Kumbe Tamko La "Wasomi" Ni Fake

My Take:

Natoa wito kwa viongozi wa wanafunzi, kufanya mambo yao kwa kuzingatia utaratibu waliojiwekea badala ya kufanya mambo wao binafsi na kudai kuwa ni mawazo ya wote. Kufanya hivyo ni kuwadhalilisha wanafunzi ambao katika suala husika lilotolewa tamko limeligawa taifa wakiwepo wanafunzi wenyewe ambao ni wapenzi wa vyama na itikadi mbalimbali.

QED
Hii CCM sasa sijui ni urithi gani inaviachia vizazi vijavyo...................yaani hata viongozi wa wanafunzi sasa ni magwiji wa kuchakachua.............tutafika kweli?
 
Na hao wawakilishi wa vyombo vya habari wanakwenda tu kichwa kichwa hawahakikishi utambulisho wa mtoa habari inakuwaje?Yaani mtu anajipachika uwakilishi wa vyuo nyie hata hamuwezi kugundua. Embu naomba waandishi wa habari mtueleze hili linatokeaje kama sio uzembe wa kupitiliza.Hii ni aibu kwa profession ya uandishi.

Hili linanikumbusha ule mkasa wa balozi wa kijiji cha Kyoruba kule Musoma aliekwenda safari bongo na kupokelewa kwa hadhi zote za kibalozi jamaa wakidhani nio balozi anyewakilisha nchi ya Kyuba. Jamaa alikula kuku wiki nzima mpaka alipomaliza shughuli zake na kurudi Kyoruba....:whoo::whoo:
 
UDSM bana.....yaani huyo Punch kazi yake ilikuwa/ ni kufuatilia maisha ya watu tu....kaazi kweri kweri

Ingawa Mzee Punch alikuwa na maapungufu mengi, lakini alisaidia sana kuwaweka "Governometer" wale waliojisahau na kufanya chuo kama danguro. Sasa hivi vyuo vingi inasemekana wengi wanashindana kufanya maovu.

Enzi za Mzee Punch hata the so called maksi za "C#UP!" hazikuwepo, maana ikigundulika tu, next day utakuwa kwenye the so called "Literature Wall"
 
hata viongozi wa nchi waliadhibiwa na Mzee pale walipokose...... Mzee Ruksa ..... anajua... aliwahi kuambiwa "akili yake kama nyumba ya msonge"
 
Hili linanikumbusha ule mkasa wa balozi wa kijiji cha Kyoruba kule Musoma aliekwenda safari bongo na kupokelewa kwa hadhi zote za kibalozi jamaa wakidhani nio balozi anyewakilisha nchi ya Kyuba. Jamaa alikula kuku wiki nzima mpaka alipomaliza shughuli zake na kurudi Kyoruba....:whoo::whoo:

Duh! JF bana kiboko!

Asante Mkuu kwa kunifanya nicheke.
 
Jamani kuna yeyote humu anaweza akaniletea huyo mtoto aliyeandaa huo waraka?
Nina mazungumzo naye.
WARAKA ULINDALIWA UWT NA AKATAFUTWA KIJANA WA KUJIFANYA MWANAFUNZI KUUSOMA KWA NIABA YA WANANFUNZI. BAADA YA CHADEMA KUPIGA BAO LAKISIGINO, UWT WAMEPEWA KAZI YA KUHAKIKISHA CHADEMA HAPATULII ILI WASIWEZE KUPANGA MIPANGO KAMA ILI KUDHOOFISHA VUGUVUGU LA KUDAI KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGZUI.

AJENDA YA KWANZA WALIYOANZA NAYO NI KUFUFUA MNYUKANO KATI YA ZITTOvs MBOWE. UDHAIFU WANAOUTUMIA NI MAPUNGUFU YA MHE ZITTO KUTOA KAULI ZA KUCHANGANYA KATIKA FECEBOOK, VYOMBO VYA HABARI N.K

HATA THREAD NYINGI ZINAZOANZISHWA JF ZINA MWELEKEO HUO. TUNATAKIWA KUTOKA SASA TUWAPUUZE NA THREAD ZAO ZA KIPUUZI NA TUCONCENTRATE NA THREAD ZENYE KUWEZA KULETA MAPINDUZI YA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI.

KILA ATAKAYEKUWA AKIANZISHA UPUUZI WAKE KWANZA TUMHOJI MSIMAMO WAKE BINAFSI KUHUSU AJEDA HIZO MBILI
 
Punch alikuwa mharibifu tu wa maisha ya watu. kuna dada kwenye miaka ya mwisho ya 80 au 90 mwanzoni alijiua kwa sababu ya huyo Punch wenu.
 
WARAKA ULINDALIWA UWT NA AKATAFUTWA KIJANA WA KUJIFANYA MWANAFUNZI KUUSOMA KWA NIABA YA WANANFUNZI. BAADA YA CHADEMA KUPIGA BAO LAKISIGINO, UWT WAMEPEWA KAZI YA KUHAKIKISHA CHADEMA HAPATULII ILI WASIWEZE KUPANGA MIPANGO KAMA ILI KUDHOOFISHA VUGUVUGU LA KUDAI KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGZUI.

Mkuu, unaweza kutuhabarisha kwa uhakika kuhusu hili?
 
Punch alikuwa mharibifu tu wa maisha ya watu. kuna dada kwenye miaka ya mwisho ya 80 au 90 mwanzoni alijiua kwa sababu ya huyo Punch wenu.

True. Alikuwa anaitwa Levina Mukasa. Na hapo ndipo kifo cha Mzee Punch kilipotokea.
 
Hiyo barua hapanshaka watakuwa wamei-design akina 'Sheka' (anajijua na ID zake lukuki kama hayawani) na trupu lake wakishirikiana na huyo mganga njaa..wala sikupoteza muda wangu kusoma huo upupu.
 
Mkuu, unaweza kukupa details zaidi kuhusu hoja yako?
 
True. Alikuwa anaitwa Levina Mukasa. Na hapo ndipo kifo cha Mzee Punch kilipotokea.

attachment.php

Mnamo mwezi Februari mwaka jana wakati mwanafunzi wa kike wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipojiua, watu wengi walifikiri kuwa alifanya hivyo kwa sababu alikuwa na matatizo kwao na kama masomo yalikuwa yanamshinda. Hata hivyo, waliposikia kwamba alifanya hivyo kutokana naunyanyawaji wa kijinsia uliofanywa na wanafunzi wawili wa Kitivo cha Uhandisi pamoja na kikundi kilichojukana kama "Punch", baadhi walikasirika wakati wengine walicheka tu.

Marehemu Levina Mukasa, alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza aliyekuwa akisomea shahada ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulingana na maelezo ya waliokuwa wakimfahamu wanasema alikuwa mkimya mwenye msaada na ambaye wakati wote alikuwatayari kutumia vitu vyake na wenzake. Kila aliposoma wakati wote alishika nafasi ya juu darasani.

Mnamo tarehe 7 Februari 1990, Levina alikatisha maisha yake kwa kumeza vidonge vingi vya klorokwini (vinavyotumika kutibu Malaria). Swali linabaki, "kwa nini alifanya hivyo?"

Karibu kila mwanafunzi wa kike aliyesoma katika kampasi kuu ya Chuo Kikuu (inayojulikana sana kama Mlimani) atakuwa amenyanyaswa kijinsia katika kipindi cha Miongo miwili iliyopita. Wamekuwa wakidhihakiwa, kutishiwa kijinsia au kuvamiwa papo kwa hapo na kubakwa.

Pamoja na hayo lipo kundi la kisirisiri hapo mlimani linajukana sana kama PUNCH, linafikia hata kiwango cha kuchapisha maandishi na michoro michafu kuhusu habari za kimapenzi za sasa au za zamani za Mhasirika wao.

Source: http://african.lss.wisc.edu/swahili/swahili_4/lessons/lesson8/lesson8_makala_1.htm
 
Attachments

  • hayati_levina.jpg
    hayati_levina.jpg
    29.2 KB · Views: 18,770
attachment.php

Mnamo mwezi Februari mwaka jana wakati mwanafunzi wa kike wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipojiua, watu wengi walifikiri kuwa alifanya hivyo kwa sababu alikuwa na matatizo kwao na kama masomo yalikuwa yanamshinda. Hata hivyo, waliposikia kwamba alifanya hivyo kutokana naunyanyawaji wa kijinsia uliofanywa na wanafunzi wawili wa Kitivo cha Uhandisi pamoja na kikundi kilichojukana kama "Punch", baadhi walikasirika wakati wengine walicheka tu.

Marehemu Levina Mukasa, alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza aliyekuwa akisomea shahada ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulingana na maelezo ya waliokuwa wakimfahamu wanasema alikuwa mkimya mwenye msaada na ambaye wakati wote alikuwatayari kutumia vitu vyake na wenzake. Kila aliposoma wakati wote alishika nafasi ya juu darasani.

Mnamo tarehe 7 Februari 1990, Levina alikatisha maisha yake kwa kumeza vidonge vingi vya klorokwini (vinavyotumika kutibu Malaria). Swali linabaki, "kwa nini alifanya hivyo?"

Karibu kila mwanafunzi wa kike aliyesoma katika kampasi kuu ya Chuo Kikuu (inayojulikana sana kama Mlimani) atakuwa amenyanyaswa kijinsia katika kipindi cha Miongo miwili iliyopita. Wamekuwa wakidhihakiwa, kutishiwa kijinsia au kuvamiwa papo kwa hapo na kubakwa.

Pamoja na hayo lipo kundi la kisirisiri hapo mlimani linajukana sana kama PUNCH, linafikia hata kiwango cha kuchapisha maandishi na michoro michafu kuhusu habari za kimapenzi za sasa au za zamani za Mhasirika wao.

Poor her.

Asante kwa habari hii.

Huyo 'Punch' ni mbaya sana.
 
Poor her.

Asante kwa habari hii.

Huyo 'Punch' ni mbaya sana.

Kipindi cha Mzee Punch kijana kama THOBIAS MWESIGA RICHARD asingeachwa hivi hivi . . . . Angekuwa Kwishnei . . . Maana Mzee Punch katika uhalisia wake hakubagua japo kuna habari kuwa anasadikiwa alifungamana sana na wanafunzi wa Engineering.
 
Mzee Punch angekuwepo asingethubutu . . . .

Kuna binti tulikuwa nae UDSM somebody @sh@ ambaye aliendekeza sana masuala ya ngQnQ. Ingawa sikuunga mkno lakini Mzee Punch alimuumbua sana. Kisha baba yake akatumiwa cheti cha kufuzu masomo ya ngQnQ chenye sahihi ya makamu mkuu wa chuo. Mzee libidi aje UDSM kumhoji makamu mkuu wa chuo iweje binti kafuzu masomo tena katika fani ambayo siyo iliyompeleka kusomea?

Sasa huyu dogo, tumfunze tu kwamba maisha hayaendi hivyo.

Hembu tujuze, wenzako tulikuta hiyo kitu pUNCH imeshaondoka, ilikuwa inafanyaje kazi? na kwa nini iliondoka?
 
Ingawa Mzee Punch alikuwa na maapungufu mengi, lakini alisaidia sana kuwaweka "Governometer" wale waliojisahau na kufanya chuo kama danguro. Sasa hivi vyuo vingi inasemekana wengi wanashindana kufanya maovu.

Enzi za Mzee Punch hata the so called maksi za "C#UP!" hazikuwepo, maana ikigundulika tu, next day utakuwa kwenye the so called "Literature Wall"

nimesoma enzi ambazo punch alishafariki. Kwa stor nlizowah kuckia kuhusu punch, angerud angesaidia kunyoosha wasomi bubu
 
Jamani kuna yeyote humu anaweza akaniletea huyo mtoto aliyeandaa huo waraka?
Nina mazungumzo naye.

Mkuu, naweza kujiwekea picha kichwani mwangu kwamba utakua umefadhaishwa na huyu kijana Msomi wa Dodoma kwa kiasi gani, lakini chonde msamehe bure kwani mpaka sasa huko aliko atakua anajihisi jehanamu tangu chuoni, mkoani Dodoma hadi kijijini kwao.

Hata hivyo mkuu, ukimya wa UDOM na vyuo vikuu vya huko Dodoma kutokulaani TAMKO FEKI ile, wala Wahadhiri wao kutokusema japo hata neno nalo ni shida kidogo. Hilo ni kwa sababu hatuelewi kwamba ndio kusema kwa lugha ya miili yao kwamba yote yaliosemwa jamii ielewe kwamba ni ukweli na ukweli mtupu au hapana.

Naomba kuwashilisha .
 
Back
Top Bottom