Kumbe US Dollar itashuka thamani duniani hivi punde!!

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Nimeduazwa na kampeni za Obama na Romney kwenye mbio za kuelekea IKULU ya Marekani hivi juzi kwenye mdahalo wao wa pili. Obama na Romney yeyote atakaepita sera yake ya kwanza ni kurudisha viwanda Marekani ili wamarekani wapate ajira. Viwanda vingi vya Marekani vilihamishishiwa bara la Asia kwasababu thamani ya USDollar ni kubwa mno inayofanya gharama za uzalishaji ziwe kubwa mno Marekani, hivyo wenye viwanda walikimbilia China, India, Singapore, Japan, Africa kutafuta faida. Baada ya Marekani kushindwa kuishawishi China iongeze thamani ya fedha yake sasa wana mkakati wa kuishusha thamani ya dollar yao ili kuvutia uwekezaji na wamarekani walioikimbia nchi kibiashara kurudisha mitaji yao ya viwanda nchini mwao. Kwasasa Marekani haina viwanda kabisa, ukifika pale Detroit mji ambao ulikuwa chimbuko la viwanda duniani sasa hivi yamebaki magofu tu watu pia wameukimbia mji na majumba yao kwa kukosa ajira. Nikiwanda cha kutengeneza magari ya FORD tu ndicho bado kikubwa kilichobakia pale. Mkakati mwingine wa kukuza uchumi wao ni kuanza kuchimba mafuta na gesi yao wenyewe badala ya kuagiza bidhaa hizo ng'ambo. Hivyo, bei ya mafuta duniani nayo itashuka miserably kwakua mnunuzi mkubwa atabakia China na India tu. Kama Obama atapita atapunguza matumizi ya kijeshi kwa kupunguza ukubwa wa jeshi na kuacha vita Afghanstan. Hivyo nawapa tahadhali watu wanaoiabudu sarafu ya US$ kuwa kuweni chonjo msije mkapata hasara ghafla punde dola inaposhuka kufuatia mabadiliko ya kiuchumi yanayotarajiwa kufanywa marekani baada ya uchaguzi wa NOvemba.
 
Labda hili litarudisha heshima ya Shilling yetu ambayo hata serikali ya Tanzania inaisahau kwa kuabudu dollar
 
I think the day the dollar will loose its sole supremacy as the transaction currency in the world market,then its value will start dropping but before then bado sana
 
Sababu kubwa inayopelekea wafanyibiashara wa Kimarekani kuhamishia viwanda vyao nchi za Asia ni gharama ya uzalishaji. Hapa Marekani miminum wage nadhani ni dola $7.50 wakati nchi za Asia unaweza kuwalipa wafanyikazi dola moja kwa saa na hizo zikaonekana kuwa hela nyingi za mshahara. Uzuri wa kushushwa kwa thamani ya dola ni kwamba bidhaa ambazo bado zinazalishwa Marekani, zitakuwa na bei rahisi katika masoko ya nje, hasa masoko ya Ulaya, na itawavutia watalii wa kigeni, hasa kutoka nchi tajiri, kama vile Ulaya na Japan, kutembelea Marekani. Unakuta viwanda vikubwa kama Nike vinawalipa wafanyikazi wake chini ya dola moja kwa saa halafu wanauza viatu vya Nike katika maduka ya Marekani kuanzia dola $60 kwenda juu. Lakini all in all, hata kama dola itashuka thamani, tusitegemee kwamba shilingi ya Tanzania automatically itapanda thamani. Hiyo ni dynamic nyingine kabisa.
 
Yule waziri aliyeibiwa baada ya kuwa na changudoa ataanza kubeba euro zitokanazo na kodi zetu!!
 
Nimeduazwa na kampeni za Obama na Romney kwenye mbio za kuelekea IKULU ya Marekani hivi juzi kwenye mdahalo wao wa pili. Obama na Romney yeyote atakaepita sera yake ya kwanza ni kurudisha viwanda Marekani ili wamarekani wapate ajira. Viwanda vingi vya Marekani vilihamishishiwa bara la Asia kwasababu thamani ya USDollar ni kubwa mno inayofanya gharama za uzalishaji ziwe kubwa mno Marekani, hivyo wenye viwanda walikimbilia China, India, Singapore, Japan, Africa kutafuta faida. Baada ya Marekani kushindwa kuishawishi China iongeze thamani ya fedha yake sasa wana mkakati wa kuishusha thamani ya dollar yao ili kuvutia uwekezaji na wamarekani walioikimbia nchi kibiashara kurudisha mitaji yao ya viwanda nchini mwao. Kwasasa Marekani haina viwanda kabisa, ukifika pale Detroit mji ambao ulikuwa chimbuko la viwanda duniani sasa hivi yamebaki magofu tu watu pia wameukimbia mji na majumba yao kwa kukosa ajira. Nikiwanda cha kutengeneza magari ya FORD tu ndicho bado kikubwa kilichobakia pale. Mkakati mwingine wa kukuza uchumi wao ni kuanza kuchimba mafuta na gesi yao wenyewe badala ya kuagiza bidhaa hizo ng'ambo. Hivyo, bei ya mafuta duniani nayo itashuka miserably kwakua mnunuzi mkubwa atabakia China na India tu. Kama Obama atapita atapunguza matumizi ya kijeshi kwa kupunguza ukubwa wa jeshi na kuacha vita Afghanstan. Hivyo nawapa tahadhali watu wanaoiabudu sarafu ya US$ kuwa kuweni chonjo msije mkapata hasara ghafla punde dola inaposhuka kufuatia mabadiliko ya kiuchumi yanayotarajiwa kufanywa marekani baada ya uchaguzi wa NOvemba.

Usidanganyike mno na wanasiasa. Marekani ilishaweka mikakati hiyo muda mrefu kwa kuweka utaratibu wa bidhaa kubwa zinazouzwa nchini Marekani uzalishaji ufanyike nchini Marekani badala ya Marekani kuwa big import wa bidhaa za kigeni duniani.
Ukitaka kuwa na soko kubwa Marekani, unatakiwa uanzishe kiwanda nchini mwao ambapo kutainufaisha Marekani, au kampuni inayoonyekana kuingiza bidhaa zake kwa wingi by law itatakiwa kufungua kiwanda nchini Marekani kwa sababu ya kuvuka kiwango cha uingizaji bidhaa zake ambapo marekani itanufaika kama ifuatavyo:
  • Utalazimika kuajiri wafanyakazi wamarekani ili kupunguza tatizo la ajira
  • Wataalamu wa Marekani watahakikishiwa kutumika katika viwanda mfano kama Kampuni ya Nissan car assemble, ina viwanda kadhaa moja wapo kikiwa kiwanda kikubwa nchini Marekani kupita viwanda vya nissan Japan, na hivyo Administration ni ya Nissani lakini makampuni yaliyofilisika katika viwanda vya magari vya marekani ndiyo yenye tenda ya kuunda magari ya nissan kujihakikishia benefits zinawanufaisha wamarekani. Viwanda vya magari ya kijapani Marekani ni pamoja na Toyota, Nissan, Honda, Mazda, Mitsubish, Suzuki, Hyundai, etc.
  • Kodi za kibiashara zinainufaisha Marekani.
  • Export ya bidhaa inahesabiwa ni ya Kimarekani wakati makampuni hodhi ni ya kigeni.
  • Makampuni ya kigeni Marekani yanatozwa kodi kubwa kuliko makampuni ya nyumbani.
  • Viwanda vitabaki na dhana ya kiwanda cha kigeni na kupata kibali cha kuendesha biashara ndani ya ardhi ya Marekani na kuweka kibao kinachoonyesha: "You are entering foreign trade zone."
  • Na mengine mengi inabidi kuwaelewa kwa kina hawa jamaa, maana mambo yao yanayohusu ujanja wa kuvujisha uchumi wa nchi nyingine ufurikie Marekani hawataweza kuweka wazi, ni siri zao.
  • Wakati huo huo mashirika makubwa ya fedha duniani yako huko Marekani na ndio wamiliki, UN ni rubber stump tu.

Mikakati hali hiyo naijua, chama kizuri cha kisiasa kitakaposhika dola nitakipa mbinu ya kudeal na mataifa ya kigeni kuanzisha viwanda nchini kwani manufaa yake ni makubwa.

Tatizo la kutokusoma uchumi.Hujui hata maana ya kushusha thamani dolla.Pili fuatilia kila uchaguzi unaposogea dolla huwa inakuwaje,Swala la ajila lipo kote China hali ni mbaya sana hata uchumi wao umeshuka sasa kwa miezi kama minne.Elewa uchumi siku zote sio Static
 
Ninachopenda viongozi wa hizi nchi zilizoendelea wako very strategically na ni rahisi mno wao kujitathmini na kuona mapungufu yao.......sio huku kwetu
 
Soon itakuwa 1$ = 1Tsh.

Unaota ndoto? Kwa nini Japana pamoja na export ya bidhaa za dhamani kubwa duniani lakini pesa yake ingali inatambaa chini? Kwa nini wanafanya hivyo? Mashirika ya fesha duninia yako wapo na yanahodhiwa na nani?
 
Kwa hiyo itachukua muda gani kufikia 1Tsh = 1$?
 
Sababu kubwa inayopelekea wafanyibiashara wa Kimarekani kuhamishia viwanda vyao nchi za Asia ni gharama ya uzalishaji. Hapa Marekani miminum wage nadhani ni dola $7.50 wakati nchi za Asia unaweza kuwalipa wafanyikazi dola moja kwa saa na hizo zikaonekana kuwa hela nyingi za mshahara. Uzuri wa kushushwa kwa thamani ya dola ni kwamba bidhaa ambazo bado zinazalishwa Marekani, zitakuwa na bei rahisi katika masoko ya nje, hasa masoko ya Ulaya, na itawavutia watalii wa kigeni, hasa kutoka nchi tajiri, kama vile Ulaya na Japan, kutembelea Marekani. Unakuta viwanda vikubwa kama Nike vinawalipa wafanyikazi wake chini ya dola moja kwa saa halafu wanauza viatu vya Nike katika maduka ya Marekani kuanzia dola $60 kwenda juu. Lakini all in all, hata kama dola itashuka thamani, tusitegemee kwamba shilingi ya Tanzania automatically itapanda thamani. Hiyo ni dynamic nyingine kabisa.

Basi walau irudi kama zamani 1USD = 5 TZS !! :thinking:
 
Tatizo la kutokusoma uchumi.Hujui hata maana ya kushusha thamani dolla.Pili fuatilia kila uchaguzi unaposogea dolla huwa inakuwaje,Swala la ajila lipo kote China hali ni mbaya sana hata uchumi wao umeshuka sasa kwa miezi kama minne.Elewa uchumi siku zote sio Static

Mr. President hueleweki, unamaana gani? hufai kuwa mwl. hata wa familia yako hawatakuelewa pia
 
Ninachopenda viongozi wa hizi nchi zilizoendelea wako very strategically na ni rahisi mno wao kujitathmini na kuona mapungufu yao.......sio huku kwetu

Mnachagua viongozi vilaza wasiojua kujitathmini!!
 
Back
Top Bottom