Kumbe USWAZI Noumaaa namna hii

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
562331_393469984010899_1195685899_n.jpg
 
Sasa mpaka choo tunataka kwa msaada wa watu wa Marekani?

Tungekuwa na barabara nzuri, tukafika kazini mapema, tungeweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi; hiyo peke yake kwa namna nyingi ingeweza kutuongezea kipato, au tungetoka kazini na kufika nyumbani mapema, tungeweza kupata muda wa kupumzika na hivyo bongo zetu kufanya kazi vizuri zaidi, hapo tungepata fursa ya kuweza kufikiri nje ya kasha.

Kama umewahi kupanda daladala au kupita karibu na vituo vya daladala hasa asubuhi na jioni, utakubaliana na mimi kwamba kwa aina ile ya usafiri ukifika huko unakokwenda, lazima uwe umeshachanganyikiwa... hebu angalia wanafunzi wanavyopata shida, wengine wanapanda mpaka malori...

Hatukaki msaada kujengewa choo, tunataka mazingira bora yatakayotuwezesha kufanya shughuli zetu kwa ufanisi zaidi ili tupate pesa nyingi zaidi hata tukila zinabakia kidogo tunajengea choo. Kama hiyo ingewezekana nina hakika tunaotumia hivi vyoo tungekuwa wachache sana.
 
Huu ni unyanyasaji wa ki-ghorofia ! utajengaje ghorofa wakati majirani zako wana nyumba za kawaida na vyoo vya passport size?
 
Mh jaman vyoo kama hivo hata haja zako hufanyi kwa raha eti

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom