GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 306
Baada ya Hitimisho la leo la kuapishwa kwa Rais aliyeshinda kwenye uchaguzi Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE ( Japokuwa mgombea wa Cahama fulani hakutokea eti amesusa, ila wenzake wala yeye akisusa) , kinacho fuatia sasa ni kuchagua baraza makini la mawaziri. Na kwa vile mpaka sasa CCM ina jumla ya wabunge 186 wa kuchaguliwa ( ukiacha wale wa viti maalum) itakuwa na hazina kubwa ya kuchagua baraza bora. Tunamuombea Rais wetu afya njema aweze kulitumikia Taifa, kwani ridhaa aliyopewa na watanzania ya ushindi wa kishindo wa 61.17% (wengine wanauita USHINDI WA SUNAMI). Uchaguzi umekwisha, tusonge mbele na tugange yajayo.