Kumbe ukiukwaji wa maadili ulianza kipindi cha j.k.nyerere?

KISOSORA

Member
Jan 14, 2011
34
0
Nilisoma jana thread ya kilichomtoa Kikwete Monduli,Mwandishi wa thread hiyo alionesha hisia zake kwa kile alichokiita kuwa aliondoka kwa aibu kubwa kutokana na kumchongea bosi wake.
Mimi nilivyofuatilia vizuri mjadala huu nikaona kuwa Kikwete alichofanya alitekeleza wajibu wake kumfahamisha Raisi kuwa kuna ukiukwaji wa taratibu kwani JWTZ ni chombo cha uma,hakiwezi mtu tu kwa kuwa ni bosi aanze kuliuzia jeshi bila ya Kuomba tenda ambayo imetangazwa kiuwazi kwa Watanzania wote ili washindane katika kutaka kuliuzia jeshi.
Nyerere kwa kusema nendeni mkamalizane wenyewe inanitia shaka kwamba aliridhia hali hiyo ya kuchanganya utumishi na kufanya biashara au la.
Pia nilitarajia kuona kama katika makala ile Nyerere amefuatilia kutaka kujua kama wameyamaliza vipi ili ajue kama kulikuwa na uadilifu au la.
Mwisho nawauliza wana JF kama Nyerere aliridhia hali hii ya mkuu wa kambi kubwa kama ya Monduli kufanya BIASHARA ya kuliuzia JWTZ bidhaa zake ni sawa au?
NAWASILISHA.
 
Mkuu Kisosora, tuwekee Sheria ya manunuzi ya wakati huo ili tuisome na kuweza kuijadili vizuri hoja yako.
 
Jibu swali nililouliza kwenye mada kwanza.
Pia nawaalika wale wazee waliokuwepo kipindi hicho watuambie kama sheria ya manunuzi ili kuwepo au la.
 
Alichokifanya JK ni Umbea na unafiki na majungu kwani alipaswa aulize ndani ya uongozi na viongozi wenzake kama alikua anahujumu jeshi au la na kama alikua akisaply kwa bei za halali na kwa kiwango kinacho kubalika alikua na haja gani ya kuwaruka viongozi wenzake na kwenda direct kwa mkuu wa nchi. Pia sio ajabu taratibu zote za kumpa kazi hiyo ilifanyika na iliridhiwa na jeshi na pia mkuu wa nchi alikua anafahamu, hivyo baada ya kuona kijana mdogo analeta fitina akaona amuumbue. pia nawashauri msiwe wakukurupuka bila kufuata chanel za uongozi kamahujaridhika na jambo. be informed Kisosora
 
Nilisoma jana thread ya kilichomtoa Kikwete Monduli,Mwandishi wa thread hiyo alionesha hisia zake kwa kile alichokiita kuwa aliondoka kwa aibu kubwa kutokana na kumchongea bosi wake.
Mimi nilivyofuatilia vizuri mjadala huu nikaona kuwa Kikwete alichofanya alitekeleza wajibu wake kumfahamisha Raisi kuwa kuna ukiukwaji wa taratibu kwani JWTZ ni chombo cha uma,hakiwezi mtu tu kwa kuwa ni bosi aanze kuliuzia jeshi bila ya Kuomba tenda ambayo imetangazwa kiuwazi kwa Watanzania wote ili washindane katika kutaka kuliuzia jeshi.
Nyerere kwa kusema nendeni mkamalizane wenyewe inanitia shaka kwamba aliridhia hali hiyo ya kuchanganya utumishi na kufanya biashara au la.
Pia nilitarajia kuona kama katika makala ile Nyerere amefuatilia kutaka kujua kama wameyamaliza vipi ili ajue kama kulikuwa na uadilifu au la.
Mwisho nawauliza wana JF kama Nyerere aliridhia hali hii ya mkuu wa kambi kubwa kama ya Monduli kufanya BIASHARA ya kuliuzia JWTZ bidhaa zake ni sawa au?
NAWASILISHA.

umbea unauita uwajibikaji???
 
Back
Top Bottom