Kumekucha! Magurudumu yaanza kung'oka kwenye gari la JK

Pengine mie ndio most pessimistic: Magurudumu hayakuwepo in the first place,kwahiyo kinachokongoroka sasa ni mahala palipostahili kuwekwa magurudumu hayo.

Kikwete ana dhambi nyingi alizochuma kati ya 1995-2005 wakati alipokabidhi utu wake kwa viumbe hatari kabisa waliokuja kufahamika baadaye kama wanamtandao.Hawa ni mithili ya mafioso,na wameacha makovu makubwa katika maisha ya wengi.

Sasa ukichanganya na hii ya kuua raia wasio na hatia huko Arusha,ni dhahiri huyu Mkwere analazimisha hasira za Muumba.Sintoshangaa siku mwanae,Ridhiwani nae akajitokeza kumpiga baba yake hadharani au Salma kuomba talaka (I know it's wishful thinking but anything goes)....
 
Kikwete hawezi kukosa usingizi, inawezekan kwa sasa amekuwa Kama Machael Jackson anatumia vidonge vya usingizi na anaota kwenye kisiwa cha Amani.
 
Roho mtakatifu amshukie baba kikwete.
Msamehe yale yote anayoyafanya na umwoneshe njia nzuri katika kipindi chake cha uongozi. Amen!
If you believe in god(s) please pray for him. Tushamblame sana
It's enough.
 
Hii post ni ukweli ila kwa suala la kusema magurudumu ni kwamba gari la Kikwete halijawahi kuwa na magurudumu, na sababu ni kwamba hili gari linaweza kuvutwa kwa ubavuni,mbele ,nyuma, kichwa chini miguu juu kwa wakati wowote ule n.k.
-Kinacho msaidia kiwete na ccm kwa ujumla ni sera mpya ya (udini na ukabila)
 
Sawa: akihamia uarabuni na familia yake ndio vizuri tunachukua nyumba na vitega uchumi vyote alivyokua anamiliki vinakua mali ya umma. Infact hatumuhitaji yeye kama yeye(maana afya yenyewe ina mgogoro) tunahitaji mali alizoibia watanzania tuzitumie kwa manufaa ya umma.

Familia ishaandaliwa makazi maalum katika nchi moja ya Ki-Arabu. Prof Mutharika kusaidia kufaulisha uondokaji wake. Ndio maana katembelewa mara mbili ndani ya wiki mbili hapo nyuma kidogo.

Makamu wa rais na mtaalam wa NUCLEAR naye kwa sasa yuko kwenye kukamilisha kazi nyeti mno huko mbugani Serengeti. Sio matairi tu kunyofoka bali na sentabolti nayo iko pabaya kupita kiasi.
 
Ni vizuri anavyokaa kimya kwasasa. tunamwomba aje na matamko na majibu ya maana kwa maslai ya nchi na wananchi.
 
Ninavyofahamu mimi, gazeti la kila wiki la Changamoto linamilikiwa na shushushu mmoja wa ngazi ya juu mstaafu (jina nafunika kwanza kwa sababu hawa huwa hawastaafu) hivyo habri zinazoandikwa humo kuhusu ya ndani ya serikali ya JK huwa yana ukweli kwa takriban asilimia 100.

Isitoshe gazeti hili lilikuwa ni anti-upinzani katika kipindi cha kampeni mwaka jana.

Leo hii katika stori yake kubwa ‘Maswahiba wamuasi Rais Kikwete’ linaeleza jinsi rafiki zake wa karibu wanavyomuasi, hali ambayo itamuweka pagumu katika kipindi chake cha pili cha utawala ambacho ndiyo amekianza tu.

Pamoja na mambo mengine, gazeti limesema kwamba hata katika vurugu za Arusha, kuna mkono wa baadhi ya maswahiba hao wa JK.

Swali: Hii si ndiyo dalili inayoonyesha kwamba magurudumu yaanza kunyofoka katika gari la JK?
Kaka HII HABARI YAKO IMENIFANYA NICHEKE SANA MAANA NIMEKUMBUKA ENZI ZA UJANA WANGU NILIJARIBU KUENDESHA BAISKELI UMBALI WA KILOMITA ZIPATAZO MIA MBILI. NILICHOKA SANA HADI NIKAAMUA KUIBEBA BAISKELI BEGANI. WAKATI HUO NILIONA NI RAHISI NA NYEPESI KULIKO KUIENDESHA. Kwa ukweli huu Kikwete na CCM yake anaona Kuibeba Tanzania Begani Badala ya Tanzania Kumbeba yeye ndio jambo rahisi! Je kuna Mtu wa kumkumbusha kwamba hana uwezo wa kuibeba Tanzania badala yake anatakiwa kubebwa na Tanzania ili kuongeza uzalishaji? wanaotakiwa kumkumbusha ndio hao akina Chatanda; Makamba; Ngereja na Rostam!!!!!!!!!!
 
-Katiba inamkosesha usingizi,

-Mauaji aliyofanya Arusha yanamtesa,

-Vyuo vikuu ndio kwanza vimepamba moto,

-Mafisadi wanamshinikiza afumbe mdomo,

-Balali ndio huyo imejulikana wazi kuwa yuko hai,

-Mawaziri wake wanahoji kauli zake na kupishana kimitizamo,

-ahadi zake zinazokaribia thamani ya bil.100 hazitekelezeki,

-Nchi ipo gizani, uzalishaji viwandani unashuka,

-Inflation inazidi kila kukicha,

-Kauli za maaskofu zinamnyima hata kusogelea hafla zao, tumbo moto!

Total confusion...ni wa kumhurumia!...Akina Rizwani na Salma walimsukumiza
kwenye madaraka na kumsaidia kuchakachua, sasa hivi wamemwacha achanganye na zake!

Pole weee!...

Mkuu bado kuna moshi mkubwa unafukuta, Wakulima waliahidiwa pembejeo lakini mpaka sasa hivi hakuna wakala aliyekwisha kulipwa, sababu kubwa ni kwamba pesa haijaingia benki, kwa maana nyingine ni Seriksli imefilisika. Huyu bro JK ni bora ang'atuke kabla ya aibu kubwa. YAANI NCHI IMEMSHIDA TATALY
 
-Katiba inamkosesha usingizi,

-Mauaji aliyofanya Arusha yanamtesa,

-Vyuo vikuu ndio kwanza vimepamba moto,

-Mafisadi wanamshinikiza afumbe mdomo,

-Balali ndio huyo imejulikana wazi kuwa yuko hai,

-Mawaziri wake wanahoji kauli zake na kupishana kimitizamo,

-ahadi zake zinazokaribia thamani ya bil.100 hazitekelezeki,

-Nchi ipo gizani, uzalishaji viwandani unashuka,

-Inflation inazidi kila kukicha,

-Kauli za maaskofu zinamnyima hata kusogelea hafla zao, tumbo moto!

Total confusion...ni wa kumhurumia!...Akina Rizwani na Salma walimsukumiza
kwenye madaraka na kumsaidia kuchakachua, sasa hivi wamemwacha achanganye na zake!

Pole weee!...

balali yuko hai?????????????? tupe data
 
Pengine mie ndio most pessimistic: Magurudumu hayakuwepo in the first place,kwahiyo kinachokongoroka sasa ni mahala palipostahili kuwekwa magurudumu hayo.

Kikwete ana dhambi nyingi alizochuma kati ya 1995-2005 wakati alipokabidhi utu wake kwa viumbe hatari kabisa waliokuja kufahamika baadaye kama wanamtandao.Hawa ni mithili ya mafioso,na wameacha makovu makubwa katika maisha ya wengi.

Sasa ukichanganya na hii ya kuua raia wasio na hatia huko Arusha,ni dhahiri huyu Mkwere analazimisha hasira za Muumba.Sintoshangaa siku mwanae,Ridhiwani nae akajitokeza kumpiga baba yake hadharani au Salma kuomba talaka (I know it's wishful thinking but anything goes)....

Kaka umepiga kichwa cha nyoka.

Need I say more?
 
Atavuna alichopanda. Mafisadi wataishia kumwachia vikapu vitupu naye atajaza humo mavuno yake. Aliyataka mwenyewe ashughulike nayo mwenyewe yeye alidhani ni lelemama. Nyerere alisema ukiingia ikulu waambie marafiki zako na jamaa zako ikulu ni mahala patakatifu sasa wewe ndugu yetu umegeuza ikulu ni nyumba ya genge la wahuni waporaji, wazulumaji, wauaji,majambazi etc.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom