Kumbukumbu ya Brigedia Gen. Moses Nnauye!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Ni miaka kumi sasa tangu ututoke mzee nnauye. Mapenzi yako yaliyotukuka kwa nchi yako yataendelea kukumbukwa milele. Ulikuwa amana ya Mungu kwa familia yako na taifa zima kiujumla, leo Mungu ameichukua amana hiyo toka kwetu, hatuna cha kulaumu bali kushukuru kwani kazi ya mungu haina makosa na kila nafsi itayaonja mauti, tulikupenda sana comrade lakini mapenzi yetu kwako hayakufua dafu mbele ya mapenzi ya mungu kwako.

Mke wako Mwanaisha, watoto wako Nape, Mariam, Joseph, Winnie, Mwate, Samora, Mussa na Bimdo wanakukumbuka na kukuombea sana kwa mungu. Wakwe zako January, Peter,Paul na Grace wanakukumbuka pia. Wajukuu zako Selemani, Adam, Otilia, Sanya, Kareen, Frank Jr wanakukumbuka pia.

Marafiki zako na watanzania kwa ujumla pia wanakukumbuka sana mzee Nnauye.

INNALILAAAHI WA INNAILAIHI RAAJIUUM!

BrigGenNnauyeKisw.jpg
 
Samahani sana wanafamilia wa mzee Nnauye, pamoja na wanajamvi wenzangu. Nina swali nataka kueleweshwa kidogo. Kuuliza si ujinga. Hivi huyu Marehemu Mzee wetu alikuwa dini gani?
 
Mzee ameacha kumbukumbu mbaya sana kwetu. Sio kwa yale aliyoyafanya kwa nchi yake bali kiumbe alichoacha kwenye familia yake. Ametuachia mtoto mwenye kiburi, kiziwi, mipasho, vuvuzela ambaye amekuwa mzigo kwa taifa ambalo baba huyu alikuwa kioo! Kama tatizo sio malezi yake basi ni hujuma na ushawishi wa mafisadi ndio vilimzidi nguuu mwanae.

Tutaendelea kumwombea mzee wetu huyu wakati tukiendelea kupambana na mafisadi waliomwaribu mwanae ili angalau afuate yale mema na mazuri aliyoyafanya baba'ake kwa nchi yetu.

R. I. P mzee Nnauye!
 
Samahani sana wanafamilia wa mzee Nnauye, pamoja na wanajamvi wenzangu. Nina swali nataka kueleweshwa kidogo. Kuuliza si ujinga. Hivi huyu Marehemu Mzee wetu alikuwa dini gani?

Alikua ni muislam mdau,jina lake ni halisi ni Mussa Nnauye,Moses alijipa ili apate nafasi ya kusoma shule za mission enzi hizo walikua wanatakiwa kusoma kwenye shule hizo wakristo tu,wengi walibadili majina hata marehemu kighoma malima anaingia kwenye kundi hili!
 
Mzee ameacha kumbukumbu mbaya sana kwetu. Sio kwa yale aliyoyafanya kwa nchi yake bali kiumbe alichoacha kwenye familia yake. Ametuachia mtoto mwenye kiburi, kiziwi, mipasho, vuvuzela ambaye amekuwa mzigo kwa taifa ambalo baba huyu alikuwa kioo! Kama tatizo sio malezi yake basi ni hujuma na ushawishi wa mafisadi ndio vilimzidi nguuu mwanae.

Tutaendelea kumwombea mzee wetu huyu wakati tukiendelea kupambana na mafisadi waliomwaribu mwanae ili angalau afuate yale mema na mazuri aliyoyafanya baba'ake kwa nchi yetu.
Answer:
Mbona kama umeongea kinyume mkuu,hao wanaoitwa mafisadi si maadui zake huyu au mafisadi gani pengine unaowazungumzia???labda na wewe un a tafsiri yako kuhusu ufisadi na mafisadi!
 
Picha hapo juu nimeitoa michuzi blog, mbona jina la Nape silioni katika members wa familia ya Nnauye? Naomba maelezo kwa wadau wenye taarifa sahihi

Lilisahaulika wakati taarifa inachapwa. Na miongoni mwa wakwe nimeona January, ni Makamba? Nape anashambuliwa sana hapa kuwa ni balaa tuliloachiwa na baba yake. Lakini ukweli ni kwamba huyu ni miongoni mwa watanzania wachache sana wenye ujasiri wa kusimama mbele ya mafisadi ndani ya chama chake cha mafisadi. Shutuma zote tunazomrushia zingeelekezwa kwa mwenyekiti wa chama chake.
 
Nape ni kiongozi jasiri sana,nashangaa wanaombeza
 
Lilisahaulika wakati taarifa inachapwa. Na miongoni mwa wakwe nimeona January, ni Makamba? Nape anashambuliwa sana hapa kuwa ni balaa tuliloachiwa na baba yake. Lakini ukwei kwamba huyu ni miongoni mwa watanzania wachache sana wenye ujasiri wa kusimama mbele ya mafisadi ndani ya chama chake cha mafisadi. Shutuma zote tunazomrushia zingeelekezwa kwa mwenyekiti wa chama chake.
Ni kitu gani kinachokufanya umuone Nape kama hapo kwenye Red? Ninachokiona ni kwamba huyu kijana ni "zao" la siasa za makundi na tabia ya "kulipuana" vyote vilivyoletwa na siasa za wanamtandao. Bado sijamuona kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia anachoamini. Swali ni kundi gani analolifanyia "uvuvuzela?". Angalizo kwake Nape " hakuna marafiki wala maadui wa kudumu katika siasa"
 
Samahani sana wanafamilia wa mzee Nnauye, pamoja na wanajamvi wenzangu. Nina swali nataka kueleweshwa kidogo. Kuuliza si ujinga. Hivi huyu Marehemu Mzee wetu alikuwa dini gani?

wakati anakaribia kufariki alibadili dini akahamia kwenye dini ya wana KAFU
 
Nape ni kiongozi jasiri sana,nashangaa wanaombeza

sielewi ujasiri wa Nape unatoka wapi! Nape alianza kusikika wakati akijiandaa kugombea uenyekiti wa UVCCM alipopigia kelele ushiriki mbovu wa EL kwenye ujenzi wa ghorofa la umoja wa vijana.

Kila mwenye akili timamu alijua Nepi anatumika kunufaisha kundi fulani hasimu kwa EL ktk mradi huo wa jengo la vijana. Baadae akadakia singo ya Slaa ya mafisadi ndan ya Mume wa KAFU.

Jk alipokurupuka na dhana ya kusadikika ya kujivua gamba na yeye Nepi akakurupuka kuzunguka nayo lakini kwa kuhakikisha anamkata makali EL. Sasa ujasiri wake ni upi wakati anafanya shughuli zake kwa misingi ya chuki na kukomoana akinufaisha makundi flan ya wanaotaka urais?
 
Picha hapo juu nimeitoa michuzi blog, mbona jina la Nape silioni katika members wa familia ya Nnauye? Naomba maelezo kwa wadau wenye taarifa sahihi

Ni ishara kwamba hata Wanafamilia hawampendi maana anawadhalilisha!
 
Binafsi namkumbuka Brigedia Mosses Nnauye kuliko hata ninavyomkumbuka Nyerere. Nnauye aliipenda sana nchi yake, alionyesha njia kwa wasanii wa nchi hii hasa kundi lake la TOT.
Brigedia Nnauye ni mtu wa kuheshimiwa sana, kwani hata wakati wa serikali ya Mwalimu na ya Mwinyi alionyesha wazi kuwa yeye ni mtu anayetetea ukweli mpaka mwisho.

Brigedia Nnauye angelikuwa hai akiwa na akili zake zile zile asingevumilia kuwa ndani ya chama cha majambazi akina jk!

Nyimbo:
sisi tunataka kuwasha mwenge,
Tunataka kuwasha mwenge,
umulike hata nje ya ya mipaka yetu
ulete tumaini.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom