Kumbukumbu ya Brigedia Gen. Moses Nnauye!

Alikua ni muislam mdau,jina lake ni halisi ni Mussa Nnauye,Moses alijipa ili apate nafasi ya kusoma shule za mission enzi hizo walikua wanatakiwa kusoma kwenye shule hizo wakristo tu,wengi walibadili majina hata marehemu kighoma malima anaingia kwenye kundi hili!

kumbe ni kama alivyofanya Shaaban Robert enzi zile
 
Alikua ni muislam mdau,jina lake ni halisi ni Mussa Nnauye,Moses alijipa ili apate nafasi ya kusoma shule za mission enzi hizo walikua wanatakiwa kusoma kwenye shule hizo wakristo tu,wengi walibadili majina hata marehemu kighoma malima anaingia kwenye kundi hili!

Kwa hiyo hao jamaa kitimoto 'waliikamata' kama kawa. Aisee haya mamo ya imani kuna wakati mtu unasema wewe ni dini fulani kwa sababu ya jina tu lakini sio kiimani.
 
Hukupaswa kujibu hoja hiyo. BTW, ina maana hizo nyumba zimeshindwa kutoa/kufanya kumbukumbu ya pamoja kwa jambo kama hili, hivi kuna maasiliano kweli hapo?

Hamna mawasiliano....!kilamtu anauchungu wake na style yake ya kumlilia mpendwa wake
 
Picha hapo juu nimeitoa michuzi blog, mbona jina la Nape silioni katika members wa familia ya Nnauye? Naomba maelezo kwa wadau wenye taarifa sahihi
Kwa kumbukumbu zangu, wakati ule wa Ugomvi wake na akina Lowassa kuhusu Jengo la Umoja wa Vijana, Mke wa Marehemu Moses Nnauye alimkana kwamba si mtoto wa Marehemu na alianza kumwona baada ya Msiba wa Mzee Nnauye.
 
Kwa hiyo hao jamaa kitimoto 'waliikamata' kama kawa. Aisee haya mamo ya imani kuna wakati mtu unasema wewe ni dini fulani kwa sababu ya jina tu lakini sio kiimani.
"walikamata" kitimoto????wat u do mean?sijakunyaka wala nini kamanda,u wanna say wapagani woooote wanakamata kitimoto au?
 
Comrades,atleast lets be fair to the deceased,hayo mambo ya mwanae (Nnape) tumbebeshe mtoto rather than putting the budden kwa marehemu, Mapungufu na uozo wa Nape aubebe mwenyewe Nape na si baba.
Unafikiri anayo mapungufu yoyote basi?!! hamna ni siasa za maji taka tu za hawa watoto wa kiarusha waliojaa humu, wao kwao Nape tokea alivyokacha kujiunga na hicho chama chao cha kususa na kuandamana basi ndio imekua ni beef nae kwa kwenda mbele....

Zamani alikua shujaa wao humu ndani,anaebisha airejeshe ile thread ya Nape kuteuliwa ukuu wa wilaya uone mjione mlivyokuwa mkimpongeza na kumwita mpiganaji,nongwa ilianza pale alipoteuliwa kuwa katibu muenezi wa CCM. Jamaa eti wakataka katibu muenezi wa ccm afanye kazi za chama cha kususa na kuandamana! Haiwezekani nyie watoto! Mwisho wa siku tukubali kutokubaliana ili tusonge mbele!
 
Watu wa kukumbukwa kwenye hii nchi ni wawili tu, Nyerere na Sokoine University of Agriculture. Hao wengine ni wa kuwapotezea tu.

Mwita,
Nakumkumbuka huyu mzee kwasababu alikuwa mpenda mziki kwelikweli na yale mambo yetu yale....He was a good guy in his own ways, trust me, kwa hilo namuombea apumzike pema peponi. Ameni
 
Kwa kumbukumbu zangu, wakati ule wa Ugomvi wake na akina Lowassa kuhusu Jengo la Umoja wa Vijana, Mke wa Marehemu Moses Nnauye alimkana kwamba si mtoto wa Marehemu na alianza kumwona baada ya Msiba wa Mzee Nnauye.
Ule ulikua ni mchezo wa kitoto wa mzee makamba baada ya kushindwa kumnyamazisha Nape kuhusu hilo jengo jambo ambalo aliwaahidi kina lowassa kwamba nape wamuachie yeye kwa kuwa mwanae atamtuliza.

ndio mana makamba alipoanza kuropoka baada ya kumtumia yule mjane wa nyumba kubwa kwamba nape si mtoto wa mzee Nnauye,Nape aliwaambia waandishi waliomuuliza kwamba nasikia yeye sio mtoto wa moses nnauye,akawajibu wakamuulize makamba je yeye Nape alikua anaishi kwa mzee makamba na kina Januari, Ridhiwani na Mwamvita kama nani??

Waandishi walipomuuliza makamba hilo swali hakujibu, badala yake akamwita Nape wayamalize na kumtuliza zaidi akamtuma amuwakilishe kwenye mkutano mkuu wa chadema ambao makamba alialikwa pale sabasaba PTA hall, nyie watoto wa kiarusha mlikuwepo pale siku ile?
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Wakuu huu wimbo kama sikosei ulitungwa na kuimbwa na Moses Nnauye.
 
Wengi wa wanaomtuhumu Nape ni wale wanaogopa hata kivuli chake ,ni wale wenye virusi vya Ufisadi,mbona kabla ya mambo ya ufisadi na hata alipokuwa UVCCM yote hayo ya kumuita vuvuzela hatukusikia ,Nape ni kijana jasiri ukilinganisha na umri wake yuko tofauti na hao vijana wenu akina Malisa,Milya,Bashe n.k.
Kwa Nape Mzee Nnauye kazaa kidume ambacho kinaendeleza yale Mzee Nnauye aliyasimamia na kuyaamini
 
tena ndio mtoto pekee aliyerithi mikoba ya mzee kwa kuwa mzee aliwahi pia kuwa kwenye cheo alichonacho nape sasa!acheni wivu wa kike!
 
Alikua ni muislam mdau,jina lake ni halisi ni Mussa Nnauye,Moses alijipa ili apate nafasi ya kusoma shule za mission enzi hizo walikua wanatakiwa kusoma kwenye shule hizo wakristo tu,wengi walibadili majina hata marehemu kighoma malima anaingia kwenye kundi hili!

MOSSES kwa kiswahili ni MUSSA, ninaye rafiki ambaye mwanaye amebatizwa kwa jina la Mussa (ni mkatoliki)
 
Back
Top Bottom