Kumbe umeme upo wa kumwaga?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
ukisoma hapo kwenye underlined sijui utaelewa nini

Wafanya kazi na wizara
Wafanya kazi katika mkutano huo walitaja mambo waliyodai ni kero kwao na yanayoangamiza Shirika hilo ikiwamo mikataba ya kuuziana umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo.

Mmoja wa wafanyakazi hao, Kamil Mwalangwa kutoka kituo cha kuzalisha umeme wa Mega watts 100 alisema:
"Katika kituo cha Mg 100 kuna makundi manne yanayonunua gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme,Kampuni ya Tegeta,Simbion, Songas na sisi Tanesco,lakini sisi bei tunayouziwa ni kubwa tofauti na wenzetu,nini sababu inayotufanya tununue kwa bei ya juu?alihoji na kuongeza:
"Mheshimiwa Waziri pamoja na kununua kwa bei hiyo wakati mwingine sisi huamuriwa kuzima mashine zote ili kampuni nyingine ziweze kuzalisha na kuuza umeme na maagizo haya hutoka ngazi za juu"alisema Mwalangwa huku akishangiliwa na wafanya kazi wengine.
Alisema kwa sasa muda wa matengezo wa injini zinazofanya kazi katika eneo hilo umepita na shirika halina vifaa vya ziada (spea)wala fedha za kununulia jambo alilodai ni hatari na wakati wowote mitambo hiyo inaweza kuzima na kuongeza tatizo la umeme nchini.
Mwalangwa litaja tatizo jingine litakalolikumba Shirika hilo kuwa ni kuharibika kwa mitambo kutokana na kuwasha na kuzima kila wakati kwa lengo la kupisha mitambo ya kampuni nyingine kuwasha mitambo yao na kuuza umeme.
Alison Mwambaga mmoja wa wafanyakazi wa Tanesco , alipendekeza kwa waziri huyo mwenye dhamana kufuta mikataba yote mibovu ukiwamo wa IPTL kwa kuwa ndiyo inayoliangamiza shirika hilo na Taifa kwa jumla.
article yote hii hapa
Profesa Muhongo: Nimekuta ‘madudu' ya kutisha Tanesco Send to a friend
Monday, 21 May 2012 08:11
0digg

Geofrey Nyang'oro
WAZIRI wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amemkaanga mtangulize wake akisema baadhi ya madudu aliyoyakuta katika wizara hiyo ni makubwa ambayo hawezi kuyasema hadharani.
Profesa Muhongo ni miongoni mwa Mawaziri wapywa walioteuliwa Mei 3, mwaka huu kushika wadhifa katika baraza jipya la mawaziri ambapo kabla ya uteuzi huo aliteuliwa kuwa mbunge kupitia viti maalum na Rais.
Profesa Muhongo mwenye taaluma ya Jiolojia alitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akizunguza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika mkutano wao uliofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wafanya kazi walitaja mambo kadhaa yanayolifanya shirika hilo kushindwa kujiendesha kuwa ni pamoja na mikataba mibovu iliyoingiwa na Serikali kwa Kampuni ya kufua umeme na vitendo vya baadhi ya watendaji wizarani ambao hujihusisha na hujuma dhidi ya shirika hilo.

Akijibu hoja mbalimbali za wafanya kazi alisisitiza kuwa, suala la mikataba mibovu iliyoingia na Serikali inajulikana na wananchi wote lakini akasema hata yeye alipoingia wizarani amekuta mambo mabaya ambayo hawezi kuyasema hadharani.

"Ninyi mnazunguzia mikataba mibovu na mnataka tuifute,wafanyakazi wa Tanesco ni watu waliokwenda shule tuongee vitu vinavyowezekana,ile ni mikataba….siyo kwamba mimi natetea mikataba mibovu yapo mambo niliyoyakuta huku ni makubwa hata mimi siwezi kuyasema hadharani"alisema Muhongo na kuongeza:
"Suala la mikataba huwezi kulibadilisha kwani imeshatufunga , Serikalini nne zimeingia mikataba,awamu ya kwanza ya pili ya tatu na hata ya nne, sisi katika awamu yetu tunawaahidi hatuwezi kuingia mikataba mibovu ndio sababu nikagusia kuwa mimi kama waziri siwezi kusaini mkataba wowote unaohusu umeme bila kushirikisha Tanesco,TPDC" alisema Muhongo.

Profesa Muhongo pia alitaja mambo mengine aliyodai ameyakuta wizarani na kuyafanyia kazi katika kipindi kifupi cha siku 18 alizokaa kwenye wadhifa huo kuwa ni pamoja na suala la uhusiano mbovu baina ya wafanya kazi wa wizara hiyo,Samico, Tanesco na TPDC ambapo kila upande unafanya kazi kivyake na kushutumu upande mwingine.
"Nimekuta hakuna ushirikiano baina ya Wizara,TPDC,Samico na ninyi Tanesco,mbaya zaidi kila upande unatupia lawama upande mwingine,nimenza kwa kulifanyika kazi hilo na kuanzia sasa sisi wote ni timu moja kazi yetu ni kuhakiksha tunatoa huduma bora ya umeme kwa watanzania"alisema Muhongo.
Muhongo alisema yeye ameshaanza kazi na moja ya mambo aliyoyafanya ni kurejesha rasimu ya mapendekezo ya muswada wa kurekebisha sheria ya umeme iliyokuwa imeandaliwa bila kushirikisha pande zote zinazohusika na masuala ya umeme ikiwamo Tanesco na TPDC.
"Kuanzia sasa pale wizarani kila kitu kitakuwa wazi,mimi sitasaini mkataba wowote bila kuwashirikisha ninyi,sitaruhusu vitendo vya hujuma na mtu yeyote wala kuruhusu kutungwa kwa sheria bila ya kuwashirikisha"alisema Muhongo.
Kuhusu jitihadi za kutafuta ufumbuzi suala la umeme alisema, kesho Jumanne Maofisa kutoka TPDC,Tanesco na Wazara ya Madini wanatarajia kukutana na Naibu waziri wa Nishati ya umeme , George Simbachewene kujadili na kuandaa mkakati wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme nchini.
Alitaka wataalamu wa umeme kujadili namna ya kulitoa Taifa katika mtindo wa kutegemea chanzo kimoja cha umeme wa maji na badala yake kuangazia vyanzo vingine ambavyo ni makaa ya mawe na gesi.
Pia waziri huyo alitaja vyanzo vingine kuwa ni umeme wa upepo,Jiothramu na jua ambao alisema vyanzo hivi vikitumika vizuri vitalisaidia taifa.
Katika mkutano huo pia Waziri huoaliwatangazia neema ya kupatikana kwa gesi katika shirika hilo aliposema bombo la kusafirisha gesi linalojengwa kwa sasa ni mali ya serikali.
"Ninachotaka mimi tuache yote yaliyopita kwani tukijikita kushughulika na hayo tunaweza kushindwa kutekeleza hii mipango tuliyojiwekea,hivi sasa bomba la gesi linalojengwa ni mali ya serikali lakini pia Mgodi wa Kiwira taratibu za kuurejesha serikalini zimekamilika na utakuwa chini ya Samico"alisema Muhongo.
Kuhusu mikataba alisema hatua za kufanyia marekebisho mikataba hiyo, zinaendelea ndani ya wizara kama ilivyofanyika kwa ile ya madini ambayo kwa sasa inalipa asilimia 4 ya mirabaha badala ya asilimia tatu ya awali.

Waziri huyo alitaja pia hatua ambazo wizara imefanya kwa sasa kuwa ni kupitia na kubaini namna Kampuni zilivyoingia na kufanya kazi ya kusafirisha gesi ambapo alisema, kuna kampuni nyingi zinazofanya kazi hiyo.
Wafanya kazi na wizara
Wafanya kazi katika mkutano huo walitaja mambo waliyodai ni kero kwao na yanayoangamiza Shirika hilo ikiwamo mikataba ya kuuziana umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo.

Mmoja wa wafanyakazi hao, Kamil Mwalangwa kutoka kituo cha kuzalisha umeme wa Mega watts 100 alisema:
"Katika kituo cha Mg 100 kuna makundi manne yanayonunua gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme,Kampuni ya Tegeta,Simbion, Songas na sisi Tanesco,lakini sisi bei tunayouziwa ni kubwa tofauti na wenzetu,nini sababu inayotufanya tununue kwa bei ya juu?alihoji na kuongeza:
"Mheshimiwa Waziri pamoja na kununua kwa bei hiyo wakati mwingine sisi huamuriwa kuzima mashine zote ili kampuni nyingine ziweze kuzalisha na kuuza umeme na maagizo haya hutoka ngazi za juu"alisema Mwalangwa huku akishangiliwa na wafanya kazi wengine.
Alisema kwa sasa muda wa matengezo wa injini zinazofanya kazi katika eneo hilo umepita na shirika halina vifaa vya ziada (spea)wala fedha za kununulia jambo alilodai ni hatari na wakati wowote mitambo hiyo inaweza kuzima na kuongeza tatizo la umeme nchini.
Mwalangwa litaja tatizo jingine litakalolikumba Shirika hilo kuwa ni kuharibika kwa mitambo kutokana na kuwasha na kuzima kila wakati kwa lengo la kupisha mitambo ya kampuni nyingine kuwasha mitambo yao na kuuza umeme.
Alison Mwambaga mmoja wa wafanyakazi wa Tanesco , alipendekeza kwa waziri huyo mwenye dhamana kufuta mikataba yote mibovu ukiwamo wa IPTL kwa kuwa ndiyo inayoliangamiza shirika hilo na Taifa kwa jumla.
 
huu mi nauita ushenzi, haiwezekani unikataze nisizalishe eti nikuache uniuzie kwa bei kubwa. Afu muuzaji wa hiyo gas ni nani wakuu?
 
Please tell me what is wrong with us. Some people have reached a stage that even their conscious can no tell them what is right and what is wrong. These People are not supposed to be called human being but evil human being. If you are among them please just call yourself evil human being because what you doing is beyond human understanding. Mr. President, you can not help us to get rid of these people using all the power you are given by constitution. It means all these have not reached your table? or you have just ignored. We are crying for our motherland, when our land is going to be liberated from the hands of these evil people. When our Most high God will bring another Mosses who can go and tell Pharaoh that God has said I want my people out of bondage. Let us stand together for the future for our nation and our children.
 
Ten perecenti izi zitakuja tutokea puani!
Na hii monopoly ya Pan African Energy ikome hawawezi tuuzie gas kwa gharama ivyo wakati wanachimba kwenye ardhi yetu na huu uhuni wa kusubortage bomba jipya la gesi tushawastukia.Likikamilika mtakula gasi yenu otherwise mubadilike maana hao waliokuwa wanakula izo perecenti wengi washatoka kuweni na huruma
 
namkumbuka marehemu Edward moringe sokoine, enzi zake wahusika wote wangeishia magerezani
 
dah..haya maneno mazito mkuu.hapa naweza kusema tu kuwa kidumu chama cha mapinduzi

Saint Ivuga kwa sauti kubwa tunasema kidumuuuu
Na zidumu fikra za Mwenyekiti ambazo always ni sahihi
Na tutaendelea kukichagua milele na milele ili kiendelee kula ten percent zetu
Kidumuuuuu
 
Saint Ivuga kwa sauti kubwa tunasema kidumuuuu
Na zidumu fikra za Mwenyekiti ambazo always ni sahihi
Na tutaendelea kukichagua milele na milele ili kiendelee kula ten percent zetu
Kidumuuuuu

kidumuuuuuuuuu
ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeee
mtoni kijichi wanakatiwa umeme hatz mara tano kwa siku yaani wao kuanzia januari hadi desemba ila wamechagua ccm.....

Ccm oyeeeeeeeeeeee
kidumu kidumu kidumu chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom