Kumbe Wabunge wa Upinzani hawawakilishi wananchi Bungeni?

MANAMBA

Senior Member
Jan 16, 2011
169
16
Kwa muda mrefu kila nikifuatilia vipindi vya bunge inatokea nakutana na wabunge wa CCM wakiponda hoja za wabunge wa upinzani, kwa mtazamo wangu kuponda hoja ya mtu mwingine si tatizo ila kinachonishangaza na kukera ni pale wapondaji hao wanapojinadi kuwa wao wanawakilisha mawazo ya wapiga kura wao!

Sasa swali langu ni kama wabunge wa CCM wanajiona kuwa wanawakilisha majimbo yao, iweje wabunge wa upinzani waonekane kama wanajiwakilisha wenyewe na siyo majimbo yao?

Nadhali kuna haja kwa mheshimiwa spika kukemea hali hii kwa faida ya democrasia ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom