Leo tarehe 2/9/2014 imetimia miaka miwili tangu mwandishi wa habari wa Channel ten Ndugu Mwangosi alipouawa kinyama na jeshi la polisi mkoani Iringa tarehe 2/9/2012, na baadaye kuzikwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Mwangosi aliuawa na polisi akitafuta habari kwenye mikutano midogo midogo ya CHADEMA iliyoandaliwa kwa ajili ya kufungua misingi na matawi ya chama.
Kutoka katika kutafuta habari akageuka yeye mwenyewe kuwa habari nzito iliyotikisa taarifa za habari za hapa nchini na nje ya mipaka ya nchi.
Ripoti za awali za polisi zilionyesha mauaji hayo yamefanywa na waandamanaji waliomrushia Mwangosi kitu chenye ncha kali.
Lakini picha za mauaji hayo ziliporushwa mitandaoni zilishtua wengi na kunyamazisha polisi kuficha ukweli wa mauaji hayo. Walionekana polisi wakifanya kitendo hicho bila huruma yoyote?
Taarifa niliyoipata leo jioni toka Wilayani Rungwe kwa Saimoni Mwaisope ni kwa kwamba, Leo mchana kutakuwa na mikusanyiko midogo ya kumbu kumbu ya mauaji ya kikatili ya Mwangosi (Iringa - Nyololo na Mbeya - Rungwe). Mwaisope amesema tunamkumbuka kwa kutafakari mambo mbali mbali ya husuyo kifo chake na mengineyo.
Mytake:
Nasi twaweza kuanza kutafakari jambo hili:
1. Kwa nini aliuawa?
2. Nani aliagiza?
3. Wauaji wako wapi?
4. Mjane na watoto wa marehemu wanaishije?
5. Kamuhanda yuko wapi? n.k.
PIA SOMA
- TANZIA - Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA
Mwangosi aliuawa na polisi akitafuta habari kwenye mikutano midogo midogo ya CHADEMA iliyoandaliwa kwa ajili ya kufungua misingi na matawi ya chama.
Kutoka katika kutafuta habari akageuka yeye mwenyewe kuwa habari nzito iliyotikisa taarifa za habari za hapa nchini na nje ya mipaka ya nchi.
Ripoti za awali za polisi zilionyesha mauaji hayo yamefanywa na waandamanaji waliomrushia Mwangosi kitu chenye ncha kali.
Lakini picha za mauaji hayo ziliporushwa mitandaoni zilishtua wengi na kunyamazisha polisi kuficha ukweli wa mauaji hayo. Walionekana polisi wakifanya kitendo hicho bila huruma yoyote?
Taarifa niliyoipata leo jioni toka Wilayani Rungwe kwa Saimoni Mwaisope ni kwa kwamba, Leo mchana kutakuwa na mikusanyiko midogo ya kumbu kumbu ya mauaji ya kikatili ya Mwangosi (Iringa - Nyololo na Mbeya - Rungwe). Mwaisope amesema tunamkumbuka kwa kutafakari mambo mbali mbali ya husuyo kifo chake na mengineyo.
Mytake:
Nasi twaweza kuanza kutafakari jambo hili:
1. Kwa nini aliuawa?
2. Nani aliagiza?
3. Wauaji wako wapi?
4. Mjane na watoto wa marehemu wanaishije?
5. Kamuhanda yuko wapi? n.k.
Mnamo mwezi Agosti na September 2012 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilifanya ziara ya ujenzi wa Chama (M4C) huko Mkoani Morogoro na Mkoani Iringa. Tarehe 02/09/2012 kulikuwa na ufunguzi wa Ofisi ya Chama katika Kijiji cha Nyololo. Polisi walizuia ufunguzi wa ofisi hiyo kinyume na taratibu na sheria kwa kisingizio cha kuendelea kwa zoezi la sensa ya watu na Makazi ambayo Kimsingi zoezi hilo lilikuwa limeisha na taasis na vyama vingine vya siasa vilikuwa vinaendelea na shughuli zao kama kawaida. Mathalani Chama cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa kinaendelea na kampeni huko Zanzibar.
CHADEMA tulisema agizo lile la kusitisha ufunguzi wa ofisi yetu halikuwa halali kwa sababu agizo la awali ilikuwa ni kusitishwa kwa mikutano ya hadhara peke yake na si mikutano ya ndani. Ufunguzi wa Ofisi yetu haikuwa mkutano wa hadhara. Polisi walijipanga kutumia nguvu kupita kiasi ambapo majira ya asubuhi waliwatangazia wananchi wasitoke nje wala kushiriki katika shughuli hiyo. Mchana ulipofika Viongozi na Wanachama wetu wakiongozwa na Mh. Benson Kigaila walifika eneo hilo la ofisi ambapo Polisi kwa upande wao wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa Michael Kamhanda waliamua kutumia nguvu kuvunja shughuli hiyo na hatimaye askari wapatao saba wakiwa na silaha za moto walimzingira na kumlipua Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten ndugu Daud Mwangosi kwa bomu na kumwaga utumbo palepale. Kwa kweli ilikuwa ni miongoni mwa matukio mabaya sana, na la kinyama kuwahi kutokea katika nchi yetu
Ndugu Wananchi Wenzangu leo ni takribani miaka miwili sasa imepita tangu kutokea kwa tukio hilo; hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali kwa wahusika, Kamanda Kamhanda bado yuko mtaani kana kwamba hakufanya chochote tena alipandishwa na cheo kabisa baada ya tukio lile. Askari aliyefunguliwa kesi ambaye hatumfahamu na hatawahi kuonekana na wananchi hatujui hata kesi yake hiyo imeishia wapi tayari yameshafunika kombe mwanaharamu apite kama walivyosema Wahenga wetu.
Sisi kama Chama kupitia Kamati Kuu yetu tuliitaka serikali kupitia Rais kuunda tume ya kijaji kuchunguza matukio haya ambayo tumekuwa tukifanyiwa na polisi ambapo wanachama na mashabiki wetu wanauawa bila hatia lakini serikali imeziba masikio na isitoshe mauaji yameendelea. Mtakumbuka kule Soweto Arusha ambapo polisi hao hao walitupa bomu kwenye mkutano wetu wa hadhara na kuua watu wengine wanne. Morogoro walimuua Ally Zona, Igunga akafa Mbwana Masoud, Arumeru alichinjwa ndugu Mbwambo na watuhumiwa wakakamatwa lakini tunaambiwa walitoroka wakiwa mikononi mwa Polisi tena wenye bunduki za SMG. Napenda kurudia tena kuitaka serikali iunde tume ya kimahakama ili Taifa lijue ukweli na uhakika wa nani hasa anahusika na mauaji haya ya watu wetu.
Ndugu Wananchi wenzangu wakati umefika wa sisi kupaza sauti zetu kwa nguvu kuungana na vilio vya damu za ndugu zetu hawa na mateso ambayo makundi mbalimbali yanapata bila hatia katika jamii yetu. Tunao ndugu zetu Albino wanakufa na hakuna anayechukua hatua, wengine wanateswa na kudhalilishwa wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama na sheria kisa tu eti hawakubaliani na Serikali. Hivi karibuni tumesikia wanavyofanyiwa Masheikh 19 walioko mahabusu, wanadhalilishwa sana kisaikolojia. Kuna vijana wetu walibakizwa kesi za ugaidi nao waliteswa na kuharibiwa sehemu za siri na jeshi la polisi. Imefika wakati sasa tuunganishe nguvu zetu kupambana na ukatili huu.
Napenda kuchukua fursa hii kutoa salam zangu za rambirambi kwa familia ya marehem Mwangosi na kwa wanahabari wote. Nawatia moyo wanahabari kuwa majasiri hususan wakati huu tunapoelekea katika chaguzi mbalimbali katika nchi yetu. Mwalimu Nyerere alisema ukishakula nyama ya mtu hutaacha hivyo tunatarajia kabisa Polisi na Watawala wataendeleza mauaji haya hasa watakapoona dalili za wao kunyanganywa dola lakini tusiogope tutashinda.
Dr.Wilbrod Slaa
Katibu Mkuu 02/09/2014
Leo ni siku ambayo kaka yetu mpendwa Daudi Mwangosi alifariki, Machungu ya kushambuliwa kwa kipigo, kisha kwa bomu na kikosi cha FFU huko mkoani Iringa katika eneo la Nyololo chini ya amri iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa wakati huo RPC Kamuhanda
Tunaweza kujifunza nini juu ya utashi wa viongozi wa dola la Tanzania katika utekelezaji wa sheria mbali mbali? Mimi sijui sana kama kweli tuna nia ya dhati ya kuwatoa wa Tanzania hapa walipo ili wayafikie maisha bora kwa kila mtanzania.
Kwa kuwa nilikuwepo siku ya tukio, nilishuhudia yote na kwa kuwa nilikuwa kiongozi wa chadema wakati huo. Ningeomba niwashirikishe machache juu ya tukio zima. nimeattach document ambayo, nimeiandika mimi mwenyewe kwa kutumia vithibitisho halali vya chama lakini pia vya jeshi la polisi. Mpango wangu ni kuandika kitabu. tutaendelea kuwasiliana pale inapobidi
Justin Mpotwa
Leo ni mwaka wa pili toka aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi auawe pale kijiji cha Nyororo Mufindi wakati akiwa katika kazi yake ya kuandika habari.
Serikali sikivu ya CCM japo imeoneshwa kila aina ya ushahidi imepuuza kuwachukulia hatua stahiki waliofanya ukatili huu.Tumeambiwa waliofanya ukatili huu wamepandishwa vyeo na watawala wetu wasikivu.
Dhihaka nyingi zimefanywa juu ya kifo hiki hata kufikia hatua ya mpiga propaganda Habibu Mchange kusema mauaji yalifanywa na CHADEMA.Anataka tuamini eti watu waliovalia sare za polisi tunaowaona kwenye picha ya mauaji ni CHADEMA na magwanda yao.
Familia yake na ndugu zake, IPC, UTPC na wadau wengine hawawezi kamwe kusahau mauaji ya Daudi Mwangosi kwani yalikua ni mauaji ya kinyama na ukatili wa hali ya juu.
Kuna kila dalili kwamba wauaji wameshajitangaza washindi hapa duniani.R.I.P Mwangosi.
PIA SOMA
- TANZIA - Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA