interest
 
Swali la msingi ni kuwa mnafikiri kweli tumejifunza? Leo hii ziwa Tanganyika meli ya Mv. Lihemba bado iko katika huduma; Lake Victoria Mv. Victoria nayo iko katika huduma. Kwa taifa ambalo limezungukwa na maji mengi na watu wake wanategemea usafiri wa majini ni jambo la kushangaza kuwa hatuna mfumo mzuri wa usafiri wa majini. Ndio matokeo ya pande mbili za kitu kile kile - ufisadi na ubepari.
Mkuu wangu kusema kweli meli zote hizo zinatakiwa kuwa grounded.. Tunatakiwa kutoipanda kabisa, lakini utaweza vipi kuwashawishi wananchi ambao wamezoea kupanda mitumbwi na ngalawa wakuelewe vizuri?
 
Back
Top Bottom