Kumbe wapo watu ambo Kifikra bado wanatawaliwa na wakoloni.

Aug 21, 2016
33
504
Mwaka 1992 nilipokuwa nimemaliza masomo yangu Chuo kikuu cha Leeds Uingereza, nilienda nyumbani na nilimtembelea rafiki yangu huko kijijini ambae nae alikuwa amemaliza masomo yake huko Urussi. Baada ya kukaa kama saa moja hivi niliona hali ambayo ilinishangaza sana. Rafiki yangu huyu mara kwa mara katika maongezi alikuwa akichanganya lugha.

Mara aongee kirussi wakati wazazi wake hata Kiswahili kilikuwa cha shida. Mara aongee kingereza. Baadae ndugu zake na wazazi wake waliniuliza, mbona wewe unaongea kiswahili tu wakati na wewe umesoma ulaya kama wenzako ? Mimi nilinyamaza tu kwani hata mimi hali hiyo ilikuwa imenisikitisha sana.

Rafiki yangu huyu aliajiriwa kwenye Kiwanda cha bia huko Mwanza. Mimi niliajiriwa Kampuni ya Sukari kilombero. Baada ya muda mfupi nikaambiwa kwamba alitelemshwa cheo kutoka Mhandisi wa Kiwanda hadi Mhandisi wa kawaida na nafasi yake ilichukuliwa na kijana aliyekuwa na diploma ya kutoka Chuo cha Uhandisi Dar es salaam.

Nilipofuatilia niliambiwa kwamba hakuonyesha uwezo kama aliyemaliza mafunzo ya digrii, isipokuwa alikuwa na majigambo makubwa. Alijisikia sana na kuonyesha dharau kwa watanzania waliosoma Tanzania. Alitaka atambuliwe kama alisoma nje ya nchi Urussi na aliona fahari sana kuongea kirussi hata amabapo hapakustahili aongee kirussi.

Nilielezwa, alipoajiliwa, kwenye vikao alitaka aonekane amesoma Urussi. Mara kwa mara ajifanya kama amesahau hivyo anazungumza kirussi badala ya Kiswahili au kiingereza. Lakini kibaya zaidi uwezo wa kazi ukawa mdogo sana. Akashushwa cheo. Baadae akafukuzwa kazi.

Mkasa huu wa kweli naufananisha na watanzania ambao wanaona fahari sana kuongea kiingereza na wangependa hata Bunge letu litumie kiingereza badala ya lugha ya taifa ya Kiswahili. Siku moja niliona kwenye mitandao ya kijamii eti Breaking news: “Mwanasheria wa UKAWA awazidi mawakili wa serikali katika kujibu hoja kwa kiingereza”.

Siku nyingine nikaona tena Breaking news: Kwenye mkutano wa UN Tanzania haijawakilishwa na inaonekana UN wanatumia kiingereza siyo kiswahili..” Pia kuna vikatuni vya kijinga tu vimewekwa kwenye mitandao. Katika katuni hizo na breaking news hizo, ujumbe unaonekana ni kwamba watanzania hawa kuhawaoni fahari ya Lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili bali wanatukuza lugha ya kiingereza. Inasikitisha na ni aibu.

Nadhani wakati umefika, tuone fahari kwa viongozi wa kitaifa kutumia lugha ya Kiswahili wanapotembelewa na viongozi wa nchi za ulaya na marekani hapa nchini. Na wanapokwenda nje ya nchi wahutubie Kiswahili kwa sababu imekubalika kwenye UN na AU kiswahili kitumike. Nchi nyingi za Afrika zimeanza kujiandaa na hali hii.

Tanzania ndiyo chimbuko la Kiswahili lakini baadhi ya watanzania hawaoni fahari na lugha ya Kiswahili ambayo nchi nyingine za Afrika na ulaya na marekani wanatamani kuielewa kwa ufasaha.
Zipo nchi hazishabikii lugha ya kiingereza au lugha za kigeni na pia zimepiga hatua kimaendeleo. Mfano China, Korea, Japani, Urussi na Ujerumani.

Nchi hizi zinaheshimu lugha zake za asili, na wanapokwenda kwenye mikuatano ya kimataifa wanatumia lugha zao. Na wanaona fahari kufanya hivyo. Lakini hapa Tanzania kumbe wapo watu amabo kifikra bado wanatawaliwa na wakoloni. Wanaona fahari sana kuongea kiingereza. Na watamani hata Bunge litumie kiingereza na ofisi za serikali zitumuie kiingereza na hata hafla za kitaifa kitumike kiingereza.

Tatizo walilonao baadhi ya watanzania hawa ni fikra zilizokuwa zimepandikizwa wakati wa mkoloni kwamba ukijua kuongea kiingereza basi unaonekana msomi na umeendelea. Huo ni ulimbukeni kama aliokuwa nao yule rafiki yangu. Alijionyesha amesoma kwa kuongea kirussi mahali pasipostahili akadharau hata lugha yake, lakini baadae ikaonekana hata uwezo hakuwa nao.

Kwa mtu lugha ni mhimu katika kuwasiliana lakini mhimu sana kwa mtu ni kuwa na hekima, maarifa, ujuzi na busara katika kufanya maamuzi na uwezo wa kusimamia maamuzi hayo. Na kwa nchi ni hivyo pia. Nchi itapiga hatua kimaendeleo kama ina rasilimali watu wenye maarifa, ujuzi, viongozi wenye hekima na waliojitoa na wenye kufuatilia maamuzi yaani uongozi bora. Tanzania imeanza kusika duniani nkote kwa uongozi mahiri unaoonyeshwa na Raisi Magufuli. Ni kweli.
 
Miaka ishirini darasani bado hujui kiingereza acheni dharau huo ni umbumbumbu mbona wakenya hapo watoto wao tu wanaongea hii lugha ya malkia fresh? Daaa kuna siku nimekutana na mama alikua anauza mito ya kulalia sokoni anajua kingereza balaa na anadai alikuwa typwriter (mchapaji) sa unajiuliza unapataje PhD hujui kingereza ulichokitumia miaka yote shule? Hapo achana na hoja za lissu sijui wanasheria wa wapi sijui utumwa ukweli usemwee, Nyerere aliipenda lugha yetu ya kiswahili ila alijua kuna umuhimu kujua kiingereza na alikijuwa wala hakuwa na phd ,kiingereza ni lazima dunia ya sasa huwezi kiepukaaa kama ni utumwa basi tuache kla kitu kuanzia usafiri hizo ndege, nguo si vyao? Poor you
Mwaka 1992 nilipokuwa nimemaliza masomo yangu Chuo kikuu cha Leeds Uingereza, nilienda nyumbani na nilimtembelea rafiki yangu huko kijijini ambae nae alikuwa amemaliza masomo yake huko Urussi. Baada ya kukaa kama saa moja hivi niliona hali ambayo ilinishangaza sana. Rafiki yangu huyu mara kwa mara katika maongezi alikuwa akichanganya lugha. Mara aongee kirussi wakati wazazi wake hata Kiswahili kilikuwa cha shida. Mara aongee kingereza. Baadae ndugu zake na wazazi wake waliniuliza, mbona wewe unaongea kiswahili tu wakati na wewe umesoma ulaya kama wenzako ? Mimi nilinyamaza tu kwani hata mimi hali hiyo ilikuwa imenisikitisha sana.
Rafiki yangu huyu aliajiriwa kwenye Kiwanda cha bia huko Mwanza. Mimi niliajiriwa Kampuni ya Sukari kilombero. Baada ya muda mfupi nikaambiwa kwamba alitelemshwa cheo kutoka Mhandisi wa Kiwanda hadi Mhandisi wa kawaida na nafasi yake ilichukuliwa na kijana aliyekuwa na diploma ya kutoka Chuo cha Uhandisi Dar es salaam. Nilipofuatilia niliambiwa kwamba hakuonyesha uwezo kama aliyemaliza mafunzo ya digrii, isipokuwa alikuwa na majigambo makubwa. Alijisikia sana na kuonyesha dharau kwa watanzania waliosoma Tanzania. Alitaka atambuliwe kama alisoma nje ya nchi Urussi na aliona fahari sana kuongea kirussi hata amabapo hapakustahili aongee kirussi.
Nilielezwa, alipoajiliwa, kwenye vikao alitaka aonekane amesoma Urussi. Mara kwa mara ajifanya kama amesahau hivyo anazungumza kirussi badala ya Kiswahili au kiingereza. Lakini kibaya zaidi uwezo wa kazi ukawa mdogo sana. Akashushwa cheo. Baadae akafukuzwa kazi.
Mkasa huu wa kweli naufananisha na watanzania ambao wanaona fahari sana kuongea kiingereza na wangependa hata Bunge letu litumie kiingereza badala ya lugha ya taifa ya Kiswahili. Siku moja niliona kwenye mitandao ya kijamii eti Breaking news: “Mwanasheria wa UKAWA awazidi mawakili wa serikali katika kujibu hoja kwa kiingereza”. Siku nyingine nikaona tena Breaking news: Kwenye mkutano wa UN Tanzania haijawakilishwa na inaonekana UN wanatumia kiingereza siyo kiswahili..” Pia kuna vikatuni vya kijinga tu vimewekwa kwenye mitandao. Katika katuni hizo na breaking news hizo, ujumbe unaonekana ni kwamba watanzania hawa kuhawaoni fahari ya Lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili bali wanatukuza lugha ya kiingereza. Inasikitisha na ni aibu.
Nadhani wakati umefika, tuone fahari kwa viongozi wa kitaifa kutumia lugha ya Kiswahili wanapotembelewa na viongozi wa nchi za ulaya na marekani hapa nchini. Na wanapokwenda nje ya nchi wahutubie Kiswahili kwa sababu imekubalika kwenye UN na AU kiswahili kitumike. Nchi nyingi za Afrika zimeanza kujiandaa na hali hii. Tanzania ndiyo chimbuko la Kiswahili lakini baadhi ya watanzania hawaoni fahari na lugha ya Kiswahili ambayo nchi nyingine za Afrika na ulaya na marekani wanatamani kuielewa kwa ufasaha.
Zipo nchi hazishabikii lugha ya kiingereza au lugha za kigeni na pia zimepiga hatua kimaendeleo. Mfano China, Korea, Japani, Urussi na Ujerumani. Nchi hizi zinaheshimu lugha zake za asili, na wanapokwenda kwenye mikuatano ya kimataifa wanatumia lugha zao. Na wanaona fahari kufanya hivyo. Lakini hapa Tanzania kumbe wapo watu amabo kifikra bado wanatawaliwa na wakoloni. Wanaona fahari sana kuongea kiingereza. Na watamani hata Bunge litumie kiingereza na ofisi za serikali zitumuie kiingereza na hata hafla za kitaifa kitumike kiingereza.
Tatizo walilonao baadhi ya watanzania hawa ni fikra zilizokuwa zimepandikizwa wakati wa mkoloni kwamba ukijua kuongea kiingereza basi unaonekana msomi na umeendelea. Huo ni ulimbukeni kama aliokuwa nao yule rafiki yangu. Alijionyesha amesoma kwa kuongea kirussi mahali pasipostahili akadharau hata lugha yake, lakini baadae ikaonekana hata uwezo hakuwa nao.
Kwa mtu lugha ni mhimu katika kuwasiliana lakini mhimu sana kwa mtu ni kuwa na hekima, maarifa, ujuzi na busara katika kufanya maamuzi na uwezo wa kusimamia maamuzi hayo. Na kwa nchi ni hivyo pia. Nchi itapiga hatua kimaendeleo kama ina rasilimali watu wenye maarifa, ujuzi, viongozi wenye hekima na waliojitoa na wenye kufuatilia maamuzi yaani uongozi bora. Tanzania imeanza kusika duniani nkote kwa uongozi mahiri unaoonyeshwa na JPM. Ni kweli.
 
bila shaka umesoma uingereza na lugha hiyo unaielewa vizuri,mfumo wa elimu hapa nchini upoje?je waweza kufanya vizuri kwenye masomo bila kujua kingereza?kama hapana washauri wizara ya elimu waweze kuendesha masomo ya sekondari na chuo kwa kiswahili badala ya kingereza
 
Nchi za east africa zote zinaongea kiswahili plus another language cjui kwann hapa kwetu watu wanataka tuongee kiswahili tupu eti kuongea kiingereza ni kutukuza ukoloni...watanzania tuache uvivu jmn km kiingereza kigum bas tujifunze ht kichina
 
Mkuu umetoa elimu nzuri sana..

Ufanisi sio lugha ufanisi ni vitendo..

Unamsikia mtu eti kenya watoto wadogo tu wanaongea kingereza iweje msomi Tz ashindwe, yani wa Tz tuna hali mbaya sana ki fikra na mitazamo...

Lugha alie kwambia nikukaa darasani nani, mbona Tz mtoto mdogo tu anaongea kiswahili bila matatizo na shule hajaanza..
 
Kwa hili nakubaliana na mtoa mada, ipo haja ya kujivunia lugha yetu ya kiswahili, lakini licha ya hivyo pia iko haja ya kufahamu lugha ya kiingereza na hata lugha nyingine nyingi ili kuweza kuwasiliana na watu ambao hawaelewi kiswahili (hapa namaanisha marafiki/mtu mmoja mmoja).
 
Haya ndiyo matatizo anayoyaongelea mleta mada. Watanzania wengi hatuwezi kutumia lugha moja kwa ufasaha.

Mfano ni wewe! Hii lugha uliyotumia kuandika hapa haipo na wala haitambuliki.

Ni vyema kujifunza na kutumia lugha moja kwa ufasaha. Hii inatoa fursa kwa lugha ya kiswahili kueleweka zaidi kuliko lugha ya kigeni.
Watu tunatofautiana sana mitazamo
 
Angalau sasa hivi umeandika lugha moja kwa ufasaha.

Wewe mtazamo wako katika lugha ya kufundishia na mawasiliano ni nini?
Nashkuru umeelewa kuwa si kwamba siwez kuandika kiswahili kwa ufasaha bali ilikuwa ni uamuz kuchanganya lugha nazozielewa kuchangia kwenye jukwaa hili ambalo wengi wanazitambua lugha hizo,sasa ndugu unashauri hata watoto wetu tusiwafundishe kiingereza au kifaransa mpaka pale watakapoweza kuongea na kuandika kiswahili fasaha?rejea ulichojibu kwenye mchango wangu uliopita
 
Jaribu kupitia mchango wangu hapa chini.

Tatizo siyo matumizi ya lugha za kigeni, sababu ni maamuzi ya mtu binafsi kujifunza lugha anayotaka mwenyewe.

Jukumu lililopo ni kufanya kiswahili kuwa lugha inayotambulisha taifa katika shughuli za kiserikali.
Nmekupata mkuu hapo naunga mkono hoja
 
Mkuu umetoa elimu nzuri sana..

Ufanisi sio lugha ufanisi ni vitendo..

Unamsikia mtu eti kenya watoto wadogo tu wanaongea kingereza iweje msomi Tz ashindwe, yani wa Tz tuna hali mbaya sana ki fikra na mitazamo...

Lugha alie kwambia nikukaa darasani nani, mbona Tz mtoto mdogo tu anaongea kiswahili bila matatizo na shule hajaanza..
kama lugha ni kuongea tu na wala si kwenda darasani,niambie maneno haya kwa kiswahili fasaha "nipe chips na juice.
 
Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha za asili na za mataifa mbalimbali. Mifano Kifaransa champ = shamba, kireno mesa = meza, kijerumani schule = shule, kichina Chá = chai, kiingereza car = gari, nk.

Kuchanganya kiingereza na kiswahili huku hadhira inakuelewa sio utumwa bali kudumisha asili ya kiswahili. Kuna maneno yatabadilika na kuwa ya kiswahili moja kwa moja, hiyo itapelekea kupungua kuchanganya kiswahili na kiingereza kwa vizazi vijavyo.

Tuna upungufu wa misamiati na hiyo inayotungwa na bakita inadumaza kiswahili.

Anywayz, jitahidi kusifia magu atakuona.
 
Mwaka 1992 nilipokuwa nimemaliza masomo yangu Chuo kikuu cha Leeds Uingereza, nilienda nyumbani na nilimtembelea rafiki yangu huko kijijini ambae nae alikuwa amemaliza masomo yake huko Urussi. Baada ya kukaa kama saa moja hivi niliona hali ambayo ilinishangaza sana. Rafiki yangu huyu mara kwa mara katika maongezi alikuwa akichanganya lugha.

Mara aongee kirussi wakati wazazi wake hata Kiswahili kilikuwa cha shida. Mara aongee kingereza. Baadae ndugu zake na wazazi wake waliniuliza, mbona wewe unaongea kiswahili tu wakati na wewe umesoma ulaya kama wenzako ? Mimi nilinyamaza tu kwani hata mimi hali hiyo ilikuwa imenisikitisha sana.

Rafiki yangu huyu aliajiriwa kwenye Kiwanda cha bia huko Mwanza. Mimi niliajiriwa Kampuni ya Sukari kilombero. Baada ya muda mfupi nikaambiwa kwamba alitelemshwa cheo kutoka Mhandisi wa Kiwanda hadi Mhandisi wa kawaida na nafasi yake ilichukuliwa na kijana aliyekuwa na diploma ya kutoka Chuo cha Uhandisi Dar es salaam.

Nilipofuatilia niliambiwa kwamba hakuonyesha uwezo kama aliyemaliza mafunzo ya digrii, isipokuwa alikuwa na majigambo makubwa. Alijisikia sana na kuonyesha dharau kwa watanzania waliosoma Tanzania. Alitaka atambuliwe kama alisoma nje ya nchi Urussi na aliona fahari sana kuongea kirussi hata amabapo hapakustahili aongee kirussi.

Nilielezwa, alipoajiliwa, kwenye vikao alitaka aonekane amesoma Urussi. Mara kwa mara ajifanya kama amesahau hivyo anazungumza kirussi badala ya Kiswahili au kiingereza. Lakini kibaya zaidi uwezo wa kazi ukawa mdogo sana. Akashushwa cheo. Baadae akafukuzwa kazi.

Mkasa huu wa kweli naufananisha na watanzania ambao wanaona fahari sana kuongea kiingereza na wangependa hata Bunge letu litumie kiingereza badala ya lugha ya taifa ya Kiswahili. Siku moja niliona kwenye mitandao ya kijamii eti Breaking news: “Mwanasheria wa UKAWA awazidi mawakili wa serikali katika kujibu hoja kwa kiingereza”.

Siku nyingine nikaona tena Breaking news: Kwenye mkutano wa UN Tanzania haijawakilishwa na inaonekana UN wanatumia kiingereza siyo kiswahili..” Pia kuna vikatuni vya kijinga tu vimewekwa kwenye mitandao. Katika katuni hizo na breaking news hizo, ujumbe unaonekana ni kwamba watanzania hawa kuhawaoni fahari ya Lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili bali wanatukuza lugha ya kiingereza. Inasikitisha na ni aibu.

Nadhani wakati umefika, tuone fahari kwa viongozi wa kitaifa kutumia lugha ya Kiswahili wanapotembelewa na viongozi wa nchi za ulaya na marekani hapa nchini. Na wanapokwenda nje ya nchi wahutubie Kiswahili kwa sababu imekubalika kwenye UN na AU kiswahili kitumike. Nchi nyingi za Afrika zimeanza kujiandaa na hali hii.

Tanzania ndiyo chimbuko la Kiswahili lakini baadhi ya watanzania hawaoni fahari na lugha ya Kiswahili ambayo nchi nyingine za Afrika na ulaya na marekani wanatamani kuielewa kwa ufasaha.
Zipo nchi hazishabikii lugha ya kiingereza au lugha za kigeni na pia zimepiga hatua kimaendeleo. Mfano China, Korea, Japani, Urussi na Ujerumani.

Nchi hizi zinaheshimu lugha zake za asili, na wanapokwenda kwenye mikuatano ya kimataifa wanatumia lugha zao. Na wanaona fahari kufanya hivyo. Lakini hapa Tanzania kumbe wapo watu amabo kifikra bado wanatawaliwa na wakoloni. Wanaona fahari sana kuongea kiingereza. Na watamani hata Bunge litumie kiingereza na ofisi za serikali zitumuie kiingereza na hata hafla za kitaifa kitumike kiingereza.

Tatizo walilonao baadhi ya watanzania hawa ni fikra zilizokuwa zimepandikizwa wakati wa mkoloni kwamba ukijua kuongea kiingereza basi unaonekana msomi na umeendelea. Huo ni ulimbukeni kama aliokuwa nao yule rafiki yangu. Alijionyesha amesoma kwa kuongea kirussi mahali pasipostahili akadharau hata lugha yake, lakini baadae ikaonekana hata uwezo hakuwa nao.

Kwa mtu lugha ni mhimu katika kuwasiliana lakini mhimu sana kwa mtu ni kuwa na hekima, maarifa, ujuzi na busara katika kufanya maamuzi na uwezo wa kusimamia maamuzi hayo. Na kwa nchi ni hivyo pia. Nchi itapiga hatua kimaendeleo kama ina rasilimali watu wenye maarifa, ujuzi, viongozi wenye hekima na waliojitoa na wenye kufuatilia maamuzi yaani uongozi bora. Tanzania imeanza kusika duniani nkote kwa uongozi mahiri unaoonyeshwa na Raisi Magufuli. Ni kweli.
Umeongea kitu cha msingi sana mheshimiwa, Watanzania wengi tunakoelekea fikra za kikoloni zitaongezeka sana , mtu anaona ufahali sana kuongea LUGHA YA KIGENI hasa kiingereza , kwa nini tusijivunie lugha yetu , wasomi wa siku hizi nao wanaona kuitwa profesa, doctor ndo fahari unakuta mtu makaratasi yake yanaonyesha anaelimu nzuri kumbe kichwani zero , siku hizi elimu imekuwa pesa yako chochote utakacho utapata kena kwa mda muafaka , NInampongeza Raisi kwa kukienzi kiswahili chetu, haina haja ya kutumia kiingereza mbona wao wakija kwetu wanatumia lugha yao , ufanisi wa lugha siyo kigezo cha uongozi ila Busara, Maarifa vinahitajika sana .tuwe wazalendo jamani.
 
..vipi inapotokea kiongozi wa nchi anaboronga hata lugha ya taifa lake?

..kwasababu "mtu fulani" hata kiswahili anachozungumza si cha kupigiwa mfano.

..halafu "mtu fulani" ana tabia ya kuchanganya kiswahili na kiingereza. Je, hiyo inakubalika?

cc Fred Mpendazoe
 
Back
Top Bottom